Utangulizi
Kitu muhimu cha kuzingatia wakati wa ufugaji wa samaki ili kuongeza uzalishaji ni kuwalisha samaki chakula ambacho kipo kamili (balanced diet). Mfugaji hapo nyumbani unaweza kutengeneza chakula chako hapo nyumbani kama upon a malighafi zifuatazo pumba za mahindi pamoja , mashudu , dagaa,pumba za mchele katika mchanganyiko maalamu ambao utatoa chakula bora kwa ajili ya kuwalisha samaki wako
Jinsi ya kuwalisha samaki
Baada ya kutengeneza chakula chako kwa ajili ya samaki, hakikisha unasimama katika pembe moja yapo ya bwawa la samaki na fanya kurusha chakula kwa kutumia mkono wako katika muda maalumu ambao huo muda ndio utakuwa muda maalamu kwa samaki kula chakula chao.
Baada ya kurusha chakula anza kutazama kama samaki watakikubali chakula ulichowapa hii itajidhirisha kwa samaki kula chakula na wao watajenga mazoea kuibuka muda huo kuja kula chakula na katika pembe husika uliyowarushia samaki…. Na kwa kawaida samaki huchukua takrabi dakika kumi na tano kula chakula.
Muda wa kuwalisha samaki
Kwa kawaida tilapia (sato) hutumia muda mwingi kunywa maji na hula chakula kidogo sana kwa kuwa huwa na matumbo madogo. Na kwa kawaida unatakiwa kuwalisha sato katika muda wa saa4 asubuhi na saa10 jioni hii ni kwa sababu joto la maji pamoja na kiwango cha oxygen (dissolved oxygen) huwa juu sana.
Na hakikisha unazingatia muda ambao unautu ia kuwalisha samaki na sehemu husika ambayo uitumia kuwalisha samaki na mtu ambaye hutumika kuwalisha samaki anatakiwa kuwepo muda wote na aipende kazi yake.
Faida za kuwalisha samaki kwa kutumia mkono
Kuna njia mbalimabli ambazo mfugaji anaweza kuzitumia kwa ajili ya kuwalisha samaki lakni mkulima anashauriwa kuwalisha samaki kwa kutumia mkono ili kuweza kuwaangalia kama samaki wako katika hali nzuri(afya) kwa kuwaangalia jinsi wanavyokula kwa kawaida samaki wanapoona chakula hufurahia na huwa katika staili fualni hivi ya kupigania chakula nje ya hapo ukiona samaki hayuko katika hali hiyo jua kuwa kuna tatizo…
Vifuatavyo huweza sababisha samaki wasiweze kula chakula kama hapo mwanzo:
- Maji ya bwawa yaweza kuwa baridi
- Kiwango cha oxygen (dissolve oxygen) kipo chini
- Samaki wanaweza kuwa wagonjwa
- Samaki baadhi wanaweza kuwa wamekufa
- Chakula kinaweza kuwa kizito ambavyo yaweza pelekea kuzama chini
Kiwango cha chakula anachokula samaki
Wewe kama mfugaji unashauriwa kuwa na record ni samaki wangapi ambao wapo kwenye bwawa lako kwa kawaida pale unapoweka fingerling katika bwawa lako ni vyema kuwa na record sahihi umeingiza vifaranga wangapi wa samaki katika bwawa lako hii itakupelekea wewe mfugaji kujua ni kiwango gani cha chakula kinahitajika kuwalisha samaki katika bwawa lako:
Hapa chini nimeambatanisha jedwali ambalo litakupa mwanga ni kiwango gani cha chakula kinahitajika katika kila umri..
View attachment 621374
Imeandaliwa na
theriogenology
Doctor of Veterinary Medicine
Karibuni kwa maswali na Huduma