mkuu wangu unapotukanwa na kukejeliwa wewe shukuru maana unapata mengi, hapo kwenye red umeeleza vizuri sana kuwa JF ni km shule, sasa mbona hubadiliki? mkuu majibu yako hayafananii na kiongozi kabisa, kitendo cha wewe kujibu ati kuwa kuna padri mmoja ndo anakuzushia hayo ni mambo ya mipasho, kwanini usingemtaja huyo padri na kanisa analosimamia? km JF ni shule kwako jifunze kutokana na ushauri unaopewa na watu.
CCM ni chama tawala,pia kinavyojiona ni chama mfumo.Tatizo langu aliko kwenye chama tawala,tatizo langu liko kwenye namna kinavyojiona kuwa ni chama mfumo, Nape hapa ndipo kwenye tatizo.Chama Mfumo ni mtizamo wa CCM kwa sasa,na sio ukweli [Reality] kuwa pasipo CCM HAKUNA TANZANIA.Ndio wakati wa mfumo wa Chama kimoja enzi ya Mwalimu alipoamua Tanzania kuwa Nchi ya mfumo wa chama kimoja kulingana na maono [Vision] yake kama kiongozi wa harakati za uhuru na hatimae kiongozi wa kwanza wa taifa huru la Tanganyika ilikuwa sawa,lakini baada ya Taifa.
Nyakati ni muda,na kila zama na vitabu vyake [Msemo wa Mzee Mwenyi]. Viongozi tulionao wengi ndani ya Chama cha Mapinduzi na Serikali ni wale ambao wengi wao bado
WAMO KWENYE MFUMO WA CCM NCHI.Hakika watambue kuwa mfumo huo alikuwa nao marehemu Baba wa Taifa na Mzee mpiga kinanda Marehemu Moses,na mfumo huo ilikwisha pale TAIFA lilipolizia kuingia mfumo wa vyama vingi.
Hayakuwa maigizo kuwafurahiisha wahisani bali ni hali halisi ya dunia kuwa binadamu anabadilika [EVOLUTION] kulingana na nyakati ambazo mwongozo wake ni nguvu ambazo sisi kama binadamu hatuna uwezo nazo, ambazo kwa lugha ya kibinadamu ndizo tunazoziita uwezo Mungu.
Wanasayansi wanasema hata watoto wanarithi
[INHERIT] aina fulani aina ya
VINASABA [GENETICS] kulingana na uwezo ambao mzazi anakuwa amefikia katika upeo wa kujitambua kulingana na zama au nyakati
kabla hajamzaa mtoto
husika.Kwa maana kuwa kama Mzazi amepitia chamgamoto nyingi na mbalimbali katika maisha na kuzikabili ikiwemo kupanda na kushuka kimaisha na kuweza kusimama imara au kuanguka kimaisha,mtoto atakayezaliwa na Mzazi huyu baada ya kupitia hatihati hiyo na mikiki ya maisha, tayari Mzazi huyu anavilisha vizazi vyake
vinasaba [genetics] ambavyo amevitengeneza kama alikuwa ni Mtu hasi au chanya [Negative or Positive] katika mambo yake kama vile uvumilivu, uelevu, ukatili, uchoyo, uongo, unafiki, upole, usikivu, uchangamfu,ugomvi, ulevi, uzinzi, utaperi, misimamo, utanashati,uthubutu na mengineyo yote yanayotufanya tuwe na haiba za ubinadamu tunazojitanabaisha nazo katika jamii.
Kwa ufahamu huo napata shida sana kujua wazee wengi [Viongozi] walio ndani ya CCM chama kikongwe wakikuona wewe Nape kama Mtoto wa Mkongwe na gwiji wa Propaganda za CHAMA CHA MAPINDUZI miaka hiyo arobaini na saba,wanafikiria ni SIASA za namna gani
WANAPASWA kuturithisha SISI WATANZANIA, WEWE na WATOTO WAO na TAIFA kama kizazi kinachohitaji kukabidhiwa mbio za vijiti na hatimae kizazi chao kujiendesha nao kama TAIFA,uku wakiwa na uwezo wa KIAKILI NA AFYA kujiendesha kama TAIFA.
Ni Siasa za kumuona kila aliye nje ya Chama cha Mapinduzi ni ADUI,ni siasa za kuamini kuwa bila CCM HAKUNA TAIFA.Japo Mwalimu alisema Kiongozi bora atatoka CCM.Lakini kwa kauli hiyo hiyo ya Mwalimu uenda alitumia msemo huo akaogopa zaidi kusema sana akihofi kuwa KUWA YU MTU ANAYEMWAMINI MUNGU.
INAWEZEKANA PIA KIONGOZI BORA SANA WA TAIFA LETU ANAWEZEKANA ASITOKE CCM.
Kwa kuwa kiviwango vya Nchi tayari tulishapata
BABA WA TAIFA,hivyo hatutapata tena
BABA WA TAIFA MWINGINE ILO LI WAZI.Tulichobakiza kitaifa kuwa na namba
- ya viongozi VIONGOZI WABAYA,VIONGOZI BORA,NA VIONGOZI BORA SANA.
Nikirejea kwenye kusudio langu la maelezo ya kinasaba, tayari wewe ni KUNDI TOFAUTI kati ya wewe na Viongozi hao,ambao kiumri ni BABA ZAKO NA BABU ZAKO.Wazee wetu hao yaweza kuwa upokeaji wa hoja yenye KUMPINGA YEYE [CHALLENGE] akachukulia UADUI lakini zama zako wewe ukaona ni CHANGAMOTO.Hayo yote ndio mabadiliko ambayo wapende wasipende waelewe Mzee Mwinyi aliposema kila zama na vitabu vyake alimaanisha kuna umri ukifika upaswi kuamua dhidi ya hatima ya kundi ambalo wewe wakati WANAISHI WEWE MUAMUAJI KAMA UMRI NI KIGEZO WEWE HUTAKUWEPO,WAO NDIO WATAKUA NA ATHARI NA MAAMUZI YAKO.
Ndio vision ya Mwalimu kuwa NANG"ATUKA,angetaka angebaki kama MUGABE kwani asingeweza.SIO KUWA NAPINGA WAZEE WASISHUGHULIKE NA SIASA HAPANA.WAKAE PEMBAENI NA WATUMIKE KAMA MIZANIA [BALANCE] kati ya MOTO NA KASI YA UJANA NA UKWELI WA MAISHA YA MWANADAMU [REALITY]. Kwa kuwa UTU UZIMA DAWA, NA JUNGU KUU ALIKOSI UKOKO.
Hivyo bsi kukurithisha siasa zao zile za vijembe,ambavyo wewe hapo juu UMEKANUSHA KUTUKANA,INGAWA KWA WENYE AKIRI JAPO NDOGO WANAJUA KUWA KUWA HUYO PADRI UNAMAANISHA NANI.
Najua soo hii uliianza mwenyewe,lakini kwangu nasema kukosea ndio kujua,kwangu mimi kama kijana mwenzio NISIYE EGAMIA CHAMA CHOCHOTE,TANZANIA KWANZA.Lakini wakati huo nikipenda kuwaona vijana kama ninyi pande zote mbili CCM na Chadema mkishindana kwa hoja zenye umakini na ufahamu kuwa uwenda siku za mbele mkapewa dhamana za maamuzi ya umma mkubwa wa Watanzania.
Hivyo kujitanabaisha kwa kuwa na haiba ya vijembe ambayo kwa zama hizi hilo ni mapungufu,ambayo MwanaCCM TAJIRI na MFANYABISHARA MKUBWA PENGINE KUPITA WOTE TANZANIA [Binafsi C Amini] ,AMEZIITA KUWA SIASA UCHALWA [GUTTER POLITICS].Azipendezi kuendelezwa nawe ukarithi kuwa ni mfumo wako wa kisiasa,kwa maana Mwalimu alipata kusema kuna mambo mazuri walifanya,lakini nyie [Sio wewe kwa maana ya zama] mnachukua mabaya mnaacha mazuri.So please chukua mazuri ambayo UNAONA yanakubalika kwenye jamii,mabaya yapotezee.
Manake ni heri kuwa tayari kuwajibika kwa kukataa usichoamini,kuliko kukubali kisa WAZEE wamekutuma.Wakati ukuta maamuzi mabaya ya leo hukumu yake kesho,ishi vizuri,ili kesho usisutwe na dhamira.Manake kilio cha nafsi ni KIFO HUKU UNATEMBEA, Binadamu wake UTU.Fanya mizaa yote lakini MAISHA YA WATU SI KITU CHA KUFANYIA MZAA KAMA VIONGOZI WENGI WATU WAZIMA WA CHAMA CHAKO WANAVYOYAFANYIA MZAA MAISHA YA WATANZANI.
Mrisho Mpoto aka MJOMBA,anasema maisha ya watu sio ya kuyafanyia MAJARIBIO [Rehearse],Maisha ni dhidi ya UKWELI [Reality].Mwisho anasema ni Dhambi kwa MUNGU.