Ugonjwa wa Figo wazidi kuwatesa vijana, Hospitali zapokea wanne hadi 9 kila siku

“Kumekuwa na changamoto ya ongezeko la wagonjwa wanaofika wakiwa katika hatua za mwisho za kuchuja damu. Kwa wastani, kwa wiki tunawapata wanne mpaka tisa wanaohitaji kuchuja damu na wengi ni vijana.Tunajaribu kutafakari sana kwamba changamoto hasa ni nini,” anasema Kessy Shija, mkuu wa kitengo cha figo na daktari bingwa mshauri wa magonjwa hayo katika hospitali hiyo.

Hata hivyo, Dk Shija anasema utafiti mdogo wa mahojiano kati ya daktari na mgonjwa, unaonyesha kuwepo kwa matumizi makubwa ya vinywaji maarufu vya kuongeza nguvu (energy drinks) na pombe kali.
Ukisema TBS wafanye kazi yao kwa weledi na viwanda vya vinywaji viweke viwngo stahiki za kemikali utaambiwa mchochezi au unasumbua wawekezaji
 
3308ca0f02dd2abb38cce4c21545cc.jpg
 
Kuna siku ntaleta uzi jinsi hivi tunavyokula vinaleta magonjwa Kama kansa n.k, mavitu sokoni wake zenu wananunua vimepigwa dawa, makabeji hayo, hizo nyanya, michicha na mboga zingine za majani, na zaidi Kuna makala maalum ililetwa na channel flan kuhusu dawa za kuulia wadudu mashambani ambazo zimepigwa marufuku huko nchi za ulaya ila afrika zinauzwa na hata Tanzania zipo,,na hio ishu ni nzito sana hata waandishi was habari waliandaa hizo makala walipitia vikwazo vingi hata huyo mfanyakazi wa shirika la chakula alietoa Siri hakuwekwa wazi sura yake wakati anahojiwa, na ni mpango wa siri wa China huu hata ukienda kuangalia uongozi wote wa juu was shirika la chakula, ni wachina, hata anaengoza ni mchina,,wakati wa kinyang'anyiro hicho Cha uchaguzi wa kuchagua head of hilo shirika la chakula, watainiwa walikua wanne, lakin ajabu wote watatu walijiengua akabaki mchina akashinda,,je China Wana interest gani na shirika hili la chakula? Mambo ni mengi. Tuwe makini Sana Kama unaweza kulima mboga zakko bila kutumia madawa haya nyumbani fanya hivyo...utanishukuru baadae.
Umenena vema
 
Haya ma energy drink yameshathibitishwa ni hatari lakini viwanda vyao hapa bongo ndio vinachipuka kama uyoga na Kodi wanachukua, vinjwaji havijaandikwa tahadhari kama pombe Wala sigara . Naishauri serikali ifute vinjwaji hivi hatari na viwekwe kwenye orodha ya madawa ya kulevya
 
Back
Top Bottom