Ufugaji wa Kuku wa Kisasa: Fahamu Mbinu, Faida, Changamoto na Masoko

Ndugu zangu habari yenu na polen kwa miangaiko, naombeni msaada wenu mm ni mfugaji wa Kuku wa nyama ninayeanza but nmepata changamoto wana wiki ya 4 ila hawaongezeki/kukua nifanyaje au ntumie njia gan ?
IMG_20211029_125406_504.jpg
View attachment 1994743
 
Naweza pata mteja wa kuku layers wako 700
,200 nimewachinja wako kwene frizer,location kakola,kahama 0692959979 kwa maelezo zaid na bei
 
Kuku sasso wanauzwa
Umri miezi3 na wiki3.
Wako120,
Bei ni 12000,
Location Ushirombo.
Kama mteja ni wa mbali atapunguziwa bei ili abakie na nauli ya kusafirishia. 0629306194 karibuni
IMG-20211122-WA0005.jpg
 
Mlachake, una experience kwenye ufugaji kuku? kama huna basi, kuanza na kuku 1000 utakuja kulia. Na kama ni lazima uanze na kuku wengi,basi usiwe na mkono wa birika, kwamba usiwe bahili.

Lazima utafute part time animal scientist ambae atakuwa mara kwa mara anakushauri suala zima la poutry management!!! aidha,usiwe bahiri, hususani kwenye feeding!!! poultry keeper wengi wana-collapse kv wanataka kubana matumizi kwenye chakula---manake wale jamaa wanafukia ile mbaya.

In order to have productive layers or broilers, lazima kwenye masuala ya misosi wajiachie!!! and even more important, especially kama ni kuku wa mayai, tenga bajeti ya chakula pembeni na usiichezee kwa kitu kingine chochote kile, iwe pale ready for feeding!! Kama utapata mtaalamu, akakupa techinques za kutengeneza chakula itakuwa more wise kwako, kwavile feed cost ipo juu sana.

BUT be careful, usi-opt tu kutengeneza chakula chao wakati feed chemistry haunayo!!! kama ni wa mayai, badala ya kuanza kutaga after 5 ro 6 months, wataanza after 8 months!!!Kama unazani hutaweza kufanya mixing vizuri, u better ukajilipue kwenye vyakula vya madukani ambavyo ni very expensive- but don' worry, bei hiyo haitakufanya upate hasara, but itapunguza faida!! na kitu kingine muhimu, don buy day old chicks mitaani, utakuja kulia!!!hizo ni few hints, but the project, inalipa wangu!!!

Mengine yote, unaweza kushauriwa na animal scientist, but the first good strategy --- tafuta kijana ambae tayari ameajiriwa kwenye suala zima la utunzaji kuku -- mchomoe anakofanya kazi na mpe mshahara mkubwa zaidi, na mpangie room very close na yalipo mabanda yako!!! uki-opt kujenga annex ya kukaa poultry keeper, itakuwa ni more productive idea! wish u all the best
 
helow mkuu kampuni ngapi tanzania zinazotoa mbegu nzuri ya kuku BROILERS?
 
HATUA KWA HATUA UFUGAJI WA KUKU BORA WA NYAMA (BROILER)

Lengo la makala hii ni kukuwezesha wewe mkulima kupata kuku wa nyama wenye uzito sahihi kukuwezesha wewe kupata faida. Hivyo basi wewe kama mfugaji ni vyema ukajua ya kwamba wiki mbili za mwanzo katika uleaji wa kuku wa nyama ni muhimu sana na hivyo yakupasa kuwa mwangalifu.

★ Mambo ya kuzingatia kabla vifaranga wako hawajafika kwenye shamba

Banda la kuku, mazingira yanayolizunguka na vyombo vyote vilivyotumiwa kwa batch iliyopita yapaswa kusafishwa vyema kwa maji safi na dawa ili kuua vimelea ambavyo vinaweza sababisha magonjwa.

Hakikisha sehemu ya kuwekea vifaranga (brooding area) linapashwa na joto saa limoja kabla ya vifaranga kuingia ndani ya brooding area.

Kwa matokeo chanya na yenye faida vifaranga vyapaswa kufikishwa kwenye banda haraka iwezekanavyo na kama inawezekana wapewe chakula muda huo huo.

Kamwe usisafirishe vifaranga kwa kutumia buti la gari mara nyingi vifaranga husafirishwa wakiwa wamewekwa kwenye seat ya gari ambapo watapata hewa ya kutosha na kuepuka stress.

Nafasi ya vifaranga inatakiwa kuwa vifaranga kumi kwa mita square moja (10bird/1m2) epuka kuwajaza kuku wengi katika eneo dogo.

Mambo ya kuzingatia baada ya vifaranga kufika eneo la shamba

Mara wafikapo tu vifaranga wanatakiwa kuondolewa kwenye box mara moja. Unapowachelewesha ndani ya box utawafanya kuku kuwa na stress na hivyo kupelekea vifo au kuku kutokua vizuri.

Kwa siku saba za mwanzo wape mwanga kwa masaa23 ili kuwawezesha vifaranga kuzoea mazingira mapya na kuwafanya wao kula chakula.

Wape maji na chakula baada ya vifaranga kuingia bandani na hakikisha unaongeza vitamin kwenye maji au glucose kabla ya kuwapa hao vifaranga.

Hakikisha unapanga vyema vyombo vya kulia (feeders) na vyombo vya maji (drinkers) katika mpangalio ambao utawawezesha vifaranga kula na kunywa maji bila kuapata shida.

★ JOTO

Nunua thermometer (kipima joto) na kiweke katika urefu unaozidi vifaranga kidogo lakini iwe mbali na heater or chanzo chochote cha joto.

Rekodi joto la kila siku kwa kawaida joto sahihi la vifaranga linapaswa kuwa kati ya 40-41 degree centrigrade. (na njia sahihi ya kupima joto la vifaranga chukua miguu ya vifaranga na uweke katika shavu au shingo lako ukisikia miguu inajoto jua vifaranga wapo kwa joto sahihi lakni ukisikia miguu ni ya baridi basi jua ya kwamba vifaranga wanahitaji joto zaidi na hivyo unashauliwa kuongeza joto).

Joto ni muhimu sana katika ukuaji wa vifaranga kwa wiki ya kwanza na hivyo ni vyema kulifuatilia kila siku kuepuka vifo visivyotarajiwa.

★ RATIBA MWANGA

Angalia jedwali katika picha hapo chini

Unashauriwa kuwapima uzito vifaranga/kuku wako kila wafikishapo siku ya 7,14,21,28 na 35kwa kutumia digital balance

★ MAJI

Mabadiliko yoyote katika unywaji wa maji ni njia sahihi au kihairishi moja wapo ya kwamba maji huvuja, kuna tatizo katika chakula au magonjwa. (Kuku kutokunywa kielezo tosha ya kwamba kuku wako wana shida).

Kwa kawaida inatakiwa drinkers 4 kwa kuku 100 na hakikisha maji ni masafi na salama na yanapatikana katika banda kwa masaa yote 24 na jua ya kwamba upungufu wa maji hupelekea kuku kudumaa.

★ CHAKULA

Chakula kinapaswa kuwekwa katika tray za mayai zilizo safi na salama, gunia or magazeti kwa siku saba za mwanzo kuwawezesha vifaranga kula chakula na baada ya siku saba taratibu anza kuwawekea chakula feeders.

Kwa kawaida inashauriwa kuweka tray 4 za chakula kwa vifaranga mia moja. (na hii inafaa kufiti eneo la 50% tu la brooding area).

Kwa feeder za kawaida inashauriwa inapaswa kuwa feeders 3 kwa kuku 100, na hakikisha chakula kinahifadhiwa sehemu salama mbali na mwanga, majimaji na panya. Epuka kuwalisha vifaranga chakula ambacho kina unyevu unyevu au fangasi wa chakula.

Ili kufahamu kama vifaranga wako wanakula chukua vifaranga 5 kama sampuli waangalie baada ya masaa8 then masaa 24 kama wamekula nah ii hufanya kwa kugusa mfuko wa chakula taratibu ukikuta mfuko wa chakula uko umetuna na unagusika jua ya kwamba wamekula na kinyume ya hapo ni kweli pia.

★ AINA YA CHAKULA KWA VIFARANGA

a) Chick starter

Wape 0.5kg kwa kifaranga kimoja kikiwa katika mfumo wa pellet kwa muda wa wiki 2

b) Grower

Wape 1.5kg chakula cha ukuaji kwa vifaranga kikiwa katika mfumo wa pellet kwa muda wa wiki 2

c) Finisher

Wape 1.5kg chakula cha umaliziaji kwa muda wa wiki mbili kabla ya kuwachinja au kuwauza.

★ CHATI YA ULISHAJI WA KUKU BROILER

Angalia katika jedwali hapo chini

ZINGATIO: Jedwali hili lipo applicable kwa broiler waliokuzwa kwa wiki 6 pekee kwa wale wanaowatoa ndani ya wiki tano gharama za uendeshaji pia zinapungua.

★ BROILER TIPS

a) SIKU 1-5

Wape glucose na mchanganyo mmoja wapo kati yah ii ifuatayo;
Neoxyvital au otc plus na typhorium au trimazin
Fluban na vitamin kama vile broiler boost au aminovit au supervit broiler au vitalyte

CHAKULA

Weka vigostart ambayo ina ridocox kwenye chakula, kilo moja kwa mfuko kuanzia wiki ya kwanza hadi nne ili kuzuia coccidiosis, baada ya kuacha endelea kutumia ridocox 200g/tani kwa kuzuia coccidiosis hadi wiki 1 kabla kuwauza kwa nyama.

★ SIKU YA 6

Vitamini (vitastress)

★ SIKU YA 7

Chanjo ya newcastle masaa mawili tu, halafu endelea na maji ya vitamin (vitastress)

★ WIKI YA PILI

Chanjo ya gumboro masaa wawili tu, halafu endelea na vitamin (vitastress)

★ WIKI YA TATU

Wape doxycol au ctc 20% au anflox gpld au fluban na amprolium,vitalyte au vitastress,molasses kwa siku 5-7

★ WIKI YA NNE

Hakikisha kuku wa nyama wanakuwa katika dozi kubwa ya vitamin (vitastress/vitalyte/broiler boost/supervit broiler)

★ WIKI YA TANO

Hakikisha kuku wa nyama wanakuwa katika dozi ndogo ya vitamin (vitastress/vitalyte/broiler boost/supervit broiler)

★ WIKI YA SITA

Wape kuku maji ya vitamin asubuhi na matupu jioni

Na baada ya hapo kuku wako watakuwa wako tayari kuingia sokoni kwa ajili ya mauzo

★ HITIMISHO

Na imani kwa muongozo huo hapo juu utakuwa msaada mkubwa kwa wale ambao wangependa kuanzisha project ya kuku wa nyama na pia kwa wale wenye project hiyo.

Kama upo na uhitaji wa muongozo bora wa kuku wa mayai na pia formular za kutengeneza chakula cha Kuku ili kuepeuka gharama zaidi basi usisite kuwasiliana nasi nasi tutaitikia wito wako

Kwa maswali na msaada zaidi usisite kuwasiliana nami
C.E.O ( JMVC)
464bd28e64ec39af880e0018369f467d.jpg
0ade42736bc1cdb649c97aa62c435d78.jpg

Dr : Theriogenology
Phone : +255686236365 (whatsaap)
Dr. za kwako mkuu natumaini ni mzima
samahani ni kwa kampuni zipi naweza pata mbegu nzuri za kuku BROILERS?
 
Uzuri wake ni upi tofauti na kuku wengine?
Sasso ni kuku Bora Sana Kwa mfugaji anayefuga kisasa na kienyeji Yoda Sasso wanavumilia mazingira na magonjwa. Wanafugwa kienyeji, unaweza kuwaachia wakatembee kwenye shamba. Wape chakula kiasi asubuhi Kisha waachie waende kujitafutia na jioni wape chakula kiasi tu na yatanenepa Sana.
Wana uzito mzuri, wanakuwa haraka kiasi kwamba ukimlisha vizuuri miezi 4-6 unamuuza Bei nzuri 12,000 - 20,000.
Sasso wanataga mayai na anaweza kutaga kila siku.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom