Ugomvi wa Zanzibar na wamasai ni mwendelezo wa Ubaguzi

Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
21,563
50,415
Kutembea na sime kwa wamasai haijaanzia leo ni jadi yao na wamasai hawana ugomvi na mtu.

Kuna ajenda fichika juu ya operesheni inayoendelea Zanzibar dhidi ya wamasai wenye sime. Wazanzibari wamekuwa na ubaguzi sana dhidi ya watu toka bara.

Wamasai wanatokea bara na wanazidi kuongezeka huko visiwani. Wanawaondoaje? Wametafuta sababu.

Wazanzibari wanaona kama wamasai wamechukua fursa zao huko Zanzibar.

Acha tuone mwisho wake.
 
Kitu ambacho wazanizbari walikiweza ni kutoacha utambulisho / Identity yao hata baada ya kuingia kwenye muungano ndio maana wana serikali yao, ajira zao, taasisi yao, sheria zao, n.k. na bad huku bara linakuwa ni taifa la "cha wote"

Tanganyika ilipoteza hata jina lake kwajili ya muungano,
 
Warudi huko maporini wakatembee na sime,
"When you are Rome, Do what Romans do"
Hiyo ni silaha, hakuna cha utamaduni hapa, unless ni mlinzi na kitambulisho kinachosema ni mlinzi.
Huku bara wanatembea nazo lkn hatujawai kuona Wala kusikia mmasai kamchinja hata kuku.

Kwann ninyi mhangaike nao? Ni ubaguzi unawasumbua.

Siku zinakuja mtajuta wazanzibari wote mlioko bara.
 
Huku bara wanatembea nazo lkn hatujawai kuona Wala kusikia mmasai kamchinja hata kuku.

Kwann ninyi mhangaike nao? Ni ubaguzi unawasumbua.

Siku zinakuja mtajuta wazanzibari wote mlioko bara.
Mkuu umekaa sana mjini inaelekea pengine hata kilimo hujawahi kufanya,

Wamasai wanaweza kulisha ngombe zao kwenye shamba lako sasa ole wako usogee, sime zina kazi zile

Nakumbuka pale Mbarali kulitokea ugomvi, wamasai walilipoza kwa kulisha ngombe zao shamba la mtu flani halafu wanacheza muziki, mwenye shamba anabaki kuangalia tu/
 
Usually,ukishamuona mtu anajipendekeza sana kwa watu,waarabu( na huku historia inasema watu hao waliwatesa mababu zake) na kufikia kuikana asili yake huyo moja kwa moja akili hana!

So nahitimisha kwa kusema Wapemba hawana akili sawasawa vichwani mwao,huwezi tu kulala usiku ukaamka asubuhi na hoja zako mfu kutaka jamii fulani iache tamaduni zao kisa siyo utamaduni wako.

Tukisema kila mtu aishi kulingana na tamaduni ya mwenzake hapa patakalika?
 
Huku bara wanatembea nazo lkn hatujawai kuona Wala kusikia mmasai kamchinja hata kuku.

Kwann ninyi mhangaike nao? Ni ubaguzi unawasumbua.

Siku zinakuja mtajuta wazanzibari wote mlioko bara.
Haya yameshaongelewa toka zamani
Warudi kwao huko maporini wanakoruhusiwa kutembea na sime na mapanga

Kifungu cha sheria za kanuni za adhabu, sura ya 6
Kifungu 84.
"Mtu yeyote anayetembea na silaha katika hadhara bila ya jambo lahalali linaloruhusiwa kisheria kwa namna ambayo inaweza kuleta utisho kwa mtu yeyote mtu huyo anatenda kosa na silaha yake yaweza kuhodhiwa"

Mkuu umekaa sana mjini inaelekea pengine hata kilimo hujawahi kufanya,

Wamasai wanaweza kulisha ngombe zao kwenye shamba lako sasa ole wako usogee, sime zina kazi zile

Nakumbuka pale Mbarali kulitokea ugomvi, wamasai walilipoza kwa kulisha ngombe zao shamba la mtu flani halafu wanacheza muziki, mwenye shamba anabaki kuangalia tu/
Kuna sakata la ugomvi kati ya wamasai na wakulima liliwahi kutokea Bagamoyo mkoa wa Pwani na Kilosa mkoani Morogoro.

Sexless unit tulipofuatilia sababu ya masakata hayo, ikaja kugundulika kuwa wakulima ndiyo wana nongwa sana. Ndiyo waliokuwa chanzo cha ugomvi na wamasai. Mmasai akisogeza ng'ombe jirani na shamba mkulima anapiga ukunga watu wanakusanyika na kuwakamata ng'ombe. Wamasai wakachoka na kuamua kuliamsha.

Nataka kusema nn hapa?? Ni kwamba mara nyingi ukiona migogoro kati ya wamasai na makundi mengine ya watu basi uwe na uhakika kuwa wamasai wamechokozwa
 
Back
Top Bottom