Matumizi makubwa ya Diclofenac, Diclopar na Mitishamba husababisha Ugonjwa wa Figo

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
#AFYA: Wataalamu wa Afya wameonya kuhusu matumizi makubwa ya Dawa za Kuondoa Maumivu zikiwemo Diclopar na Diclofenac na kueleza kuwa yanasababisha madhara kwenye Figo ambapo mtu anayepata athari hizo ataishia kuhitaji huduma za Kusafishwa Damu (Dialysis).

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Ndani na Figo wa Hospitali ya Muhimbili – Mlonganzila Dkt. Anthony Gyunda, amesema wengine walioko hatarini ni wanaotumia Dawa za Mitishamba ambazo hazina kipimo maalumu na nyingi husababisha Figo kushindwa kufanya kazi.

Aidha, Dkt. Gyunda amesema tafiti za hivi karibuni zinaonesha ongezeko kubwa la Wagonjwa wa Figo nchini linachangiwa na Mtindo wa Maisha usiofaa ambapo kuna matumizi yaliyopitiliza ya Pombe, Sigara Vyakula vya Wanga na Mafuta vinavyoogeza Uizto wa Mwili, Dawa n.k
 
Haya sasa, wale waliomtolea profesa janabi alipoelezea mambo kama haya waje na hapa watoe povu. Fuateni maelekezo ya wataalamu wa afya
 
Matumizi ya Paracetamol ambayo ni ya kuoitiliza yana madhara makubwa sana kwenye Ini kwa nji nchi yetu matibabu exactly ya Ini bado sana zaidi utapewa dawa za ku skip maisha ila kufa ni soon tuu
 
Back
Top Bottom