Teuzi za Rais Mwinyi zaanza kuivuruga ACT Wazalendo, Zitto apinga wazi

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
Hatua ya Rais Hussein Mwinyi kumteua Thabit Idarous Faina kuwa mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) ambayo ilikosolewa na Chama cha ACT Wazalendo kilichopendekeza asiapishwe, imekichanganya kiasi cha kuitisha mkutano wa dharura kujadili hatua za kuchukua.

Kikubwa kinacholalamikiwa na ACT Wazalendo ni kwamba Faina ndiye alikuwa mkurugenzi wa ZEC kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 ulioshuhudia wagombea wao zaidi ya 16 wakienguliwa bila sababu za msingi na uchaguzi ukifanyika katika mazingira ambayo yasiyo huru wala ya haki na kuacha vifo na vilema kwa wananchi.

Tayari ACT kimeitisha kikao cha dharura cha kamati maalumu ya Kamati Kuu ya Taifa itakayokaa Oktoba 15.

Akizungumza na Mwananchi kwa simu jana, Mjumbe wa Kamati Kuu ya ACT Wazalendo, Ismail Jussa Ladhu alisema, “siwezi kusema chochote kwa sasa maana kuna vikao vitafanyika na vitaeleza nini cha kufanya kuhusu hilo.”

Kikao hicho kinachotarajiwa kuongozwa na Makamu Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Zanzibar, Othman Masoud Othman ambaye ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, kitawahusisha pia wajumbe wa kamati kuu wanaoishi Zanzibar pamoja na wajumbe wa kamati kuu wanaotoka katika vyombo vya kutunga sheria kama Bunge na Baraza la Wawakilishi.

Akizungumzia malalamiko ya ACT Wazalendo, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Catherine Nao alisema hayana mashiko na ni vyema kubainisha wazi wanachokitaka.

“Rais anao washauri, wakimshauri anasikiliza lakini ana haki ya kutosikiliza pia. Sasa Rais anateua halafu wewe unapinga unakwenda kinyume na Katiba ya nchi,” alisema Catherine.

Vilevile, alisena hata yeye hajui wanachopinga ACT Wazalendo kama ni jina au nafasi, “maana kwa sasa hakuna uchaguzi, kama tungekuwa kwenye uchaguzi kusema hawana imani naye ingekuwa sawa.”

Alisema ipo haja ya Makamu wa Kwanza wa Rais, Othman Masoud kusimamia nafasi yake akiwa mshauri namba moja wa Rais iwapo wanaona kuna sehemu mambo hayapo sawa badala ya kuanza kulalamika.

“Rais haangalii chama, anaangalia mustakabali wa nchi, sasa vyama tukianza kusema fulani hatumtaki hatutafika popote,” alikumbusha Catherine.

Wachambuzi wafunguka
Mchambuzi wa masuala ya siasa na mwanaharakati kisiwani hapa, Makame Ali Makame alisema ACT Wazalendo ni sehemu ya Serikali inayoongozwa na Dk Mwinyi, nafasi inayowapa uwezo wa kukijenga chama chao.

Wakati wote wa utekelezaji wa majukumu yake, alisema “Serikali inafuata sheria za nchi na chama hicho kulalamika ni haki yao ilimradi hawavunji sheria, lakini mamlaka ya Rais kuna mambo haiingiliwi.”

Kuhusu malalamiko hayo, Makame alisema kwa sasa sio wakati sahihi wa kulalamika kwa sababu maoni yaliyotolewa na wadau wa demokrasia bado yanafanyiwa kazi.

“Tukumbuke haya ni maoni yaliyotolewa, yanaweza kuchukuliwa ama yakaachwa, suala la msingi tusiwanyime viongozi nafasi zao za kisheria,” alisema.

Katika maoni yaliyowasilishwa katika kikosi kazi, inapendekezwa mwenyekiti wa tume ya uchaguzi na makamishna wake wapatikane kwa njia ya wazi na nafasi zao zitangazwe kisha wachaguliwe kwa sifa badala ya kuteuliwa.

Kwa maoni yake, Mwanasheria Said Awadhi alisema Tume ya Uchaguzi Zanzibar ilishindwa kusimamia uchaguzi wa mwaka 2020 kiasi cha kusababisha maafa.

“Hata kama hakukuwa na Serikali ya Umoja wa Kitaifa, huyo huyo aliyeshiriki kusababisha hayo ulimwondoa halafu unamrudisha, unatoa ujumbe gani kwa vifo vya watu vilivyotokea? Unaona ni sawa huyu aliyekuwa mtendaji mkuu wa Tume arudi tena pale?” alihoji.

MWANANCHI
Mchambuzi mwingine, Thuleiya Hamad alisema malalamiko hayo yanaweza kujitokeza zaidi, maana kwa sasa vyama vimepoteza mwelekeo na vimebaki kupigania maslahi yao binafsi na si maslahi ya Taifa, suala ambalo lilikipoteza Chama cha Wananchi (CUF) kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020, akisisitiza kuwa kuna haja ya kubadilisha siasa ili zifanyike zinazoleta tija kwa wananchi.

“Ikiwa unazungumza utaifa ila pembeni unaangalia maslahi binafsi itakuwa kazi ngumu sana, lazima tufanya jambo ambalo linawanufaisha Wazanzibari wote kupitia siasa, tatizo vyama vinakosa umoja,” alisema Thuleiya.
 
Hatua ya Rais Hussein Mwinyi kumteua Thabit Idarous Faina kuwa mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) ambayo ilikosolewa na Chama cha ACT Wazalendo kilichopendekeza asiapishwe, imekichanganya kiasi cha kuitisha mkutano wa dharura kujadili hatua za kuchukua.
ACT 🤔🤔🤔🤔🤔🤔
 
Maswali kwa Zitto na ACT Wazalendo

Ni kwanini huku bara mnashiriki uchaguzi chini ya tume ya Mahera aliyepora uchaguzi 2020?? Alafu mporaji wa uchaguzi wa zenji ndiyo mnamsusia?

Ipi tofauti ya mahera na thabit?
Hawa ACT walipoteza dira 2020.... Walidhani Chadema ndio ingeporwa viti pekee Ili wao wapewe na wangekua chama kikuu cha mageuzi. Sasa wamekosa vyote Imani ya wananchi plus viti vya kupewa..... Na 2025 ndio kaburi lao.
 
Back
Top Bottom