Ufisadi wa Blandina Nyoni huu hapa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ufisadi wa Blandina Nyoni huu hapa!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by TUMBIRI, Feb 9, 2012.

 1. TUMBIRI

  TUMBIRI JF-Expert Member

  #1
  Feb 9, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,934
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kama nilivyohaidi, nimeendelea kuwasiliana na watumishi wa Wizara ya Afya na wa Wizara ya Maliasili na Utalii kuhusu Ufisadi wa Blandina Nyoni. Yafuatayo ni baadhi ya vitendo vya Ufisadi vya Mama huyu ambaye kwa wengine wanamuona kama mchapa kazi hodari asiyekuwa na doa na anaezuia mianya ya wizi:-

  1. Amekuwa akijilipa mshahara wa ziada kupitia Mradi wa Taifa wa Kudhibiti Ukimwi (NACP) wakati tayari serikali inamlipa mshahara wa ngazi ya Commissioner kupita Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)


  2. Ametengua utaratibu rasmi wa kila Idara ya Wizara ya Afya kuwa na afisa manunuzi wake badala yake ame centralize kwake mwenyewe. Kwa maana hiyo, manunuzi yote ya Wizara anamlazimisha (Comand) Mkurugenzi wa Kitengo cha Manunuzi kumpa kazi zote ndugu yake anaeitwa Donatha Koko.

  3. Amekuwa akicomand wizara kununua uniform za madereva, suti za sikukuu (Sabasaba na Nanenane) na Maua kutoka Mariedo bila kushindanisha na muuzaji mwingine kinyume na kanuni za manunuzi.

  4. Katika mikutano yote inayofanyika Wizarani, amekuwa akicomand kampuni ya Kaliula Catering Services kupewa tenda ya kulisha chakula washiriki tangu alipotua Wizarani kama Katibu Mkuu.

  5. Miezi mitatu iliyopita aliiteua kampuni ya Soft tech ambayo yeye ni mbia kwenda kukagua Accounts System ya Muhimbili kinyume na kanuni za kikaguzi kwa kuwa tayari ana ‘Conflict of Interest'

  6. Amekuwa akiongoza Wizara kwa kutumia Informers ambao kazi yao kubwa ni kumpelekea habari nani anasema nini na nani anasema nini kuhusu yeye binafsi na uongozi wake. Informers wake wakuu ni Elias Mkumbo ambaye ni dereva na Donatha Koko ambeye ni ndugu yake wa damu damu na ni afisa ugavi wa wizara

  7. Amemkopesha gari la serikali aina ya Suzuki Informer wake Elias Mkumbo (dereva) ambae kimsingi hastahili kukopeshwa gari kutokana na cheo chake. Kwa dereva wa serikali, anachoruhusiwa kukopa ni Baiskeli, Piki piki na Piki piki ya miguu mitatu (Bajaj)

  8. Amenunua vingamuzi vya magari (Vehicle Security and Fuel control system) vibovu kwa ajili ya magari manne kwa shilingi 1.3 Billion bila kufuata taratibu za manunuzi kwa kucomand Single source procurement kutoka kampuni moja yenye makao yake huko Israel. Manunuzi haya yamefanyika wakati Hospitali nchini zikiwa hazina dawa, Interns doctors hawajalipwa mishahara yao, watumishi wake wakidai fedha za likizo, uhamisho na vyuo vingi vya afya vilivyo chini yake vikiwa na madeni lukuki.

  9. Mwishoni mwa mwaka wa fedha 2009/2010 alihamisha kiasi cha Shilingi 1,968,475,931 mali ya Wizara ya Afya kwenda National Institute for Medical Research (NIMR) bila kibali cha hazina kwa matumizi yasiyojulikana. Fedha hizi zilikuja kuhojiwa na CAG katika ripoti yake ya serikali kuu ya mwaka 2009/2010

  10. Mwishoni mwa mwaka huo huo wa fedha alihamisha kiasi cha Shilingi 3,083,400,000 mali ya Wizara ya Afya kwenda Health Sector Development Project bila kibali cha hazina kwa matumizi yasiyojulikana. Fedha hizo pia zilihojiwa na CAG.

  11. Amelikosesha Taifa kupata fedha za Mfuko wa dunia mzunguko wa 11 (Global Fund Round 11) kwa kupitia Mradi wa Taifa wa kudhibiti Malaria Nchini (NMCP) kwa kushindwa kutumia fedha zote zilizotolewa na mfuko huo katika mizinguko ya nyuma. Kwa kifupi ni kwamba Global Fund hawatoi pesa wakiona una Significant unspent balances.

  12. Amekuwa akizuia uhamisho wa Chief Accountant (Bi Helen Saria Mwakipunda), Chief Internal Auditor (Bi Anna Joseph Mhere) na Director of Adminstration and Personnel (Bi Tabu Chando) kwa kile anachodai wanamsaidia katika utendaji wa Wizara. Amezua barua za uhamisho za Chief Accountant mara mbili, Chief Internal Auditor mara moja na Director of Administration and Personnnel mara moja. Ukweli ni kwamba amekuwa akizua uhamisho wa wakurugenzi hawa kwa sababu ni watu waoga na wamekuwa wakikubali chochote anachosema hata kama kinavunja kanunu na taratibu za serikali mfano katika maeneo ya Manunuzi.

  Kwa nini Chief Accountant (Hellen Saria Mwakipunda) na Chief Internal Auditor (Anna Joseph Mhere) wanamuogopa kama Mungu Blandina Nyoni? Ni hivi: Hellen Mwakipunda, alikua Junior staff kwa Nyoni, kipindi hicho Nyoni ni Mhasibu mkuu wa Serikali. Blandina Nyoni ndiye aliye mpandisha cheo Mwakipunda na kuwa Chief Accountant, kipindi hicho hata CPA hakuwa nayo. Anna Mhere alipata u-CIA akiwa na Advance Diploma in Accountancy - ADA tu. Ili swala lilikuwa linawashangaza watu wengi sana. Sasa kwa inferiority complex walizokuwa nazo hawa wakina mama, ni lazima wamuabudu Blandina Nyoni.

  13. Amemuhamisha aliyekuwa Kaimu wa Kitecho cha Ugavi Mzee Funga kwenda Hospitali ya Mirembe Dodoma kwa kukataa kununua Uniforms, suti na Maua kutoka kwa Mariedo kwa sababu alihoji ni kwa nini Mariedo watoe huduma wakiwa hawana Mkataba na hawajashindanishwa na wauzaji wengine.

  14. Amekuwa akihama hama na dereva wake toka Hazina alipokuwa Muhasibu Mkuu wa serikali hadi Wizara ya Maliasili na Utalii kama Katibu Mkuu. Pia amehama na dereva huyo huyo kutoka Maliasili hadi Wizara ya Afya kinyume na taratibu na kanuni za Utumishi wa umma ambazo haziruhusu kiongozi au mtendaji yeyote wa serikali kuhama na dereva au / na secretary

  15. Hamsalimii Naibu wake Waziri Bi Lucy Nkya kutokana na Naibu huyo kugoma kupangiwa dereva ambaye ni Informer wake. Hadi leo hii hamsalimii hata wakikutana kwenye kordo. Kinachowazungumzisha ni madokezo tu.

  16. Alikuwa na uhusiano mbaya na Naibu Waziri wake aliyeondoka Bi Aisha Kigoda kwa sababu ambazo hazijulikani. Kama ilivyo kwa Lucy Nkya nae pia walikuwa hawasalimiani.

  17. Akiwa Wizara ya Maliasili na Utalii, aligombana na Waziri wake Bi Shamsa Mwangunga na wakawa hawasalimiani hata wakikutana kwenye kordo

  18. Alipokuwa Mhasibu Mkuu wa Serikali alikuwa anateua ndugu zake na watu anaofahamiana nao na kuwapa vyeo vya u Chief Accountants na Chief Internal auditors bila kuwa na sifa kamili ya kupewa vyeo hivyo. Mfano kuhold CPA (T) na Masters.

  19. Amesababisha kushuka kwa morali ya utumishi kwa Wafanyakazi wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii. Hivi sasa ndiyo Wizara inayoongoza kwa kuwa na watumishi wengi walioamua kwenda likizo ya masomo ili kuepuka manyanyaso yake.

  20. Ameanzisha utaratibu ndani ya Wizara ya Afya wa kupokea Excheque kutoka hazina na anazihold bila kufanya distribution kwenye idara zake. Kutokana na utaratibu wake huu anafanya malipo kwa kutegemea mahitaji yanavyojitokeza. Utaratibu huu ni kinyume na kanuni za hazina za matumizi ya fedha za umma.

  21. Ikitokea kazi za Construction na maintanance anacomand tenda ipewe kwa Mzenzi Contractors Ltd. Alishinikisha Mzenzi ajenge ofisi za Wizara zilizopo Dodoma na akafanikiwa, baadae alishinikiza Mzenzi ajenge jengo banda la Maonyesho la Wizara kwa ajili ya Nane nane lilipo Dodoma na akafanikiwa na alishinikiza Mzenzi apewe tenda ya kufanya small maintanance wizarani kwenye ofisi yake, Ofisi ya Waziri na Naibu Waziri kwa ajili ya kuweka tiles na kuboresha vyoo na akafanikiwa.

  22. Katika section ya Matibabu ya nje amejenga Network na Hospitali za India ambazo zinapelekewa wagonjwa kuibill wizara inflated invoice prices.

  23. Amechukua mashine za kusafishia figo akishirikiana na Dk Linda Ezekiel pamoja na reagent na filter wakazipeleka Msasani kwenye Hospitali yao ambayo Blandina Nyoni ana shares.

  24. Amejenga banda la maonyesho ya sikukuu ya nane nane kwa kutumia fedha za NIMR kwa Shilingi 1.5 billion. Lakini banda lenyewe lililopo pale Nane nane Dodoma ukiliangalia tu kwa haraka haraka kwa macho thamani yake haizidi hata million 400.

  25. Ameingiza robo tatu ya vifaa bandia vya vipimo vya Ukimwi kutoka Korea Kusini.

  26. Ameingiza kinyemela bila kufuata taratibu za Manunuzi kampuni ya kufanya usafi ndani ya Hospitali ya Taifa Muhimbili.

  27. Ameshinikiza kampuni ya Jambo Concept Tanzania Limited kupewa tenda namba ME/007/2009-10/HQ/G/191 kwa ajili ya Printing and Placing of Billboards with TB/TBHIV bila kufuata taratibu za manunuzi. Kwa maelezo zaidi juu hii tenda soma maelezo kutoka 'someone' kama nilivyoyaatach hapa chini baada hii orodha

  28. Blandina Nyoni akishirikiana na Dr Deo Mtasiwa wamecheza mchezo mchafu katika tenda ya ununuzi wa Bajaj kama ilivyoratibiwa na Wizara ya Miundombinu kupitia tenda namba ME/015/2009 - 2010/S/06. Katika tenda hiyo bajaj moja ilinunuliwa kwa US$ 8,400. Kwa maelezo zaidi juu hii tenda soma maelezo kutoka kwa 'someone' kama nilivyoyaatach hapa chini baada ya orodha hii.

  29. Ametengua uteuzi wa Dr Mtimba kama Mkurugenzi Msaidizi na kumuhamishia Damu Salama Tabora na badala yake amemkaimisha Dr Budeba kwa miaka miwili mfululizo bila kumthibitisha kushika nafasi hiyo kinyume na taratibu za utumishi. Anafanya hivyo kwa sababu Dr Mtima hana urafiki naye.

  30. Ametengua uteuzi wa Dr Sawe ambaye angeenda India kuwapokea Wagonjwa na badala yake kamteua Dr Goroka ambaye kiudugu ni mtu na Mama yake. Hivi sasa kampeleka Dr Ngoka ambaye ni family friend wake pia.

  31. Ametengua uteuzi wa Dr Sawa anayesimamia uandikishaji / usajili wa Hospitali binafsi na kumpatia Mtoto wa Balozi Lusinde ambaye ni rafiki yake na walisoma nae High School Kilakala mmoja akiwa Form V mwingine akiwa Form VI

  32. Ametengua uteuzi wa Dr Muhame ambaye alikuwa Msajili wa tiba asilia na kumpatia Dr Naomi ambaye ni Mama Mdogo wake. Yaani yeye na Blandina ni mtu na mtoto wa binamu.


  33. Yeye ndiye chanzo cha masahibu yaliyowakabili Watanzania kwa kukosa huduma ya afya kwa zaidi ya Wiki mbili katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa kitendo chake cha kutaka kulipiza kisasi kwa Intern Doctors kwa kuwahamishia Mikoani pale walipodai haki zao ambazo ni stahili zao halali.

  Note: Orodha itaendelea kuongezwa kadri tunavyozidi kupata data kwa watu walio karibu na Wizara za Afya, Maliasili, Hazina na Muhimbili

  From 'someone'

  From
  assuredly4

   
 2. j

  jigoku JF-Expert Member

  #2
  Feb 9, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,347
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  Mkuu nashukuru kwa taarifa za kiuchunguzi,endelea kutoa madudu ya kifisadi ya Bi Nyoni anaejiona ni Mungu Mtu
   
 3. mchadema

  mchadema JF-Expert Member

  #3
  Feb 9, 2012
  Joined: Jul 8, 2011
  Messages: 412
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 33
  du kweli huyu mama anatakiwa afilisiwe just after stepdown
   
 4. BIG X

  BIG X JF-Expert Member

  #4
  Feb 9, 2012
  Joined: Nov 4, 2011
  Messages: 777
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Loh Loh Loh........ tapika tapika tapika yote mwaya. yasikukabe, isiwe fitina tu.
   
 5. kimatire

  kimatire JF-Expert Member

  #5
  Feb 9, 2012
  Joined: Nov 27, 2008
  Messages: 365
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Hizi tuhuma zote ni za kweli au zimekuja baada ya sakata la mgomo wa madaktari? Na kama zina ukweli mbona zimeachwa muda wote huo? Nakawia kuzikubali lakini pia najiuliza mtuhumiwa wa jinsi hii kwanini bado yungali madarakani tena kwa bidii ya kuhudumia umma?? Mengi ni marudio ya kile kinachosema kwamba anatumia madaraka aliyopewa vibaya!

  Lakini upande mwingine inasemekana ni mchapa kazi,Yamkini ana kundi fulani dogo lililoko madarakani linamtetea kwa gharama za kundi kubwa linaloumia.Kiburi na ujasiri huu kama upo basi una mashiko mahali fulani!

  Ni muhimu akawekwa pembeni na kushughulikiwa kwa maana ya kuchunguzwa! Haingii akilini Waziri Mkuu leo kuongea na wadau wa Afya kama hili halioni na kulishughulikia(hata mimi nisingemsikiliza!!).Ni mwisho mbaya kuwa na viongozi walio mzigo kwa jamii maskini kama tulivyo.Lolote jambo laweza kutokea na zaidi maisha ya waTZ yanapotea kwa gharama za kumlinda mtu wa aina hii.

  :canada:
   
 6. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #6
  Feb 9, 2012
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Mbele ya JK hapa hajaona lolote .Huyu mamakweli kama ni hivi kule Hazina alikosajekwenye EPA au anakula kwa kuwa analipwa fadhila ? Hii si kawaida labda ana pepowa wizi na roho mbaya .
   
 7. Eddy Love

  Eddy Love JF-Expert Member

  #7
  Feb 9, 2012
  Joined: Jul 25, 2011
  Messages: 12,859
  Likes Received: 6,313
  Trophy Points: 280
  Mtumeeee
   
 8. t

  testa JF-Expert Member

  #8
  Feb 9, 2012
  Joined: Jan 16, 2012
  Messages: 372
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Yethuu wangu na maria lo!Huyu mama ni balaa
   
 9. U

  Unstoppable JF-Expert Member

  #9
  Feb 9, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,049
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Quote (Mwishoni mwa mwaka wa fedha 2009/2010 alihamisha kiasi cha Shilingi 1,968,475,931 mali ya Wizara ya Afya kwenda National Institute for Medical Research (NIMR) bila kibali cha hazina kwa matumizi yasiyojulikana. Fedha hizi zilikuja kuhojiwa na CAG katika ripoti yake ya serikali kuu ya mwaka 2009/2010) Quote

  If this is true then: Dr Mwele Malecela anauhusiano upi na huyu mama? Kama sijakosea yeye ndio bosi wa NIRM; je haka kamchezo anakajua? Ukiangalia vizuri kuna chain ya watu fulani fulani inabidi wawajibike na huyu mama Nyoni if the accusations are true.
   
 10. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #10
  Feb 9, 2012
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Well, unadhani ni sehemu gani ya ofisi za kibongo haya yaliyoorodheshwa hapo juu hayafanyiki?
  Tafakari!
   
 11. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #11
  Feb 9, 2012
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Siyo pekee yake.

  Blandina analindwa na Seriklai ya CCM.

  Huyu dereva ni lazima awe anampiga kijiti Blandina, piga ua.
   
 12. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #12
  Feb 9, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,010
  Likes Received: 1,815
  Trophy Points: 280
  Mkuu nomesoma post nikagundua Mzee Funga ni shujaa. Katika mambo ya manunuzi, mkuu wa kitengo cha manaunuzi anatakiwa akomae kama Mzee Funga. Nafahamu kwa hakika katika huko kulazimisha huwa Nyoni haandiki popote na hivyo anaweza kumruka afisa manunuzi wakati wowote na jumba bovu likamuangukia.
   
 13. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #13
  Feb 9, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  dah, afadhali hapa hujapumbika kama kule kwa madokta
   
 14. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #14
  Feb 9, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Haitoshi kujiuzulu au kuwajibishwa kama haya yaliyosemwa ni kweli kwa asilimia hamsini tu basi sehemu yake ni jela tu!
   
 15. Ufunuo

  Ufunuo JF-Expert Member

  #15
  Feb 9, 2012
  Joined: Jun 6, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  bado n ile mashine ya kupima figo aliyohamisha muhimbili
   
 16. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #16
  Feb 9, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,010
  Likes Received: 1,815
  Trophy Points: 280
  Bahati mbaya unasoma ukiwa na kiwi ya macho wewe! Hakuna pumba yoyote. Tunaweza tukatofautiana kimawazo.
  Hizo pumba ziko wapi?
   
 17. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #17
  Feb 9, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  pamoja mkuu....
   
 18. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #18
  Feb 9, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,317
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  sasa tuhuma zote hizi wafanyakazi wa wizara walikuwa wanasubiri madaktari wawagomee?
   
 19. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #19
  Feb 9, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  kaka!!!

  sometimes watu wanakua wanajua maovu ila kama hujawaingia anga zao wanakupisha tu, ila sasa huyu mama amekula sana nyama za watu ameshajisahau.... ameingilia na bakuli za wenzake na wamemuamulia

  TO BE HONEST, SHE IS GREEDY, SELFISH, IGNORANT NA ANA DHARAU ZILE ZA FAVOR!!!

  YOTE HAPO JUU YANA ELEMENT KUBWA ZA UKWELI, ANALAZIMISHA TENDA, KUNA MOJA LA MABANDA YA MAONYESHO SABASABA, MIAKA 50 YA UHURU NA HATA KUTANGAZA UTALII WATU WAMESAHAU... ANA WATU WAKE WA KUFANYA HIZO KAZI
   
 20. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #20
  Feb 9, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,506
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Huyo mama ana dharau hata kwa ndugu zake wa kuzaliwa nae. But personal issues zisitupumbaze, let's focus.
  Hivi sheria ya maadili ya uongozi na ile ya kazi (hiyo #15 hapo) inaruhusu kununiana?
  The Boss alisema wanawake na kususa na kununanuna, haya yule shoga yake FF, bi Asha, akiwa prezidaa sijui atamnunia waziri mkuu?
   
Loading...