Ugumu wa Biashara: Nakumatt tawi la Mlimani City Jijini Dar es Salaam yafungwa kisa kushindwa kulipa kodi

Kunguru Mjanja

JF-Expert Member
Aug 22, 2012
2,036
3,927
Uongozi wa Mlimani City imeifunga Supermarket ya Nakumatt Tawi la Mlimani City Jijini Dar es Salaam kutokana na kutotimiza majukumu yake kama mlipakodi wa jengo hilo hivyo kurudisha nyuma upatikanaji wa Mapato.

Meneja Mkuu wa Mlimani City, Pastory Mrosso amesema wamechukua hatua hiyo baada ya uongozi wa Supermarket kutotekeleza wajibu wake kama mpangaji.

Wafanyakazi wa Nakumatt wameonekana wakiwa nje ya supermarket hiyo baada ya kukuta imefungwa bila taarifa huku wakisema bado wanadai stahiki zao


nakumatt 1.jpg


nakumatt 6.jpg


CHANZO: ITV
 
Sasa watu wanakwenda kununua pipi tu

wengine wanakwenda kushangaa shangaa tu

purchasing power kwa wtz ni ndogo mno
Hiyo sio sababu ni kuwa Nakumatt wana matatizo huko kwao Kenya ambako nako wanazidi kuyafunga maduka yao,kisa ni ugomvi wa wanandungu ambao ndio wanamiliki Nakumatt,wengine wanamwaga mboga na wengine wanamwaga ugali.Watanzania tusiwe wepesi sana wa kulaumu kila jambo kwa Watanzania ,tujaribu kufukunyua chanzo kwanza kabla ya kurupoka kwenye mitandao
 
Sasa watu wanakwenda kununua pipi tu

wengine wanakwenda kushangaa shangaa tu

purchasing power kwa wtz ni ndogo mno

Siyo kweli kuwa Nakumatt imekufa kwa ukosefu wa wateja Tanzania. Wateja walikuwa wengi sana na vitu kwenye mashelf vilikuwa vinaisha. Mbona Game, Mayfair, TSN na Mr. Price hawajafa na kuna utitiri wa mini-supermarkets mitaani? Kuna mahali Nakumatt walikosea mahesabu kama ndugu yao Uchumi.
 
Biashara ya Supermarkets Tanzania ni ngumu sana..

Labda ukaifungulie Oyesterbay au Masaki ambako hakuna viduka vya Mangi.
U nailed. Wabongo supermarkets sio culture yao kabisa. Huko ulikosema wakazi wengi ni wageni ambao wamezoea supermarkets.
Masaki na Oysterbay pekee kuna Food Lovers, Village Supermarkets, Shoppers supermarket, Target Supermarket, Shreejees(mbili) na zote zinafanyabiashara nzuri sana.
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom