Uhamiaji: Dereva na V8 Iliyobeba wahamiaji Haramu 20 wa Ethiopia Isihusishwe na CCM

Baada ya Dereva Mtanzania Edward Erihard (31) Mkazi wa Dodoma kukamatwa akiwa amebeba Wahamiaji 20 Raia wa Ethiopia katika gari aina ya Land Cruiser V8 likiwa na bendera ya Chama cha Mapinduzi CCM katika eneo la Minjingu mkononi Manyara, Kamishna Msaidizi wa Uhamiaji Mkoani Manyara Philon Kyetema leo amesema gari hilo, bendera pamoja na Dereva havina uhusiano wowote na Chama cha Mapinduzi.

“Gari lilikuwa na mlingoti na baada ya kufunuliwa ikakutwa bendera inayofanana na bendera ya Chama cha Mapinduzi maana yake ni kwamba huyu bwana Edward alijiandaa kuhadaa Vyombo vya ulinzi na usalama ili visimtie nguvuni lakini tunashukuru Askari Polisi wa Minjingu waliweza kumtilia shaka na kuzuia gari na ndani kukuta Wahamiaji hao 20, kesho tutawafikisha Mahakamani”

“Naomba kufafanua kwa Watanzania ninaomba wasihusishe gari hilo na bendera inayoonekana kwenye gari hilo haina uhusiano na Chama Tawala cha CCM, hilo gari lenyewe, bendera yenyewe pamoja na Dereva hawana uhusiano na Chama cha Mapinduzi”

Source: Millard Ayo
Gari mali ya mwenyekiti wa ccm ilala
 
Taarifa ya Awali: Asafirisha wahamiaji 20 kwa V8 yenye bendera ya CCM
Nashauri wabadilishe waweke ya Chadema ili isiwe nongwa waseme ya Chadema chama ambacho si tawala.
 
Kuna taarifa inasambaa mitandano kutoka kwa Kamishina wa Uhamiaji mkoa wa Manyara alijulikana kwa jina Kyetema akidai yakuwa hakuna uhusiano kati ya Gari, Dereva na Bendera ya CCM ya mtumiwa wa kusafirisha waethopia 20.

Kyetema kwa nini unatema nyongo hisiyotemeka?

Hivi kwa gari hiyo ungekuta bendera ya chadema ingekuaje?

Aliyekamatwa ni kada mtiifu wa CCM na amekuwa akifanya biashara hiyo miaka mingi

Sema juzi kajifanya kujitia wazimu lakini hakuanza leo hata hiyo cruza ni zao la biashara hiyo.
 
Baada ya Dereva Mtanzania Edward Erihard (31) Mkazi wa Dodoma kukamatwa akiwa amebeba Wahamiaji 20 Raia wa Ethiopia katika gari aina ya Land Cruiser V8 likiwa na bendera ya Chama cha Mapinduzi CCM katika eneo la Minjingu mkononi Manyara, Kamishna Msaidizi wa Uhamiaji Mkoani Manyara Philon Kyetema leo amesema gari hilo, bendera pamoja na Dereva havina uhusiano wowote na Chama cha Mapinduzi.

“Gari lilikuwa na mlingoti na baada ya kufunuliwa ikakutwa bendera inayofanana na bendera ya Chama cha Mapinduzi maana yake ni kwamba huyu bwana Edward alijiandaa kuhadaa Vyombo vya ulinzi na usalama ili visimtie nguvuni lakini tunashukuru Askari Polisi wa Minjingu waliweza kumtilia shaka na kuzuia gari na ndani kukuta Wahamiaji hao 20, kesho tutawafikisha Mahakamani”

“Naomba kufafanua kwa Watanzania ninaomba wasihusishe gari hilo na bendera inayoonekana kwenye gari hilo haina uhusiano na Chama Tawala cha CCM, hilo gari lenyewe, bendera yenyewe pamoja na Dereva hawana uhusiano na Chama cha Mapinduzi”

Source: Millard Ayo

Taarifa ya Awali: Asafirisha wahamiaji 20 kwa V8 yenye bendera ya CCM
Huyo kamishna naye asilete siasa uchwara hapo,yeye azungumzie yanayohusu uhamiaji hayo mengine awaachie CCM wenyewe na polisi. Mwenye gari ni kiongozi wa CCM na bendera ni ya CCM.
IMG-20240325-WA0040.jpg
 
Back
Top Bottom