Ugali ni chakula cha kimasikini

hahaha si wanasemaga ukiongea ujinga kwa kiingereza unaonekana umeongea vya maana?
Hajui wenzie wanakula burger huko kwao kwa sababu ni cheap and very convinient.

Halafu na pembeni usisahau kisamvu cha nazi/karanga ama majani ya kunde ya nazi. Mmmh hadi nimeskia njaa.:glasses-nerdy:
Anaona processed food ndo za maana badala ya natural, organic food?!

Halafu I'm drooling na hii recipe ya dagaa, naenda ifungia kibwebwe!
 
Wazungu wanatumia sana nafaka ya mahindi, kuna hizi cornflaks, ni mahindi yale, cornoil,viongo km aromat, yaani kuna vingi sana, hata uji wa maindi wanakunywa sana, yaani mahindi wao wanatoa bidhaa nyingi tofauti na sisi.
 

Nimeenda nchi fulani za ulaya nimekuta dagaa, tena sio wale wa kutoka nchi za kiafrika wanaopelekwa na west africans au wakongo, ni dagaa wa hukohuko waliofanyiwa packaging safi kabisa.
Unga wa mahindi upo na unatumika pia na nimekula sana ugali wake ingawa unakuwa hauna ladha timamu kama wetu lakini ni unga wa mahindi kabisa.
Mexico wana ile kitu wanaita taco, grain inayotumika ni hindi.
Wakati mwingine tusipuuze vyetu kwa kudhani ni duni wakati hatuufahamu umuhimu wake vyema. Hata watafiti wengi wa lishe kutoka nchi zilizoendelea ndio wanaanza kuzijua faida za hivi vyakula tunavyoviona duni.
 
Mtoa mada umeandika kipuuzi!

Ugali ni chakula cha Afrika na sio cha wazungu, so kwa vile tupo poor ndio unahalalisha ugali=poverty?

Nonsense, bure kabisa
 

Ni kweli mkuu...
King'asti kasema nilivokuwa nafikiria, mfano wa hizo zinazoonekana za maana kama burgers they're cheap, convenient and unhealthy.
Ona hii menu aliyoweka King'asti, ni balanced diet, tasty, halafu chakula cha nyumbani una guarantee kiko fresh na si hizo burger patties zinazokuwa frozen miezi nenda rudi!
 
Last edited by a moderator:
unachotafuta kwenye grains yoyote ni carbs sasa wewe huelewi huo unga wa baga wa ngano na mahindi ya ugali yote ni starch pole sana
au rudi shule
 
Tumia chakula kitokanacho na ngano na utakuwa na akili sawa na wazungu,utalala kitanda kimoja na mbwa,utawabusu mbwa,utaongea na mbwa na utamfanya mbwa ndio kila kitu hakuna mwandani na rafiki kama madog!

Think wide, umeona hilo! Huoni ndege wanazotengeneza (labda hiyo inaweza hujawahi panda kama mimi), dawa unazomeza, nguo unazovaa, viatu, mafuta ya taa unayotumia and many many more. Umeona la mbwa tu! Mbwa ni kwa vile wana ziada ya kumpa mbwa. Je wewe una ziada, lazima mbwa awe adui kwetu! Mbwa koko tunaita
 
Nchi nyingi za wenzetu vyakula vya kikwetu ambavyo miaka ya nyuma ilikuwa ni ngumu sana kuvipata labda mpaka kwenye maduka ya wahamiaji siku hizi vimejaa belele tena kwenye supermarkets ni pumzi yako tu kama unathamini kula vyakula vya kikwetu au kama unataka kula uchafu wa vyakula vinavyotengenezwa kwa dakika tatu burger na fries. Huwa nawashangaa sana wanaosema ugali ni chakula cha kimaskini, sasa sijui ni kipi ni chakula cha kitajiri. Na kama unapenda kula ugali hata ukiwa tajiri bado utautamani tu ugali kwa nyama choma nzuri sana/samaki pembeni kuna mchicha....Acha unashusha mlima taratibu tena kwa raha zao siyo haya mavyakula hata ukiwa na njaa bado havikutamanishi.

 
Mtoa mada umeandika kipuuzi!

Ugali ni chakula cha Afrika na sio cha wazungu, so kwa vile tupo poor ndio unahalalisha ugali=poverty?

Nonsense, bure kabisa

Msigwa, mbona watoto wetu wanapenda chips na Piza? Lakini wazungu sijawahi ona wanatamani ugali? I stand to be corected
 
unachotafuta kwenye grains yoyote ni carbs sasa wewe huelewi huo unga wa baga wa ngano na mahindi ya ugali yote ni starch pole sana
au rudi shule
Wewe masai dada, the way you treat carbohydrates matters a lot!
 

Uko sahihi sana, lakini wanaleta wanigeria (majority) kufanya biashara kwa waafrika waliopo huko. Not for wazungu! Wazungu hawali. Tumekaa sana huko western world, hawatamani , watajifanya wanakula kukupendezesha tu muwe kitu kimoja (ili asionyeshe dharau ya chakula chako)
 

Mkuu hebu soma post namba 112. Wamemodify vyakula vingi na huwezi kutambua ingredients kirahisi yakiwemo mahindi na vingine vingi. Kuna kiasi kikubwa tu cha vyakula wanavyotumia ambavyo ndani yake kuna asilimia kubwa tu ya vile tunavyovidharau, ni recipes tu zimepishana na vingi vinapitia kiwandani ila wanatumia. Vitu kama dengu, mbaazi, choroko na mahindi, vinatumika sana ila si kama ugali au vile tunavyoandaa sisi. Kingine ni kuwa wazungu wanatumia samaki na dagaa wakavu katika baadhi ya nchi, amini hicho. Unajua Mreno anakula ng'onda na Muhogo?
 

Tuko pamoja, Masai dada amesema vyote ni carbohydrates, nikamjibu kuwa what matters ni treatment ya hizo carbohydrates
 
 
 
Msigwa, mbona watoto wetu wanapenda chips na Piza? Lakini wazungu sijawahi ona wanatamani ugali? I stand to be corected

Siki zote junk foods ziko tasty sana na si kwa hapa tu, Ulaya, Marekani, China na nchi nyingi tu, ndio maana kuna kampeni kubwa duniani juu ya matumizi ya junk foods kutokana na kuwa chanzo cha obesity kwa wengi kwani ni tasty sana na zimebeba calories nyingi combination ambayo ni lethal sana.
Kingine ni kuwa, ukiacha matunda yaliyo na ladha ya sukari, asilimia kubwa ya vyakula vilivyo na value kubwa kiafya na ambavyo havikuwa modified, yaani vilivyoandaliwa katika namna ya kawaida, huwa vinachukua muda kupendwa, si na watoto tu, bali hata na watu wazima hasa endapo watakuwa wamewahi kuonja fast meals, au refined foods. Ndio maana siku zote ni kazi kumlisha mtoto mboga za majani.
 
Reactions: kui
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…