Mahakama yathibitisha Ushindi wa Bola Tinubu kuwa Rais wa Nigeria

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,502
9,281
Mahakama ya juu ya Nigeria Alhamis imethibitisha ushindi wa rais Bola Tinubu na kufikisha mwisho wa kesi iliyofunguliwa na wapinzani wake wawili, ambao walisema ushindi wake uligubikwa na makosa.

Uamuzi huo wa mahakama utampa Tinubu mwenye umri wa miaka 71 nafasi ya kuliongoza taifa hilo maarufu Afrika, ambalo linakabiliwa na hali ngumu ya maisha mara mbili zaidi, upungufu wa fedha za kigeni, na sarafu yake ya Naira iliyo dhaifu pamoja na ukosefu wa usalama katika maeneo mengi na wizi wa mafuta ghafi.

Nigeria ilirejea katika demokrasia mwaka 1999 baada ya takriban miongo mitatu ya utawala wa kijeshi usioingiliwa, lakini shutuma za wizi wa kura na ulaghai vimeendelea katika mfumo wake wa uchaguzi.

Uamuzi uliotolewa na majaji saba wa mahakama ya juu, ambapo ndio wa mwisho unafuatia yaliyojitokeza katika uchaguzi uliopita wa urais ambao ulipingwa mahakamani. Majaribio yote ya kubadilisha matokeo kupitia mahakama hayajawahi kufanikiwa.

DW
 
Back
Top Bottom