Uhakiki: Msajili akuta madudu NCCR Mageuzi na CHAUMA Zanzibar. Kimoja ofisi ziko sebuleni kwa mtu na kingine mali zake ni kiti na meza basi!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,965
141,971
Msajili wa vyama vya siasa ambaye kwa sasa anafanya uhakiki wa vyama vyote vya siasa nchini amekuta mapungufu kwa baadhi ya vyama vya siasa Zanzibar.

Msajili amesema baadhi ya vyama hali zao zinatisha na kimojawapo ofisi yake ipo sebuleni kwa mtu ambapo familia ya mtu huyo inatumia pia sebule hiyo na chama kingine kinamiliki kiti na meza pekee.

Msajili amevitaja vyama vyenye mapungufu hayo kuwa ni Nccr mageuzi na Chauma na kwamba ACT wazalendo wamepungukiwa nyaraka kadhaa.

Source: ITV!
 
Mbatia unafeli wapi?
Mbatia yupo kwenye maandalizi kabambe ya kuipiku chadema akisaidiwa na wanamikakati wa dola.. ameahidiwa kuachiwa baadhi ya viti bila kupingwa.
CHADEMA itaenguliwa kila mahali kwa kigezo kuwa hawakujaza fomu vizuri. Ila za NCCR zitajazika vizuri sana.
 
Mbona Simba na Yanga havina ruzuku bwashee!
Hivyo vina wadhamini na mashabiki wanaolipa viingilio milangoni.
Kwanini hicho chama kosa lake liwe ni ''umasikini'' ?
Tena hicho chama kwa maoni yangu naona hakika ndicho cha ''wanyonge''
 
Back
Top Bottom