Kuna hoja kubwa ambayo imeivunja CCM miguu na mikono kiasi ya kuwa hawawezi kusimama wala kutembea.
Dkt. Hussein Mwinyi hana sifa za kugombea Urais Zanzibar na kama haitoshi walio ndani ya innercore wanasema hakushinda kura za wajumbe wa CCM Zanzibar kiasi ya wasimamizi kuondoka Zanzibar bila ya kuwataja walioshinda, zilienea habari za redio kifua tu, lakini CCM hawakutoa majina ya walioshinda, walienda kuwatajia Dodoma.
Sababu inayoelezwa ni kuwa waliopendekezwa na kutakiwa na CCM hakuwemo hata mmoja na yale baadhi ya majina yaliotangazwa na kamati kuu ya CCM ndipo alipochomekwa Hussein Mwinyi. Kamati ilitegemea kupata uungwaji mkono jambo ambalo halijatokea hadi sasa, kwa maana CCM Zanzibar mara hii wamesema dharau ya kudharauliwa imevuka mipaka, kikwao wanasema imefurutu ada.
Wamesikika watu wakisema Hussein hana au hakidhi vigezo vya Katiba ya Zanzibar inakuwaje hapo? Upinzani hawakuliona hilo na kuweza kuweka pingamizi, ZEC nao hawakuliona hilo na wao kuweka pingamizi?
Je, akitokea mwanasheria anaejiamini na kupinga mahakamani ukiukwaji huu wa katiba ya Zanzibar, atakuwa amefanya kosa? Wazanzibari walio wengi wanampinga Hussein kwa dhahiri na kwa siri kiasi ya kuonyesha wote wameungana na kuwa kitu kimoja na sio kumpinga Hussein la hasha wanaipinga CCM kwa kuwa inawapoka haki yao ya kuchagua kiongozi wanemtaka.
Na sasa CCM sio inawakandamiza wapinzani kuwapindulia na kuwabadilishia matokeo, sasa hadi ndani ya CCM. CCM Zanzibar hawana ubavu wa kuamua lolote wapo wapo tu, ZEC ilipindua matokeo 2015 dhidi ya CUF, leo hii wanapinduana wenyewe kwa wenyewe.
Je, Hussein Mwinyi ameletwa ili kutekeleza kuelekea serikali moja na kisha akale bata Tanganyika.