Ugomvi wa Mengi na Prof. Muhongo nani msuluhishi?

Ugomvi wa Mengi na Prof. Muhongo nani msuluhishi?

Kwenye sector ya gesi awekeze nani?

Chuki mbaya sana mkuu...Kuna watu wanamchukia Mengi kana kwamba akikosa Kitalu atakuwa maskini ama akipata atafaidi sana...
Inshu hapa ni Namna Gani Wazawa watawezeshwa kwenye Sector ya Gesi..Mengi ni Kielelezo tu Cha Wazawa Hao si Lazima apewe yeye..
 
Tafadhali acha ushabi na hisia ambazo zina mlengo wa uoga. Ugomvi gani unatishia uchumi wa taifa katika sekta za madini na nishati? Huu ni ugomvi wa ki-mtazamo tu. Huyu anasema ukweli na mwingine anataka huruma ya wananchi, sasa hapo kuna shida gani?
 
Reginald Mengi anatumia neno uzawa kama rent-seeking.

Kuna baadhi ya wabunge nao wameanza kununua/ kununuliwa na propaganda zake.

Suala la uwekezaji kwenye gasi liko wazi na hakuna mtu aliyekatazwa kuwekeza. Form na tenda ziko kwa kila mtu. Hii ya kusema wananchi watengenezewe mazingira ili waweze kuwekeza kwenye utafutaji wa gasi ni maneno ya kisiasa yaliyoficha ajenda zake.

Hoja yake ya Uzawa ukiichunguza utagundua inazunguka tu kwenye gasi na siyo kwenye sector nyingine. Why?.

Kitu ninachokipenda ni kuwa wakati Reginald Mengi analifanya jambo la Uzawa katika sector ya gas kama la kisiasa, Waziri Muhongo analiweka katika mizani ya kitaalam na uhalisia.

Kama Rais Kikwete atamuondoa Prof. Muhongo katika Wizara, basi sina budi kusema, neno la Mh. Mnyika na baadhi ya wananchi wengine litakuwa vindicated.

Kama kuna wanachi wenye uwezo kwenye sector ya gas, kwa nini wasiende kwenye tovuti hii na kununua form za tender,

The 4th Tanzania Offshore Licensing Round

Ng'wamapalala Ni wapi Duniani Uzawa unapuuzwa?? Kuwa Mzawa tu kunatosha kupewa Upendeleo..
Mengi/Wazawa waende TPDC Wakachukue Form sawa na BP,TOTAL etc...Nafikiri haupo Serious..

Hili ni Sawa na Nyerere alivyosema Kumchukua bondia wa Heavy Weight na kumpambanisha na Middle Weight Sheria ni zilezile lakini Sio sawa...

Kwanini kusitengwe Vitalu kwa ajili ya Wazawa tukatengeza BP zetu wazawa? Kuna ugumu gani? Kwani kila kitu mpaka Tuwape wageni tu??

Tumeshaona kwenye Madini Serikali haina uwezo wa kukusanya kodi/Inadanganywa kwenye Mapato hususani na Kampuni za nje sioni tofauti kwenye hili la Gas...
 
- The real ishu pale ni Mkono against Muhongo, Mkono ni mwanasheria wa IPTL na Tanesco kwa wakati mmoja mseme ukweli kama ulivyo kuliko kudanganya umma, wananchi wamechoka kudanganywa bana!!

Le Mutuz System

Le Mutuz acha kudandia mada! Katika issue hii suala ni uwekezaji katika sekta za madini na gesi!! Sasa Mkono anaingiaje hapa?!
 
Tafadhali acha ushabi na hisia ambazo zina mlengo wa uoga. Ugomvi gani unatishia uchumi wa taifa katika sekta za madini na nishati? Huu ni ugomvi wa ki-mtazamo tu. Huyu anasema ukweli na mwingine anataka huruma ya wananchi, sasa hapo kuna shida gani?
Kama hatuna sera nzuri katika uwekezaji katika sekta za madini na nishati, bila shaka Taifa linaweza kupata hasara na hivyo kuathiri uchumi!
 
JK na Pinda walishamaliza suala hilo ila Mengi bado anaweka bifu kwani JK alisema Serikali yake haiwezi kumwezesha mtu yoyote kifedha katika maeneo ambaoyo hakuna uhakika wa kupata chochote kwa maana ya gesi na madini na ndiyo maana hata Serikali haijawekeza kwenye vitalu vya gesi. kwani hamjui kwamba Mengi anamiliki vitalu 54 vya madini lakini ameshindwa kuviendeleza na sasa anaviuza kwa wageni. vile vile Mengi, Masawe na Maramba wanamiliki kampuni ya uchimbaji wa gesi ya SWALA ambayo kwa kuwa hawana mitaji wameamua kuwatafuta wageni wa ASTRALIA washirki katika uchimbaji huo. Nenda katika WESITE ya TPDC ujue sasa Mbatia anamtetea Mengi wote ni jamii moja ya wachaga. kaka ogopa sana makabila makubwa matatu hapa nchini wachaga, wanyakyusa na Wahaya. hawaogopi kusaidiana wenzetu akiingia mmoja mahali lazima avute wenzake. mmesahau pale BOT na Wizara ya Fedha wakati wa Waziri Mramba wachaga kibao hadi wakaandikwa magazetini!!! Wanyakyusa mtakumbuka wakati wa marehemu Mwaikambo pale NIC.
 
- The real ishu pale ni Mkono against Muhongo, Mkono ni mwanasheria wa IPTL na Tanesco kwa wakati mmoja mseme ukweli kama ulivyo kuliko kudanganya umma, wananchi wamechoka kudanganywa bana!!

Le Mutuz System

hivi unajua unachokiongea kweli
 
JK na Pinda walishamaliza suala hilo ila Mengi bado anaweka bifu kwani JK alisema Serikali yake haiwezi kumwezesha mtu yoyote kifedha katika maeneo ambaoyo hakuna uhakika wa kupata chochote kwa maana ya gesi na madini na ndiyo maana hata Serikali haijawekeza kwenye vitalu vya gesi. kwani hamjui kwamba Mengi anamiliki vitalu 54 vya madini lakini ameshindwa kuviendeleza na sasa anaviuza kwa wageni. vile vile Mengi, Masawe na Maramba wanamiliki kampuni ya uchimbaji wa gesi ya SWALA ambayo kwa kuwa hawana mitaji wameamua kuwatafuta wageni wa ASTRALIA washirki katika uchimbaji huo. Nenda katika WESITE ya TPDC ujue sasa Mbatia anamtetea Mengi wote ni jamii moja ya wachaga. kaka ogopa sana makabila makubwa matatu hapa nchini wachaga, wanyakyusa na Wahaya. hawaogopi kusaidiana wenzetu akiingia mmoja mahali lazima avute wenzake. mmesahau pale BOT na Wizara ya Fedha wakati wa Waziri Mramba wachaga kibao hadi wakaandikwa magazetini!!! Wanyakyusa mtakumbuka wakati wa marehemu Mwaikambo pale NIC.

mengi hana pesa ya kuwekeza kwenye gesi
 
tuache ushabiki tuangalie ishu za ukweli kwa nini nchi hii iwapendelee watu fulani kila siku ambao wanatuibia mchana kweupe kwa kusingizia uzawa. hakuna uzawa hapa ili kutuzuga sisi ili watuibie hakuna tena hakuna prof. Muhongo akaze buti hakuna kuwapa Mengi na Mkono madeal ya kuiba kuanzia pale Wizarani hadi TANESCO mbona TANESCO wapo Wanasheria wafanye wenyewe na Mengi kama ana hela kweli awalipe wafanyakazi wake kwamba wanaomdai akina Liganga, John Marandu, Mwitunmba na wengine wengi wanaommdai halafu akanunue data pale TPDC.
 
Mwaka juzi Petrobas na Shell wametumia zaidi ya dola milioni 300 kuchimba visima na hawakupata kitu, haya makampuni yana fedha zimetengwa kwa ajili ya utafutaji mafuta na gas, sasa niambie ni mtanzania gani ana uwezo wa kuwa na dola Milioni 300 za kwenda kumwaga baharini? Na itakuwa ghali zaidi ya hizo kwa sababu haya makampuni tayari yana technologia, ndo maana tunasema, wewe njoo na pesa zako, tunakupa kitalu, ukikosa gas ni hasara yako ukipata asilimia 60 yetu, kama Mengi ana hela aende akapewe kitalu atafute, akikosa imekula kwake, akipata asilimia 60 yetu. Na sio tumpe kitalu bure akatafute mwekezaji halafu akipata anampa yeye percent, hapa na.
safi sana mkuu mpanzi. huyu mengi msanii tu anataka apewe vitalu abinafsishe kwa wazungu wawe wanamlipa yeye badala ya serilaki. na mfano hai mengi aliwahi kulalamika wakati wa mwinyi eti wazawa hawana ardhi wala viwanja maeneo ya mjini. wanapewa watu weupe tu. alipopewa akauza
akajichukulia zake mahela.huyu ni msanii
 
Ng'wamapalala Ni wapi Duniani Uzawa unapuuzwa?? Kuwa Mzawa tu kunatosha kupewa Upendeleo..
Mengi/Wazawa waende TPDC Wakachukue Form sawa na BP,TOTAL etc...Nafikiri haupo Serious..

Hili ni Sawa na Nyerere alivyosema Kumchukua bondia wa Heavy Weight na kumpambanisha na Middle Weight Sheria ni zilezile lakini Sio sawa...

Kwanini kusitengwe Vitalu kwa ajili ya Wazawa tukatengeza BP zetu wazawa? Kuna ugumu gani? Kwani kila kitu mpaka Tuwape wageni tu??

Tumeshaona kwenye Madini Serikali haina uwezo wa kukusanya kodi/Inadanganywa kwenye Mapato hususani na Kampuni za nje sioni tofauti kwenye hili la Gas...


Ni nchi gani yenye utaratibu kama huo mnaoutaka? Kwa nini msikusanye nguvu mkawekeza kwenye TPDC ambayo itatengewa vitalu kwa ajili hiyo na badala yake mnataka mpewe peke yenu. Kama hamtaki kushilikiana na watanzania kupitia TPDC kwa nini mtake kupewa kipaumbele kwa kisingizio cha uzawa?
 
Kama issue ni sera, hiyo haina uhusiano katika malumbano ya Muhongo na Mengi.
 
Ni nchi gani yenye utaratibu kama huo mnaoutaka? Kwa nini msikusanye nguvu mkawekeza kwenye TPDC ambayo itatengewa vitalu kwa ajili hiyo na badala yake mnataka mpewe peke yenu. Kama hamtaki kushilikiana na watanzania kupitia TPDC kwa nini mtake kupewa kipaumbele kwa kisingizio cha uzawa?

Mkuu Uzawa Sio kisingizio..Uzawa ni Advantage popote pale..
Na kipaumbele ni lazima vinginevyo huo Uchumi utashikiliwa na wageni tu...
 
Watanzania sijui mmelogwa?Lini mtakuwa wajanja kama majirani zenu?Mimi bado ninamtetea Mengi na hoja yake ya Wazawa wamiliki vitalu vya gesi na mafuta,Najua Watanzania wengi hawana uwezo wa kumiliki hivyo vitalu hivyo ushauri wangu ungekuwa hivi;Ianzishwe kampuni ya umma ambayo itamilikiwa na Watanzania mbalimbali kupitia ununuzi wa hisa kisha hiyo kampuni iingie kwenye umiliki wa vitalu vya gesi na mafuta;Wafanyabiashara wakubwa wazawa wa nchii waunganishe nguvu kwa kuunda kampuni moja itakayojihusisha na gesi na mafuta;Na serikali iwadhamini/iwafadhili Wazawa katika kumiliki vitalu na hatimaye kuchimba mafuta na gesi.Tunajua kuwa Watanzania wengi hawana uwezo wa kuchimba mafuta na gesi hivyo watalazimika kuingia ubia na makampuni ya nje yenye kujihusisha na shughuli za uchimbaji mafuta na gesi.Hapa Wazawa watamiliki vitalu wakati Wageni watamiliki teknolojia na biashara itafanyika.Hata hili nalo ni gumu kufanyika isipokuwa kuwapa Wageni umiliki wa rasilimali zetu kwa 100%?
Ipo TPDC mkuu,jiungeni,undeni kampuni,uzianeni hisa ila mwisho wa siku nendeni pale TPDC na cheki zenu za malipo,fwateni utaratibu vitalu mtapata tuu wala hakuna siri kwa hili.
 
Duniani makampuni makubwa ya kuchimba mafuta yako manne (4) tuu,au la tano anataka kulianzisha Mengi?
 
Duniani makampuni makubwa ya kuchimba mafuta yako manne (4) tuu,au la tano anataka kulianzisha Mengi?

Hapana Mkuu, hataki kuanzisha lingine, anataka apendelewe yeye apewe halafu akawauzie.
 
Prof. Muhongo hana ugomvi na Mengi, bali Mengi ndiye anayeanzisha ugomvi na Muhongo kwa sababu zake binafsi. Nani asiyemjua Mengi bana? Anagombana na kila mtu anayeingilia maslahi yake. Imefika wakati sasa jamii ifahamu rangi halisi ya Mengi. Si mtu mzuri kama anavyojionyesha kwenye jamii kupitia vyombo vyake vya habari. Walio karibu naye wanamjua fika! Si mtu mzuri huyo.
 
Back
Top Bottom