SoC03 Ugatuzi wa madaraka ya ajira ngazi ya Halmashauri unavyoweza kuwa mwarobaini wa upungufu wa Walimu na Wataalamu wa Afya nchini

Stories of Change - 2023 Competition

cupvich

JF-Expert Member
Aug 2, 2022
408
246
Ripoti ya Mwaka ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali (CAG) Kwa mwaka wa fedha 2021/22 inaonyesha kwamba Katika halmashauri 23 pekee zilizofanyiwa tathmini Katika uwiano wa mwalimu Kwa wanafunzi ilibainisha Upungufu wa walimu 10,071 sawa na asilimia 35 ambapo walimu waliopo katika halmashauri hizo ni 28,677 pekee. Hii ni Kwa kuzingatia mpango wa III wa Maendeleo wa miaka MITANO wa 2021/22 Hadi 2025/26 unaoeleza kuwa, uwiano wa mwalimu Kwa mwanafunzi Katika shule za msingi Unatakiwa kuwa 1:50 na Kwa shule za sekondari 1:20.
Screenshot_20230630-014335_1688078728175.jpg

(Ripoti ya CAG 2021/22 uk.118)

Kwa upande wa Watumishi wa afya hadi kufikia mwezi machi 2023, sekta ya afya Ilikuwa na jumla ya Watumishi wa afya wapatao 109,616 sawa na asilimia 50.04 tu ya Watumishi wote 219,061 wanaohitajika Katika sekta ya afya kulingana na ikama iliyoidhinishwa.(kutoka Wizara ya Afya)

Zipo sababu nyingi zinazofanya kuwepo Kwa Upungufu wa Watumishi Katika sekta ya elimu na afya nchini ikiwa ni pamoja na mapinduzi MAKUBWA yaliyofanywa na Serikali Katika kuboresha huduma na Elimu msingi na Afya kama vile kugharamia elimu bila malipo kuanzia Darasa la kwanza Hadi kidato Cha sita, Ujenzi wa shule mpya maeneo ambayo hayakuwa na shule. hivyo Kushuhudia ongezeko kubwa la wanafunzi wanao andikishwa Darasa la kwanza na wale wanaofaulu kuingia kidato Cha kwanza. Kwa mwaka huu 2023 jumla ya wanafunzi 1,073,941 walichaguliwa kujiunga na kidato Cha kwanza Ikiwa ni ongezeko la asilimia 18.30 ukilinganisha na mwaka 2022.Vilevile jumla ya wanafunzi 1,634,365 walitarajiwa kuandikishwa Darasa la kwanza mwaka huu 2023. (Kutoka OR-TAMISEMI)
Screenshot_20230629-205155_1688078773399.jpg

(Chanzo: Jamii Forums)

Kwa upande wa sekta ya afya Serikali imefanya maboresho MAKUBWA Katika Utoaji Huduma za afya nchini ikiwa ni pamoja na kujenga vituo vipya vya afya nakuongeza matibabu ya kibingwa Katika hospitali nyingi nchini Hali iliyosababisha wananchi wengi kwenda kupatiwa matibabu Katika hospitali za umma hivyo Kusababisha uhitaji mkubwa wa wataalamu wa afya.

Pamoja na changamoto hiyo ya uhaba wa Watumishi wa Afya na Elimu Katika halmashauri zetu. Serikali imeendelea kuchukua hatua mbalimbali Katika kukabiliana na changamoto hiyo ikiwa ni pamoja na Kutoa vibali vya kuajiri Watumishi wapya na kufanya Msawazo wa Watumishi Ili kukidhi ikama. Mwaka huu wa fedha 2022/2023 Serikali Ilitoa kibali Cha kuajiri walimu wa shule za msingi na sekondari 13,130 na Watumishi wa afya 8,070 kupitia OR-TAMISEMI.
images (45).jpeg

(picha kutoka mtandaoni)

Mfumo wetu wa Sasa wa Ajira za Ualimu na wataalamu wa afya Unasimamiwa na Ofisi ya Rais tawala za mikoa na Serikali za mitaa (OR-TAMISEMI) pamoja na Wizara ya afya. Ambao ndio hutoa utaratibu na vigezo vya maombi ya Ajira pamoja na Kuchakata maombi ya waombaji na kuwapangia vituo vya Kazi Moja Kwa moja. Hivyo kazi za Halmashauri ni kuwapokea waajiriwa wapya na kukamilisha taratibu zao za kiutumishi. Mfumo huu wa ajira hautoi suluhisho la kudumu Katika kukabiliana na Upungufu wa walimu na Watumishi wa afya Katika halmashauri zetu kwasababu kuu mbili zifuatazo.

Moja, Jicho la Mfumo huu liko mbali na halmashauri zetu, OR-TAMISEMI na Wizara ya afya zimekuwa zikitumia taarifa zilizopo kwenye mifumo Ili kubaini maeneo yenye Upungufu wa Watumishi wa afya na Elimu , Kila mwaka madodoso kama vile TSA,TSM,TWM yamekuwa yakijazwa na Kwa kiasi kikubwa ndiyo ambayo yanatoa uhalisia wa idadi ya walimu Katika shule zetu. lakini Bado Watumishi wanaoajiriwa wameshindwa kukidhi uhalisia wa madodoso.

Mbili, Mfumo huu wenye Madaraka ya kuajiri wataalamu wa afya na Elimu unakabiliwa na Majukumu mengi. OR-TAMISEMI ni wizara mtambuka ambayo inahusika na majukumu mengi Kwa kushirikiana na Wizara zingine za kisekta, pamoja na Majukumu mengi ndiyo wizara inayosimamia Ajira za walimu na Watumishi wa afya nchini. Hivyo kuwa na Ufanisi kidogo Katika kutatua changamoto ya uhaba wa Watumishi wa afya na Elimu nchini.

Hivyo Ili kukabiliana na changamoto hii ya Upungufu wa walimu na Watumishi wa afya nchini,Napendekeza halmashauri zipewe Madaraka ya kuajiri watumishi wapya na kuwapangia vituo vya Kazi. Kibali Cha Ajira kitolewe kama kawaida na Mheshimiwa Raisi kupitia wizara ya utumishi kulingana na Bajeti ya mwaka husika na baada ya Kibali mgawanyo wa idadi ya Watumishi wanaotakiwa kuajiriwa Kwa Kila halmashauri ufanyike. Kisha halmashauri husika Zitangaze tangazo la ajira, Baada ya tangazo la ajira, wahitimu wenye sifa wafanye maombi ya kazi kupitia sekretarieti za Halmashauri.

Ugatuzi huu wa Madaraka ngazi ya halmashauri,pamoja na Faida nyingine nyingi utasaidia pia kutimiza azma ya Wizara ya Elimu, Sayansi na teknolojia ya kuwapata walimu mahiri na waliokidhi vigezo kama ambavyo waziri wa Elimu Sayansi na teknolojia profesa Mkenda alivyotangaza utaratibu mpya wa Ajira za Ualimu tarehe 16/06/2023 Wakati wa hafla ya Utoaji tuzo Kwa Walimu walioshinda shindano la kwanza la stadi za kufundisha kuhesabu na hisabati lililoandaliwa na taasisi ya Elimu TET.

Hivyo Katika Ugatuzi huu wa Madaraka, waombaji wa Ajira watafanyiwa Usaili Katika ngazi ya halmashauri na watakao faulu watapangiwa vituo Vya kazi na Halmashauri husika Kisha MAJINA yao kutumwa OR-TAMISEMI na Utumishi Kwa ajiri ya taratibu zingine za kiutumishi. Napendekeza Usaili Kufanyika Siku Moja Katika halmashauri zote nchini au mwombaji aruhusiwe kuomba halmashauri Moja pekee Ili Kupunguza idadi ya wasailiwa Sehemu Moja na kufanya mgawanyo wa wahitimu kuwa mzuri Katika halmashauri zote nchini.

Faida Nyingine zitakazopatikana Katika Mfumo huu mpya wa Ajira za walimu na afya ni Kupunguza kuhama hama Kwa Watumishi wa Elimu na afya kwani Mhusika ataomba halmashauri Anayopenda kufanyia kazi, Itasaidia halmashauri husika Kupanga walimu na wataalamu wa afya kulingana na uhitaji kwani Jicho la halmashauri litakuwa karibu, Halmashauri Itakuwa na mamlaka ya kufanya msawazo wa Watumishi muda wowote Kwa kutumia mapato ya ndani, lakini pia halmashauri husika zitaboresha mazingira ya Watumishi wa afya na Elimu Ili kuwafanya Kutoa Huduma Bora.

Mwisho, Ili kuleta tija katika Mfumo huu wa Ugatuzi wa Madaraka ya Ajira ya Ualimu na wataalamu wa afya ngazi ya halmashauri, Serikali haina budi kuimarisha vyombo vyake vya ulinzi na usalama ambavyo ni TAKUKURU na Jeshi la polisi ngazi ya halmashauri Ili kuzuia mianya ya RUSHWA nakuweza kupata Wataalamu wanaokidhi vigezo Kwa haki pasipo upendeleo.
 
Last edited:
Ripoti ya Mwaka ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali (CAG) Kwa mwaka wa fedha 2021/22 inaonyesha kwamba Katika halmashauri 23 pekee zilizofanyiwa tathmini Katika uwiano wa mwalimu Kwa wanafunzi ilibainisha Upungufu wa walimu 10,071 sawa na asilimia 35 ambapo walimu waliopo katika halmashauri hizo ni 28,677 pekee. Hii ni Kwa kuzingatia mpango wa III wa Maendeleo wa miaka MITANO wa 2021/22 Hadi 2025/26 unaoeleza kuwa, uwiano wa mwalimu Kwa mwanafunzi Katika shule za msingi Unatakiwa kuwa 1:50 na Kwa shule za sekondari 1:20.
View attachment 2673681

View attachment 2673682
(Chanzo: Jamii forum)

View attachment 2673686

Uzi upo ubaoni,, pata Muda kuupitia.
 
Soc2023
 
Safi sana kwa andiko zuri mwana jamii forum.. HII inaweza kutusaidia wengi kuingia katika mfumo wa ajira. Andiko zuri sana. Nimekupa KURA YANGU.
 
Asante mwana jamii Forum. Serikali haina budi sasa kuangalia upya mfumo wa utoaji wa ajira za afya na elimu ili kuondoa tatizo kabisa la upungufu wa wataalam hawa muhimu.
 
Back
Top Bottom