Ufugaji wa Kuku wa Kisasa: Fahamu Mbinu, Faida, Changamoto na Masoko

Kipindi hiki cha CORONA soko la kuku wa nyama limekaaje? Nataka niingize mzigo bandandani mnanishaulije wana JF.
 
Kipindi hiki cha CORONA soko la kuku wa nyama limekaaje? Nataka niingize mzigo bandandani mnanishaulije wana JF.
Unaweza kuingiza kuku ila fanya yafuatayo

1.Kama una plan ya kuingiza kuku 1000 Basi wagawe kwenye batch 3 ili watofautiane uwatoe kwa awamu tatu

2.Soko limeshuka kidogo maana vyuo vimefungwa ,social events sio kihivyo kwahiyo lazima uende mdogo mdogo

3.Punguza matarajio yako hasa upande wa faida


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habar wakuu Hivi hawa kuku aina ya Kuroiler, jike anaweza kupandwa na jogoo wakienyeji na akataga mayai?
pia vp kuhusu jogoo wa kuroler anaweza kumpanda mtetea wakienyeji na akataga AU NILAZIMA WAPANDANE WENYEWE KWA WENYEWE?
 
Habar wakuu Hivi hawa kuku aina ya Kuroiler, jike anaweza kupandwa na jogoo wakienyeji na akataga mayai?
pia vp kuhusu jogoo wa kuroler anaweza kumpanda mtetea wakienyeji na akataga AU NILAZIMA WAPANDANE WENYEWE KWA WENYEWE?
1. Kuroiler anaweza pandwa na jogoo akatarubishwa

2. Jogoo wa Kuroiler pia anaweza panda kuku yeyote akarutubisha
 
Shukrani sana mkuu HDMI
Nina swali jingine ..
Je hawa Kroiler unaweza kuwafuga kienyeji yn ukawaachia tu ndani ya fensi nawakachakua chakua chakula nakudonoa donoa majani wenyewe au niwandani kwandani tu kama hawa broiler
 
NAUZA BIASHARA YA CAR WASH:

LOCATION: KINONDONI BLOCK 41
NAMBA YA SIMU: 0717 26 33 77

MAELEZO:

MACHINE ZOTE, UJENZI, VYOMBO, SIMTANK, KODI n.k JUMLA: TZS 7,000,000
NIMEBAHATIKA KUPATA KAZI SERIKALINI NA KITUO CHANGU KIKO MKOANI, SO NIMEAMUA KUUZA HII BIASHARA.
 
GHARAMA UFUGAJI WA KUKU WA NYAMA.

Katika ufugaji inawezekana umekuwa ukiona miradi ya watu ukawa unaona miradi ya watu jinsi ilivyo mikubwa.unapenda Sana kutembelea katika miradi mbalimbali, pia na wewe unawazo la kufuga lakini unashindwa kujua ni mtaji shingapi utakaotosha kuanzishia ufugaji wa kuku.

Ndugu siyo lazima wewe kuanza na mradi mkubwa kama unanyoiona ya wengine. Hao mpaka kufika hapo wamechukua muda kidogo na wamekutana na changamoto nyingi.

Hivyo hata mtaji mdogo kabisa unaweza anzisha mradi wako wa ufugaji wa kuku baada ya muda na wewe utakuja kutembelea katika mradi wako.
Katika ufugaji wa kuku kuna aina nyingi za kuku leo tuangalie katika ufugaji wa kuku wa nyama broiler.

Kila aina ya kuku kuna vitu vya muhimu na haya ni mahitaji ya ufugaji wa kuku wa broiler.
Eneo
Mtaji
Banda
Vifaa
Chakula/maji
Madawa
Vifaranga

Hayo ndo mahitaji kwa kuku wa broiler leo hatuta ongelea hayo mahitaji, tutaanza kuongelea gharama za matunzo kuanzia kununua vifaranga hadi kuuza na faida yake ipoje! Kwa kawaida watu hujua kuku mpaka uwe na mtaji mkubwa hapana! Hata mtaji wa laki 550,000/= unaweza kufuga kuku broiler na ukapata faida jinsi unavyoendelea kufuga na mtaji wako utaendelea kukuwa.

Hapa tuananza na mtaji mdogo wa kuanzia vifaranga 100. Kuna makampuni mengi yanauza vifaranga. Kuna bei tofauti tofauti shng 1700,shng 1800 na 1900 kwa hapa tutatumia vifaranga wa 1800.
Utanunua vifaranga 100×1800=180,000/=

Siku umeenda kuchukua unatakiwa uku nyuma uwe umekamilisha yafutayo.
Banda umesafisha vizuri, unatenga Kona moja ambayo unatengeneza umbo la duara au box ndani ya duara kutakuwa na maranda na pia weka magazeti, magaziti usaidia maji yakimwagika utaweza kusafisha kirahisi.
Bila kusahau vyombo vya chakula na maji, chanzo cha joto unaweza tumia jiko la mkaa, balbu, chungu au taa ya chemli.

MATUMIZI KATIKA CHAKULA.

Vifaranga 100 kwa wiki 4 mpk 5 unaweza tumia mifuko 5 ya kg 50 mpaka kuuzwa.

Wiki mbili za mwanzo??

Starter pilet mfuko mmoja 60000 kwa mifuko 2.
60000×2= 120,000/=

Wiki tatu.

grower pilet mfuko mmoja 59,000/=

Wiki nne.

Finisher pilet 59,000/=×2. = 118,000/=

Chanzo cha joto. 15,000/=

Pesa ya akiba 30,000/=

Madawa na maranda unaweza gharimu 35,000/=

JUMLA?
180,000 + 120,000 + 59,000+ 118,000+ 15,000 + 30,000 + 35,000 = 547,000/=

Kwahiyo matunzo Hadi kuuza yata gharimu 550,000/=

Katika kuuza kuku mmoja shng 7000 × 100= 700,000/=

Faida itakuwa shng. 150,000/= kwa mwenzi mmoja?
Utakavyoendela kufuga mtaji wako utaongezeka. Na utazidi kuwa mzoefu katika ufugaji wa kuku wa broiler. Na pia bei ya chakula utofautiana na hii bei niliotumia hapo kutokana na chakula kupana lakin kuna she chakula kg 50 unaweza uziwa 55,000/=.
2021-07-09_09%3A06%3A21.jpg
 
Nahitaji vifaranga broiler kama 100 nataka kuanza ufugaji wa kuku wa kisasa/kizungu. Mwenye nao ani PM.
 
Hela nyingi inaenda kwenye chakula.hivi akuna namna bora ya kupunguza gharama za chakula cha kuku?
 
Hela nyingi inaenda kwenye chakula.hivi akuna namna bora ya kupunguza gharama za chakula cha kuku?

Kuna homemade ration formulation
Inareduce sana cost kaz yako itakua kukusanya material then unachanganya mwenyewe, ila hapa shida hua inakuja kwenye kupangilia ratio ya chakula, wengi wanachemka hapa
 
Shukrani sana mkuu HDMI
Nina swali jingine ..
Je hawa Kroiler unaweza kuwafuga kienyeji yn ukawaachia tu ndani ya fensi nawakachakua chakua chakula nakudonoa donoa majani wenyewe au niwandani kwandani tu kama hawa broiler

Samahan kuingilia swal but naweza kulijibu
Kroiler ni cross breed, body immunity yao ni kubwa kias ukicompare na broiler au layer so wanastahimili harsh environment so unaweza wafuga kwenye semi intensive au hata free range wanamudu, vyovyote tu vile upendavyo
 
Kwa wale wafugaji hasa wa mikoa yenye gharama kubwa ya chakula sasa Bei kubwa ya chakula isikukwamishe kufuga. Sasa unaweza pata chakula cha mifugo pia nafaka mbalimbali kwa bei halisi ya mkoani

Unachotakiwa kufanya ni kuwasiliana na nasi katika group letu huwa tunapakia na kusafirisha hadi mkoa ulipo kwa bei ya mkoani na nafuu zaidi

Vyakula unavyoweza pata
1. Pumba za mahindi
2. Pumba za mpunga laini kwaajili ya nguruwe
3. Mashudu
4. Uduvi
5. Chakula cha kuchanganywa
6. Na vyakula vingine kwa order ya mteja husika kama uduvi, mahindi, chenga za dagaa, nk



 

Similar Discussions

Back
Top Bottom