Ufugaji wa kuku saso na ufugaji wa nguruwe

UWOGA=UMASKINI

JF-Expert Member
Dec 30, 2013
2,384
980
wadau niko kwenu hapa najaribu kufikiri kuanza UFUGAJI Sasa nawaza kuhusu UFUGAJI WA NGURUWE au kuku SASO naombeni ushauri wenu nataka kutengeneza pesa za ada mwakani.

NIKO MKOANI NA MTAJI WANGU NI LAKI TANO
 
1. Je, nchakula aina gani kinapatikana kwa wingi kwenye huo mkoa (mkoani)??
2. Je, hiyo laki tano (500,000) ya mtaji ni pamoja na ujenzi wa banda la kufugia??
3. Je, mkoa uliopo (mkoani) kipi kina soko kati ya kuku (saso) na mdudu??
4. Je, unajiona kabisa kwamba unaweza ukafuga ndani ya wiki 7 zilizo baki, na ukapata faida kwaajili ya ada mwakani pasipo kupitia changamoto yeyote??
5. Hua nashangaa mtu anapo kuja na wazo alafu anasema yupo mkoani, huvi mkoani ndio mkoa upi hapa Tanzania??
 
ungesema uko mkoa gani ingekua rahisi pia kujua mkoa huo kati ya kuku na nguruwe kipi kina soko zaidii...
But ukihitaji kufuga nguruwe nitafute nina experience nao na ninafuga wengi sana na kwa mda mrefu, nitakufundisha kwa vitendo na mifano iliyo hai sio kwa maandishi
 
Fedha yako ni ndogo kupata faida ya kueleweka ya haraka.

Jaribu mambo mengine katika hii chain ya ufugaji kama. Kununua kuku kwa wafugaji na kukaanga kuuza mtaani
 
1. Je, nchakula aina gani kinapatikana kwa wingi kwenye huo mkoa (mkoani)??
2. Je, hiyo laki tano (500,000) ya mtaji ni pamoja na ujenzi wa banda la kufugia??
3. Je, mkoa uliopo (mkoani) kipi kina soko kati ya kuku (saso) na mdudu??
4. Je, unajiona kabisa kwamba unaweza ukafuga ndani ya wiki 7 zilizo baki, na ukapata faida kwaajili ya ada mwakani pasipo kupitia changamoto yeyote??
5. Hua nashangaa mtu anapo kuja na wazo alafu anasema yupo mkoani, huvi mkoani ndio mkoa upi hapa Tanzania??
Dar si mkoa kwa mujibu wa wakaazi wa Dar wa maeneo ya Vingunguti,Kigogo,Tandale......
 
Fuga nguruwe tu , wanakula chochote , kuku watakuliza mpaka uzimie kwanza kukija wenge la magonjwa wanapukutika wote
 
Fug nguruwe mkuu. Mimi nimeanza kufuga sasso mwezi wa 8. Wako 100 tu ila hiyo gharama ni nyingi sana. Nilitaka kuwauza wakiwa na miezi mi2. Ila niliona watu hawafiki bei ninayotaka. Nimepambana nao na mpaka sasa wako 76 wameshakua niwauze sikukuu hizi. Niache kama 30 tu wa kutaga. Ila wanagharama sana. Na wanahitaji muda wa uangalizi kuanzia wakiwa na siku moja. Usafi wa kutosha. Wangu walipata ugonjwa kuna walikufa kama 25 nilitaka kuchanganyikiwa. Nikapata usaidizi wa daktari mpaka sasa wamekuwa na miezi 4 hawapati tena magonjwa kirahisi.
 
ungesema uko mkoa gani ingekua rahisi pia kujua mkoa huo kati ya kuku na nguruwe kipi kina soko zaidii...
But ukihitaji kufuga nguruwe nitafute nina experience nao na ninafuga wengi sana na kwa mda mrefu, nitakufundisha kwa vitendo na mifano iliyo hai sio kwa maandishi
Unafugia wapi mdau? Na una breed gani?
 
ungesema uko mkoa gani ingekua rahisi pia kujua mkoa huo kati ya kuku na nguruwe kipi kina soko zaidii...
But ukihitaji kufuga nguruwe nitafute nina experience nao na ninafuga wengi sana na kwa mda mrefu, nitakufundisha kwa vitendo na mifano iliyo hai sio kwa maandishi
Naomba elimu mkuu nahitaji kuingia kwenye kuku, mbuzi na nguruwe. Uzoefu wako tafadhali
 
Back
Top Bottom