Uganda: Mahakama ya EAC haina mamlaka ya kutoa uamuzi kuhusu kipengele cha umri wa rais

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,501
9,280
Serikali ya Uganda inasema kuwa mahakama ya Afrika Mashariki iliyoko mjini Arusha nchini Tanzania, haina mamlaka ya kusikiliza kesi kuhusu kipengele cha umri wa rais.

Kesi hii ilipelekwa kwenye mahakama hiyo na wanaharakati wakitaka ibatilishe uamuzi wa mahakama ya katiba iliyokubaliana na bunge kuondolewa kwa ukomo wa umri wa mtu kuwania urais mwezi Aprili mwaka huu.

Serikali ya Uganda ilikuwa ikijibu kesi iliyowasilishwa mbele ya majaji wa mahakama hiyo ambao watatoa uamuzi ikiwa wanaweza kusikiliza kesi hiyo au la.

Pendekezo la kuondoa ukomo kwa mgombea urais Uganda lilowasilishwa bungeni limesababisha mvutano mkubwa uliopelekea uvunjifu wa amani ndani ya Bunge.
Hatua ya kuondoa kiwango cha umri ilionekana kama juhudi za Museveni kuongeza utawala wake.

Wakosoaji wake wanasema Museveni anataka aongoze taifa hilo hadi kifo kitakapomkuta.
Uchaguzi ujao nchini Uganda utafanyika mwaka 2021 kwa mujibu wa katiba ya nchi hiyo, na umri wa mwisho wa kugombea urais kabla ya Katiba kufanyiwa marekemisho ulikuwa miaka 75.

Rais Museveni atakuwa na umri wa miaka 76 wakati wa Uchaguzi huo.
Rais Yoweri Museveni ambaye ana umri wa miaka 75, ametawala Uganda tangu alipochukua madaraka kwa nguvu mwaka 1986.
 
Kwa kiongozi mkubwa kuanza kuhoji mamlaka ya Mahakama EAC ni kuidhooisha - hence kuudhoofisha huo muungano ambao hadi leo bado unasua-sua.
 
NADHANI NI KWELI EAC HAINA MAMLAKA YA KUINGILIA MAMBO HAYO ... NI BORA KILA.MTU ATULIE NA NCHI YAKE
 
Kabisa. .tena ni utovu wa madaraka. .na kuonyesha kuwa muungano huo hauna power

Back
Top Bottom