Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi, leo Agosti 11, 2025

Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi, leo Agosti 11, 2025

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
4,783
Reaction score
14,975


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango anafungua Mkutano Mkuu wa mwaka wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi Agosti 11, 2025 Shule ya Polisi Tanzani- Moshi.

GyDJukcWgAEEInO.jpeg
Maafisa mbalimbali wakiwasili katika Viwanja vya Shule ya Polisi Tanzania - Moshi kwa ajili ya Mkutano Mkuu wa mwaka wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi unaofunguliwa leo Agosti 11, 2025 na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Philip Isdor Mpango.
GyDKTqwXEAA_pbw.jpeg

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Camillus Wambura, akiwasili katika ukumbi wa Shule ya Polisi Tanzania – Moshi, leo Agosti 11, 2025, kwa ajili ya kuhudhuria hafla ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa Maafisa Wakuu Waandamizi wa Jeshi la Polisi.
Screenshot 2025-08-11 120839.jpg
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu amesema hali ya Usalama katika mkoa wa Kilimanjaro ni shwari na amelipongeza Jeshi la Polisi mkoani humo kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuhakikisha kuwa Wananchi katika mkoa huo wanaendelea na majukumu yao bila changamoto ya kiusalama.

Babu amewasihi Maafisa wa Jeshi la Polisi kutumia fursa ya mkutano huo kujadili changamoto zinazolikabili Jeshi la Polisi na kuweka mikakati madhubuti ya kukabiliana nazo.

Aidha, amesisitiza kuwa yeyote anayefikiria kufanya uhalifu katika mkoa huo atafute pa kwenda.

Nurdin ameyasema hayo wakati akitoa salamu za Mkoa huo wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi unaofanyika Shule ya Polisi Tanzania - Moshi.
 
Mapoti waongezewe posho Wana hali ngumu sana kitaa
20250719_082812.jpg
 
Back
Top Bottom