Ufisadi wa Nape huu hapa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ufisadi wa Nape huu hapa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Msema hovyo, Jul 15, 2011.

 1. Msema hovyo

  Msema hovyo Senior Member

  #1
  Jul 15, 2011
  Joined: Jul 3, 2011
  Messages: 195
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Inaonekana huyu bwana mdogo hajui vizuri definition kamili ya ufisadi. Amewakomalia akina Rostam, Lowassa na Chenge kwamba ndo mafisadi wakubwa ndani ya CCM huku akisahau ufisadi mkubwa ambao yeye analifanyia taifa. Nape hivi sasa anaendelea kupokea na kutafuna mshahara kutoka kwa walipa kodi kama mkuu wa wilaya, ili hali kazi ya ukuu wa wilaya haifanyi tena.

  Muda wote Nape yupo kwenye mikutano ya CCM, ni saa ngapi na kwa muda gani anawatumikia wananchi wale ambao amepewa jukumu la kuwatumikia? Na je ule mshahara wa ukuu wa wilaya anaoendelea kulipwa anaupokeaje ilihali hafanyi kazi ya ukuu wa wilaya? Anaweza kuuelezeaje huu wizi anaoifanyia Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kupokea mshahara wetu ilihali hafanyi kazi?

  Tayari Rostam keshajivua gamba, the next awe ni Nape na Kikwete. Hawa ndo mafisadi wakubwa na ndo magamba ya ukweli ndani ya CCM. Wale akina Rostamu walikuwa wanapitishiwa tu hela zinazoibwa na hawa hawa akina Nape na Kikwete. Ni lazima kieleweke. Sisi kama wanaCCM hatutakubali gamba hili (Nape) liendelee kuwemo ndani ya chama chetu.
   
 2. eliesikia

  eliesikia JF-Expert Member

  #2
  Jul 15, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 423
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 45
  NAPE ni fisadi kwa kuwa cheo alipewa kwa dhana ileile ya kumuenzi mzee Nnauye.. Ubungo walionyesha ukweli kwa kumpa kura kiduchu.... hana hadhi ya kuwa mtu wa watu
   
 3. Msema hovyo

  Msema hovyo Senior Member

  #3
  Jul 15, 2011
  Joined: Jul 3, 2011
  Messages: 195
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Unajua kwa jinsi Kikwete alivyo fisadi hawezi kamwe kumpa cheo mtu asiyejua ufisadi. Maana akimpa mtu anayejali haki na usawa lazima atamuumbua. Kwa hiyo Nape amepewa nafasi hiyo kwa misingi ya ufisadi wake. Kama Kikwete anauchukia ufisadi kwanini hujamwachisha cheo kimojawapo kabla ya kumpa kingine. Yaleyale ya makamba: katibu mkuu wa CCM na mbunge wa kuteuliwa. Pu mba fu kabisa. Hili liinji bwana, bora tu mimi msema hovyo nimeanza kulipiga mnada tu. Lakini nashangaa hajajitokeza mtu kutaka kununua.
   
 4. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #4
  Jul 15, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  hii inaitaji ufafanuzi kutoka kwa NAPE,
  WIZI SIO MCHEZO MZURI HATA KIDOGO
  milioni mbili kwa mwezi bila kufanyakazi ni nini? pension au tanzania tunatoa benefit kwa wapiga yowe
   
 5. H

  Honey K JF-Expert Member

  #5
  Jul 15, 2011
  Joined: Sep 14, 2008
  Messages: 629
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Msemahovyo, nilishaacha ukuu WA wilaya DC, SIKU TU NILIPOTEULIWA KUWA KATIBU WA NEC ITIKADI NA UENEZI NILIACHA U DC, GARI YA SERIKALI NA STAHILI ZOTE ZA DC IKIWEMO NYUMBA NA OFICE. ACHILIA MBALI MSHAHARA, TENA PESA ZANGU ZA KUACHA KAZI SIJALIPWA MPAKA LEO, HII ILIKUWA PROPAGANDA YA PADRI MMOJA NILIPOULIZA MSHAHARA/POSHO YAKE.....SIJAWAHI KUPOKEA MISHAHARA MIWILI.
   
 6. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #6
  Jul 15, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Nape njoo useme uache kukomaa na Slaa bure kila kukicha .Mie nilisha wahi kuhoji hapa juu ya Nape kuwa Mkuu wa Wilaya lakini kila siku yuko mitaani .Watu wakasema oh Lunyungu fitina .Haya kasema huyu msemahovyo .Mie kama wengine nangojea kuona majibu ya mpayukaji wa CCM .
   
 7. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #7
  Jul 15, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,267
  Likes Received: 19,410
  Trophy Points: 280
  Rostam will bounce back. are you ready?
   
 8. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #8
  Jul 15, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Kama kosa kubwa ambalo CCM wamefanya kukuweka wewe katika nafasi uliyo nayo. Kiongozi mahiri mwenye itikadi sahihi na heshima mbele ya jamii yake ni heshima kwa kila mtu bila kujali cheo na jinsia.

  Nape una tabia mbaya sana ambayo ni kinyume kabisa cha maadili na falsafa ya uongozi na kwa njia hiyo inakuvunjia heshima yako uliyokuwa nbayo.

  Kiongozi safi mwenye elimu na kuelimika, busara na hekima hujenga hoja kifasafa kutokana itikadi za chama chake, kati hawezi kuanza kumshambulia mtu binafsi.

  Nape tunashindana hoja za kiitikadi na hoja ikikushinda usikimbilie kumvua nguo mtu unajiaibisha, maana huenda wewe ukivuliwa nguo utaonekana na makengeza kuliko unaowavua nguo.

  Kiongozi mahiri hupinga hoja hapingi mtu. Tunachukia hoja mbaya hatumchukii mtu. Tutakufundisha mpaka lini hadi uelewe?

  Jaribu kujifunza lugha nzuri au tukupeleke darasani kusoma elimu ya usemaji yaana effective speaking. Hali ilivyo na unavyoendelea kufoka unaharibu zaidi chama na wajihi wake. Umemwona Katibu kuu wako Mukama alivyotulia? Busara ndivyo inavyotakiwa yakhe.
   
 9. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #9
  Jul 15, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Nape umeoa hujaona hayatuhusu. Una nyumba au huna hayatuhusu. Ukiwa katika uringo wa ngumi unatakiwa ufuate maelekezo ya sheria na taratibu za mchezo wa ngumi, na ukienda kumtandika mwenzangu ngumi ya tumboni au kisogoni unakosa point. Kwa maneno mengine unapopiga ngumi kinyume cha sheria na taratibu zake ni ishara dhahiri kwamba umeishiwa ufundi na kwa namna nyingine unazidiwa.
   
 10. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #10
  Jul 16, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Kaka umempa huyu dogo maneno mazito lakini hawezi kujifunza .Kumshambulia Dr.Slaa kwa maneno ya ubinafsi hakika ni ujuha .Hivi hata kwenu hakuna wakubwa ? Slaa he never talk about personalities .Wewe una sura kama ya mwana dada mbona hatusemi hapa ? Lakini wewe kila kukicha unakosa heshima siasa gani hizo ? Una deal na watu wa kada tofauti tia akili kwanza wacha kukurupuka .
   
 11. HISIA KALI

  HISIA KALI JF-Expert Member

  #11
  Jul 16, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 694
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tatizo linaweza kuwa ni uwezo. Hivyo usimlaumu sana huyu jamaa. Hata Man United ilipofungwa na Barca 3-1 kwenye fainali ya kombe la kilabu bingwa ya Ulaya, kocha wao na mashabiki wote hawakuwalaumu wachezaji wa Man United kwani walijua wachezaji hawakuwa na uwezo wa kuwafunga Barca.
   
 12. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #12
  Jul 16, 2011
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 863
  Trophy Points: 280
  Hujalipwa na nani, na kwa nini hujalipwa. Je, seriikali ya CCM ina utaratibu gani wa kuwalipa watu mafao yao baada ya kustaafu/kuacha kazi?
   
 13. Bukanga

  Bukanga JF-Expert Member

  #13
  Jul 16, 2011
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 2,863
  Likes Received: 714
  Trophy Points: 280
  Huyu mwanasiasa wa CCM mjinga, mpumbavu na ni **** hasa, arudi shule asome vinginevyo...
   
 14. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #14
  Jul 16, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  SHEHE sema former padri unadhalilisha kanisa, ina maana wewe ukifa tutakuita NAPE bila RIP?
  Hacha udini bana mtu mzima wewe,
  hata kama unajaribu kusema hicho chama ni cha kikatoliki ina maana wakatoliki hawana haki ya kuwa na chama cha siasa hapa nchi?

  sometime respect urself kila ukija hapa una lalamika watu wanakutukana matusi lakini mbona wewe ndiye muanzilishi wa matusi, ina maana CCM ndivyo mnavyoitana kwa kufuata dini? harafu baadaye mana sema baba wataifa bla bla bla,
   
 15. G

  Given Member

  #15
  Jul 16, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 81
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 15
  Ndugu yangu Nape, tulia jitafakari na uchukue hatua. Unajiaibisha, unaaibisha chama na unadhalilisha jina Nnauye! Kuna wakati ulijenga kaheshima ktk jamii, ukahesabika kama kijana mzalendo na jasiri. Sasa heshima yoote unaifuta kwa kasi ya ajabu kwa 'uropokaji'. Ueneze sera siyo 'mipasho'! Hekima, heshima na maadili hayana chama! Na nafasi uliyonayo yataka hekima!
   
 16. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #16
  Jul 16, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Thats right dude umeguswa umejibu kwenye wakati sahihi jibu sahihi unaachana na mengine unaendeleza POSITIVE for your office.Nimependa mchango wako kwenye thread hii.Cha msingi mtatusaidia kujibizana kwa hoja.Hoja ndio zitakazo amua nani aaminiwe na umma.Matusi ayajengi kwa kuwa watu wanashida na makosa yamefanyika kama ni chama tawala kisahihishe makosa yake na kama ni chama cha upinzani wajenge chama chao kiaminike kwa umma,ili nao wapate hayao madalaka ya kuwatumikia Watanzania.

  Nilishatoa ushauri usitukane wenye ufahamu watashindwa kutofautisha tofauti yako na watangulizi wako.Tunataka mabadiliko yoyote kati ya vyama vyenye kuweza kuipatia Tanzania na Watanzania Maisha mema basi ategemee support ya umma.

  Ila tambua uko kwenye mapambano na mapambano haya yanataka busara yenye maamuzi yaliyo tathimini faida zake kuliko ushabiki wa kisiasa.Zama ulizo nazo sio zile za kibabe za chama dume au chama madalaka,ukiweka wazo hilo kwenye utendaji wako ITAKULA KWAKO NA ITAKULA KWENU WEWE NA CHAMA CHAKO CHA MAPINDUZI.Wazee wakitaka kukuweka kwenye mwelekeo unaona wa kukufanya ujisikie UBABE please UTAKIMALIZA CHAMA CHENU,kwani kwa sasa WEWE NDIE MWENYE JUKUMU LA KULUDISHA MATUMAINI YA WANACHAMA WENU NA MASHABIKI WENU.

  Nyenyekea na kujali umma,manake tizama umma kila siku ya umma unavyozidi kuwa na hasira dhidi ya Serikali inayoongozwa na chama cha Mapinduzi.Ni zama na nyakati mbaya katika historia ya chama cha Mapinduzi.Kwa Msaada tumia wazee walio waadilifu katika kuludisha jina la chama chenu.Msitumie viongozi walio madalakani ambao wengi wao wamebobea kwenye tuhuma,tumia wazee ambao wako mbali na uchafu,wale ambao walijijengea majina japo hawana CaSH bali wana aminika kwenye jamii.

  Mkiwatumia msiangalie huyu alikuwa kambii ya nani,mkiangalia hilo MMEUMIA,watu kama JOSEPH SINDE WARIOBA,CLEOPA DAVID MSUYA,na wengineo wengi watarudisha matumaini ya wengi.

  Ila kamwe kamwe msifanye kazi na mtu aliyetimu ya MAFISADI huko ni HATARI kwa kuwa UMMA unamtafuta MCHAWI wa tatizo la Maisha magumu waliyonayo,Watanzania wa sasa wanaamini kuwa ugumu wa maisha waliyo nayo umasasabishwa na MAFISADI.
   
 17. segwanga

  segwanga JF-Expert Member

  #17
  Jul 16, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 2,790
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  NAPE UNAZIDI Kujidhirishia kwamba wewe hufai kuwa kiongozi.Hivi huwa unafikiria kabla ya kuandika? Nadhani nyumba ya vioo JK inakupa kiburi mpaka unarusha mawe kwa kila mtu anayepita njiani.Unajijengea maadui ukiwa umesahau kuwa ccm inakoelekea yaweza kung'olewa na unasahau kuwa kuna maisha beyond politics.Wewe unaweza kushindana dr slaa? ninazidi kukupata zaidi na kuyakumbuka maneno niliyoyapata toka kwa shemeji yako kuwa UNAJIONA UKO JUU SANA KIASI KWAMBA UNAMSAHAU HATA MJOMBA WAKO AMBAYE NDIYE KILA KITU KWAKO.Kwa sababu hauna akili ndo unaona hicho cheo ndo umefka.NAKUHURUMIA kwa sababu upo kwenye black list ya bilionea RA na wewe pengine kwa sababu ya kuwa na akil finyu unajiona uko salama.We huwezi kujibu hoja kwa utulivu kama dr slaa anavyojibu?.Kumbuka kwenye siasa mpinzani wako anaweza akaprovoke wakati mwingine kwa kukutengenezea scandal ambayo lengo lake ni kukutegeshea ili ufunguke. Nenda udsm ukafundishwe siasa ukashagraduate uje jf
   
 18. segwanga

  segwanga JF-Expert Member

  #18
  Jul 16, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 2,790
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  NAPE UNAZIDI Kujidhirishia kwamba wewe hufai kuwa kiongozi.Hivi huwa unafikiria kabla ya kuandika? Nadhani nyumba ya vioo JK inakupa kiburi mpaka unarusha mawe kwa kila mtu anayepita njiani.Unajijengea maadui ukiwa umesahau kuwa ccm inakoelekea yaweza kung'olewa na unasahau kuwa kuna maisha beyond politics.Wewe unaweza kushindana dr slaa? ninazidi kukupata zaidi na kuyakumbuka maneno niliyoyapata toka kwa shemeji yako kuwa UNAJIONA UKO JUU SANA KIASI KWAMBA UNAMSAHAU HATA MJOMBA WAKO AMBAYE NDIYE KILA KITU KWAKO.Kwa sababu hauna akili ndo unaona hicho cheo ndo umefka.NAKUHURUMIA kwa sababu upo kwenye black list ya bilionea RA na wewe pengine kwa sababu ya kuwa na akil finyu unajiona uko salama.We huwezi kujibu hoja kwa utulivu kama dr slaa anavyojibu?.Kumbuka kwenye siasa mpinzani wako anaweza akaprovoke wakati mwingine kwa kukutengenezea scandal ambayo lengo lake ni kukutegeshea ili ufunguke. Nenda udsm ukafundishwe siasa ukashagraduate uje jf
   
 19. Msema hovyo

  Msema hovyo Senior Member

  #19
  Jul 16, 2011
  Joined: Jul 3, 2011
  Messages: 195
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Maelezo haya Nape hayatoshi. Ukuu wa wilaya hauachwi kienyeji, kuna process za kuuacha, na unatakiwa utuambie uliandika lini barua ya kuresign na ulikabidhi kwa nani hiyo ofisi ya ukuu wa wilaya. Kwa taratibu za utumishi, wa umma, utumishi huwa hauishi hadi pale utakaposimamishwa rasimi kwa barua. Je Bwana Nape una barua yoyote inayoelekeza kwamba wewe si mkuu wa Wilaya tena? Je una barua yoyote inayoeleza kwamba mshahara wako unasimamishwa kutokana na utumishi wako kubadilishwa au kukoma?

  Hatudanganyiki kirahisi hivyo mkuu. Wewe unakula mishahara miwili kwa kazi usiyofanya. Halafu ni aibu kwa mtu mkubwa kama wewe, katibu mwenezi wa chama kuandika habari za Padri na usiseme Slaa. Mbona umekosa uungwana kiasi hicho. Wewe ni fisadi tu, until you submit vivid evidences that show that you resigned from all posts you were granted by your fellow fisadi Kikwete.
   
 20. segwanga

  segwanga JF-Expert Member

  #20
  Jul 16, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 2,790
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Kama ndo marekebisho ya uongozi ambayo ccm wanataka yawavushe kwenye kipindi hki kigumu kwao ndio ya kutoa gamba (makamba) na kuweka gamba (nape) basi wameisha sababu huyu jamaa amedhihirisha siasa uchwara (Aziz,2011) za ccm. Nape unatuabisha unaibisha chama cha magamba.Hata malaria sugu ana busara mara mia zaidi kuliko wewe ambaye unawakilisha chama chenu
   
Loading...