Ugumu wa Biashara: Nakumatt tawi la Mlimani City Jijini Dar es Salaam yafungwa kisa kushindwa kulipa kodi

bado kile kiwanda chako cha gongo kitafungwa
Japo sitengenezi gongo , lakini nakubaliana na wewe kuhusu ugumu wa biashara Tanzania , ni kwa vile sisi miaka yote hatuuzi vyetu hapa bongo , tuna soko la uhakika sana ulaya na canada .

Hata hivyo watakaoumia ni masikini si sisi Matajiri .
 
Uongozi wa Mlimani City imeifunga Supermarket ya Nakumatt Tawi la Mlimani City Jijini Dar es Salaam kutokana na kutotimiza majukumu yake kama mlipakodi wa jengo hilo hivyo kurudisha nyuma upatikanaji wa Mapato.

Meneja Mkuu wa Mlimani City, Pastory Mrosso amesema wamechukua hatua hiyo baada ya uongozi wa Supermarket kutotekeleza wajibu wake kama mpangaji.

Wafanyakazi wa Nakumatt wameonekana wakiwa nje ya supermarket hiyo baada ya kukuta imefungwa bila taarifa huku wakisema bado wanadai stahiki zao


View attachment 610439

View attachment 610451

CHANZO: ITV
Nakumatt Uganda imefungwa, malori sita yakamatwa yakiondoka usiku wa manane
 
Hii ni baada ya kushindwa kulipa kodi na kuwapa stahiki wafanya kazi wake

Hivyo imefungwa rasmi leo
 
USISHINDANE NAWASIOJUA ...WASAMEHEEE AWAJUI WALITENDALO..UGANDA WAMEFUNGA ALHAMISI ILIOPITA NA BAADAYA funga wakaondia malori yao kuyaficha juzi wamekamata malori manne yakpita mtukula usiku wamanane na leo wamekamata usiku jinja malori mane yakiwa na mzigo yanayoyomaaa....imeamriwa yauzwe jmosi hii kulipia madeni ...kumbe kuna watu walikuwa wanapeleka bidhaa zao awawalipi natanguliza shukrani kwa jpm Hon ..asielipa kodi na asikae nchini tutatengeneza hata michezo yawatoto mle ndni
Asante Pdidy kwa kuweka na ushahidi,
 
Hapo kwenye mgahawa umenigusa. Wizi wa vyombo ni mkubwa.
Nakubaliana na wewe ndugu yangu. Kufanya biashara bongo ni kazi sana. Watanzania wana tabia ya udokozi. Hata ukifungua ka-mgahawa, watakuibia vijiko, sahani, sukari na mwisho wake ni biashara kufa. They just don't care kama biashara itakufa au la. Na Rais wao ana mentality hiyo hiyo. Biashara ikifa kwake ni poa, bila kujali athari kwenye soko la ajira.
 
Hata hivyo wananyanyasa wafanyakazi jambo ambalo halimpendezi Mungu. Wamrudie Mungu wao.
Kumbukeni kikichitokeaga NAKUMATT MOSHI hadi taarifa zilifika kwa mkuu wa Mkoa King kimanjaro enzi hizo na humu mjadala ulikuwa mkubwa sana.
 
Kwani tumemaliza kusoma namba, so bado sasa hivi tuko ya 19 mpaka tufike ya 100 wakati tumeiva
bawacha kwa kupenda kudandia mambo hata msiyo yajua..... Nakummat uganda nayo mali zao zinapigwa mnada, kenya nako hali mbaya twambie basi,,,,,
 
shoppers, game wataendelea kubaki maana wao bidhaa zao ni nzuri hao nakumatt mmmmm
 
Duh Magufuli kiboko, yaani anasababisha Nakumatt inafungwa hadi Uganda na Kenya!
 
Siyo kweli kuwa Nakumatt imekufa kwa ukosefu wa wateja Tanzania. Wateja walikuwa wengi sana na vitu kwenye mashelf vilikuwa vinaisha. Mbona Game, Mayfair, TSN na Mr. Price hawajafa na kuna utitiri wa mini-supermarkets mitaani? Kuna mahali Nakumatt walikosea mahesabu kama ndugu yao Uchumi.

Usione tu kwa nje. Hao wote uliowataja wanachechemea kutokana na kudorora kwa mauzo. Sitaki kuwataja, lakini wapo wengine watafuata kwa kufunga, siyo kwa kushindwa kulipa pango bali kwa kushindwa kufanya biashara yenye faida kwa ujumla. Mzunguko mdogo wa fedha umeathiri mauzo ya biashara zote zinazotegemea wateja wa ndani.
 
U nailed. Wabongo supermarkets sio culture yao kabisa. Huko ulikosema wakazi wengi ni wageni ambao wamezoea supermarkets.
Masaki na Oysterbay pekee kuna Food Lovers, Village Supermarkets, Shoppers supermarket, Target Supermarket, Shreejees(mbili) na zote zinafanyabiashara nzuri sana.

Culture ina nafasi ndogo sana. Labda kama umaskini ni sehemu ya culture. Maeneo uliyoyataja, wateja wake wengi ni wageni ambao mapato yao hayategemei mapato/biashara za ndani.

Kwa sasa biashara zote ambazo zinategemea wateja wa ndani, iwe ni biashara za wawekezaji wa nje au wa ndani zimedorora sana. Biashara ambazo mauzo yake ni nje ya Tanzania (wateja wa nje), haijalishi hizo biashara ni za wageni au watanzania, zipo Kariakoo au Manzese, zinaendelea vizuri.
 
Back
Top Bottom