Zanzibar 2020 Uhalali wa Hussein Mwinyi kugombea Urais Zanzibar ni upi? Wajumbe tuelewesheni

Shocker

Member
Sep 15, 2012
94
400
Kuna hoja kubwa ambayo imeivunja CCM miguu na mikono kiasi ya kuwa hawawezi kusimama wala kutembea.

Dkt. Hussein Mwinyi hana sifa za kugombea Urais Zanzibar na kama haitoshi walio ndani ya innercore wanasema hakushinda kura za wajumbe wa CCM Zanzibar kiasi ya wasimamizi kuondoka Zanzibar bila ya kuwataja walioshinda, zilienea habari za redio kifua tu, lakini CCM hawakutoa majina ya walioshinda, walienda kuwatajia Dodoma.

Sababu inayoelezwa ni kuwa waliopendekezwa na kutakiwa na CCM hakuwemo hata mmoja na yale baadhi ya majina yaliotangazwa na kamati kuu ya CCM ndipo alipochomekwa Hussein Mwinyi. Kamati ilitegemea kupata uungwaji mkono jambo ambalo halijatokea hadi sasa, kwa maana CCM Zanzibar mara hii wamesema dharau ya kudharauliwa imevuka mipaka, kikwao wanasema imefurutu ada.

Wamesikika watu wakisema Hussein hana au hakidhi vigezo vya Katiba ya Zanzibar inakuwaje hapo? Upinzani hawakuliona hilo na kuweza kuweka pingamizi, ZEC nao hawakuliona hilo na wao kuweka pingamizi?

Je, akitokea mwanasheria anaejiamini na kupinga mahakamani ukiukwaji huu wa katiba ya Zanzibar, atakuwa amefanya kosa? Wazanzibari walio wengi wanampinga Hussein kwa dhahiri na kwa siri kiasi ya kuonyesha wote wameungana na kuwa kitu kimoja na sio kumpinga Hussein la hasha wanaipinga CCM kwa kuwa inawapoka haki yao ya kuchagua kiongozi wanemtaka.

Na sasa CCM sio inawakandamiza wapinzani kuwapindulia na kuwabadilishia matokeo, sasa hadi ndani ya CCM. CCM Zanzibar hawana ubavu wa kuamua lolote wapo wapo tu, ZEC ilipindua matokeo 2015 dhidi ya CUF, leo hii wanapinduana wenyewe kwa wenyewe.

Je, Hussein Mwinyi ameletwa ili kutekeleza kuelekea serikali moja na kisha akale bata Tanganyika.
 
impongo

JF-Expert Member
Feb 18, 2015
7,926
2,000
Tunakoelekea Zanzibar itakuwa mkoa wa Pemba na unguja na Hussein atachaguliwa kuwa Raisi wa Tanzania (neno muungano tutalitoa) 2025 mwinyi ni Raisi ajaye wa Tanzania
 
Sesten Zakazaka

JF-Expert Member
Sep 10, 2017
9,439
2,000
Mkuu Wazanzibari wasikushughulishe saana akili. Hawana msimamo hasa Waunguja. Wakati wa Bunge la katiba wajumbe wanaotoka Zanzibar walikubaliana kwa kauli moja wakaupiganie mfumo wa Muungano wa serikali tatu ambao walidai utaipa nchi yao hadhi inayostahili katika Muungano

Baada ya kufika Dodoma sijui nini kilitokea! Pande moja la Wajumbe kutoka Zanzibar likageuka na kuanza kupingana na msimamo wao wa awali waliokubaliana tangia wapo Visiwani!!! Nakumbuka Ismail Jusa alitoa kauli maarufu ya "Mbona tulikubaliana sasa wenzetu kufika Dodoma mmeufyata?" Marehemu Asha Bakari akamwambia "Shika adabu yako, mimi nimeshaufyatua mara kadhaa na nimezaa watoto, wewe ni rijali kweli hata mke huna!!!?"

Hata aliyekuwa mwanasheria wao mkuu Bwana Othman Masoud ni kama aliuzwa kwa kile kitendo cha wajumbe kubadili msimamo walipofika Dodoma na akajikuta anapoteza kazi yake kwa kupiga kura ya wazi kuunga mkono muundo wa serikali tatu jambo ambalo hakika walikua wamekubaliana awali!!+
 
okiwira

JF-Expert Member
Jul 23, 2018
1,562
2,000
Tunakoelekea Zanzibar itakuwa mkoa wa Pemba na unguja na Hussein atachaguliwa kuwa Raisi wa Tanzania (neno muungano tutalitoa) 2025 mwinyi ni Raisi ajaye wa Tanzania
Hii sound ni kama mzee ruksa ndan ya uchumi wa mkapa.
 
Malcom XX

Member
Sep 12, 2020
81
150
Kuna hoja kubwa ambayo imeivunja CCM miguu na mikono kiasi ya kuwa hawawezi kusimama wala kutembea.

Dkt. Hussein Mwinyi hana sifa za kugombea Urais Zanzibar na kama haitoshi walio ndani ya innercore wanasema hakushinda kura za wajumbe wa CCM Zanzibar kiasi ya wasimamizi kuondoka Zanzibar bila ya kuwataja walioshinda, zilienea habari za redio kifua tu, lakini CCM hawakutoa majina ya walioshinda, walienda kuwatajia Dodoma.

Sababu inayoelezwa ni kuwa waliopendekezwa na kutakiwa na CCM hakuwemo hata mmoja na yale baadhi ya majina yaliotangazwa na kamati kuu ya CCM ndipo alipochomekwa Hussein Mwinyi. Kamati ilitegemea kupata uungwaji mkono jambo ambalo halijatokea hadi sasa, kwa maana CCM Zanzibar mara hii wamesema dharau ya kudharauliwa imevuka mipaka, kikwao wanasema imefurutu ada.

Wamesikika watu wakisema Hussein hana au hakidhi vigezo vya Katiba ya Zanzibar inakuwaje hapo? Upinzani hawakuliona hilo na kuweza kuweka pingamizi, ZEC nao hawakuliona hilo na wao kuweka pingamizi?

Je, akitokea mwanasheria anaejiamini na kupinga mahakamani ukiukwaji huu wa katiba ya Zanzibar, atakuwa amefanya kosa? Wazanzibari walio wengi wanampinga Hussein kwa dhahiri na kwa siri kiasi ya kuonyesha wote wameungana na kuwa kitu kimoja na sio kumpinga Hussein la hasha wanaipinga CCM kwa kuwa inawapoka haki yao ya kuchagua kiongozi wanemtaka.

Na sasa CCM sio inawakandamiza wapinzani kuwapindulia na kuwabadilishia matokeo, sasa hadi ndani ya CCM. CCM Zanzibar hawana ubavu wa kuamua lolote wapo wapo tu, ZEC ilipindua matokeo 2015 dhidi ya CUF, leo hii wanapinduana wenyewe kwa wenyewe.

Je, Hussein Mwinyi ameletwa ili kutekeleza kuelekea serikali moja na kisha akale bata Tanganyika.
Mwinyi ni mzaramo wa kisarawe nashangaa kwenda kugombea nchi ya watu
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom