UFISADI: The Making Of IPTL

Happy ya mwaka mpya wa new year. Ila hawa tunao mpaka kieleweke tuu, robot hongera kwa kutupatia muziki huu laini kipindi hiki cha kuufunga mwaka.
 
Bado tunahitaji kibao kinachuhusu BOT, kiko kwenye chati sana sasa hivi Bongo. Tunakiomba tukisikilize wakati tukisherekea Mwaka Mpya.
 
Invisible

geuza hiyo santuri mazee...............maana hii "once more" imeshakinai, au ndio inabidi tuchonge sindano?!!............au yule DJ wa kuchochea hayupo?.........usitukoseshe step mzee
 
Wakati Masakata ya ufisadi BoT na Richmond yakiendelea, tujikumbushe la IPTL

Joseph Mihangwa Machi 5, 2008
Raia Mwema

WATANZANIA wengi bado wanalikumbuka sakata la ugomvi kati ya kampuni ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) na TANESCO kati ya mwaka 1999 na 2001 kuhusu gharama za ujenzi wa mtambo wa umeme wa Tegeta na bei ya umeme baada ya TANESCO kugundua udanganyifu mkubwa katika mkataba wao.

Katika tafrani hiyo, IPTL iliifikisha TANESCO kwenye mahakama ya kimataifa ya usuluhishi ikidai mkataba uheshimiwe na ilipwe dola milioni 4.6 au Shilingi bilioni 4.6 kwa mwezi kwa kutumia huduma za IPTL chini ya mkataba wa miaka 20.

IPTL ilishinda kesi katika mazingira ya kutatanisha pamoja na mahakama hiyo kukiri kwamba gharama za mkataba wa IPTL ziliongezwa kinyemela kwa dola milioni 24. TANESCO inatakiwa kulipia huduma hizo iwe imezitumia au haikuzitumia. Hili tutalifafanua baadae.

Licha ya TANESCO na baadhi ya watendaji wakuu wa serikali kudai mahakamani kwamba IPTL ilighushi hati, na kwamba kulikuwa na mazingira ya rushwa katika mkataba huo, mahakama hiyo iliendelea kuagiza kuwa mkataba uheshimiwe. Hiyo maana yake ni kwamba kwa miaka 20 mfululizo watumiaji wa umeme na walipa kodi watabeba mzigo wa kulipa Shilingi bilioni 4.6 kwa umeme wasiouhitaji wala kuwa na uwezo wa kuugharamia.

Haya ni matokeo ya hujuma ya wajanja wachache waliohusika na mkataba huo.

Katika makala hii, kwa kutumia vyanzo vyetu mbalimbali, tutaelezea kwa kifupi chimbuko la sakata hili na athari lililoleta kwa uchumi wa nchi na kwa walipa kodi wa Tanzania kwa ujumla. Sakata hili lilianzaje na ilikuwaje?

Ni hivi: Ukame mkubwa uliotikisa mwaka 1994 ulisababisha kukauka kwa Bwawa la Mtera ambalo ndicho chanzo kikubwa cha umeme unaotumika nchini. Kwa sababu ya ukame huo, mgawo wa umeme ukaikumba nchi na uzalishaji viwandani ukashuka. Waliokuwa na uwezo walinunua jenereta ndogondogo za umeme kwa matumizi ya nyumbani ambapo akina mie walirejea kwenye enzi za ujima za kutumia vibatari.

Zilikuwa enzi za giza nene, enzi za dhiki na wajanja wakaamua kutumia hali hiyo kujinufaisha. Kwa vipi?

Serikali ilifikia uamuzi wa haraka wa kupata umeme wa dharura. Hapo ndipo baadhi ya wafanyabiashara nchini wakaja na mawazo ya ufumbuzi wa tatizo hili. Mmoja wa hao alikuwa Reginald John Nolan, mfanyabiashara wa Kiingereza (Irish) aliyependekeza serikali inunue mtambo wa umeme (turbine) wa megawati 109 kutoka kampuni ya General Electric, na umeme uliotarajiwa kuzalishwa ungemgharimu mtumiaji mara nne zaidi ya umeme unaozalishwa na jenereta zenye kutumia mafuta ya dizeli.

Bila kujali yote hayo, mpango wa Nolan uliendelea vizuri huku ukiungwa mkono na kupewa nguvu na wanasiasa na watendaji wa ngazi za juu nchini. Karibu na mwisho wa maelewano (deal ) mwakilishi wa Benki ya Dunia nchini, Bwana Notoo Konishi alishtushwa na gharama za mradi huo na kumwandikia Katibu Mkuu, Wizara ya Maji, Nishati na Madini, kumtahadharisha juu ya pendekezo la Nolan; akionya kwamba kama serikali ingekubali pendekezo hilo tete, Benki ya Dunia ingejitoa kuhudumia sekta ya nishati nchini na wafadhili wengine wangejiengua pia.

Kwa huruma na nia njema, na kwa lengo la kuiepusha Tanzania na mpango hatari wa Nolan, Benki ya Dunia ilijitolea kununua mitambo miwili ya megawati 75 kama msaada ili kuongeza uwezo wa TANESCO na kupunguza tatizo la umeme nchini.

Ikumbukwe pia kwamba mwezi mmoja kabla ya mazungumzo kati ya Nolan na serikali kuanza, kampuni nyingine ya Malaysia ya Mechmar, ilifikia makubaliano na Wizara ya Nishati na Madini ya kutengeneza umeme chini ya mpango wa Independent Power Project (IPP) kama njia ya kuendeleza uhusiano wa nchi masikini za Dunia ya Tatu na kufanya Mechmar kuwa kampuni kubwa ya kwanza kuwekeza katika sekta ya umeme nchini. Na kwa mara nyingine mpango wa Nolan ulizidiwa kete na Mechmar, licha ya kupigiwa debe na watendji serikalini na waunganishi wa "michuzi" wa kimataifa

Inasemekana, Waziri wa Mipango wa wakati huo, Horace Kolimba (hayati), pengine kwa nia njema kabisa, ndiye aliyefanya uwekezaji wa kampuni ya Mechmar ukubalike nchini. Inasemekana Kolimba alitembelea Malaysia, Julai, 1994 na kueleza tatizo la mgawo wa umeme nchini Tanzania na azma ya serikali ya kulimaliza haraka. Serikali ya Malaysia ilimkutanisha na wawekezaji wa nchi hiyo na baadaye akawaalika kutembelea Tanzania ili kutathmini hali.

Kwa kufanya hivyo, Kolimba hakujua kwamba alikuwa akikaribisha mwekezaji mumiani nchini.

Datuk Baharudan wa kampuni ya Mechmar alifanya mazungumzo na Waziri wa Maji Nishati na Madini pamoja na Meneja Mkuu wa TANESCO, Naibu Kamishna wa Nishati na Msaidizi wa Rais wa mambo ya uchumi ambao wote walithibitisha kwamba TANESCO na serikali ziliukaribisha "ukombozi" huo kutoka Mechmar.

Mwezi mmoja baadaye mkataba wa "kifo" ulitiwa sahihi na IPTL ikaanzishwa. Ni nani huyu IPTL? Alifikaje Tanzania? Alisaidiwa na nani kuliteka soko la umeme nchini?

IPTL ni ushirika wa kibiashara nchini kati ya Shirika la Mechmar (Malaysia) linalomiliki asilimia 70 ya hisa na kampuni iitwayo VIPEN Ltd ya mjini Dar es salaam inayomiliki asilimia 30 ya hisa. VIPEN ilianzishwa na Bakari Somji (hayati). VIPEN ni mashuhuri kwa kuunganisha mipango ya kibiashara nchini kati ya makampuni ya kimataifa na serikali ya Tanzania na kupata misaada kutoka nje.

Aidha mmoja wa watu viunganishi waliotumwa na VIPEN kwa kasi hiyo ni Mtanzania mmoja ambaye ni mmoja wa wakurugenzi wa VIPEN na IPTL. Huyo alipewa jukumu hilo kwa sababu ya kufahamiana vizuri na wakubwa wa Benki Kuu (BOT). Wakati mwingine kiunganishi huyu huambatana na msafara wa Rais katika ziara mbalimbali nje ya nchi kama mwakilishi wa sekta binafsi nchini. Kwa jinsi hii alikuwa katika nafasi nzuri kupitisha "sumu" ya IPTL kwa urahisi serikalini.

Nini kilichokubaliwa chini ya mkataba kati ya IPTL na TANESCO? Kilitekelezwa kama ilivyokusudiwa?

Wakati serikali ikiidhinisha mkataba wa miaka 20 wa kuuziana umeme (power purchase agreement) kati ya IPTL na TANESCO, mwaka 1995, ilibainisha kwamba IPTL wangejenga mtambo wenye kutumia mafuta ya dizeli wa megawti 100; yaani slow speed diesel power plant (SSD) pale Tegeta, jijini Dar es salaam, kwa gharama ya dola 163.5 na kwamba gharama za ujenzi zilikadiriwa kufikia dola milioni 126.39.

Ilikubaliwa pia kwamba ushuru kwa matumizi ya umeme huo ungetegemea gharama halisi za ujenzi

Lakini badala yake, na bila ya kukubaliana wala taarifa kwa TANESCO, IPTL, kwa makubaliano na kampuni Martsila, iliamua kujenga kwa bei hiyo ya dola milioni 163.5 mtambo wa dizeli (MSD) ambapo bei yake halisi ilikuwa dola milioni 85.7. Mtambo wa MSD unataka gharama kubwa kuhudumia na una maisha mafupi.

Kufuatia uamuzi huo wa upande mmoja, bei ya mtambo huo hafifu ilipanda kinyemela kwa asilimia 33 kutoka dola milioni 85.7 hadi dola milioni 111.2 pamoja na kwamba ulikuwa hafifu kwa sifa.

Mnamo Septemba 1997, tatizo la umeme nchini lilirejea tena. Hata hivyo, safari hii sio kwa sababu ya ukosefu wa mvua bali ilitokana na TANESCO kukosa fedha za kulipia ushuru wa mafuta ya kuendeshea kutoka nje.

Kilichoshangaza ni kwamba wakati Hazina ilikataa kuiondolea TANESCO ushuru wa mafuta wakati huo huo iliendelea kutoa msamaha wa kodi kwa wafanyabiashara wa mafuta ya kula walioagiza kutoka nje. Kwa wengi, hiki kiliashiria rushwa kwa viongozi wa serikali ili kuibeza na kuikwaza TANESCO isiweze kupata nafasi ya kujiimarisha na kuipa nafasi IPTL kusimika makucha yake katika sekta ya umeme.

Hii ilikuwa wazi kwa sababu hofu ya IPTL ilikuwa dhahiri kufuatia kusimikwa kwa mitambo ya megawati 73 pale Ubungo (Oktoba 1995) na mwingine wa megawati 180 (uliofadhiliwa) uliotarajiwa kukamilika kule Kihansi. Mitambo hiyo miwili ingetosheleza mahitaji ya watumiaji; na hivyo kutishia hali ya kuendelea na mradi wa IPTL.

Kama tulivyoona mwanzo kwamba Benki ya Dunia haikupendelea mradi wa IPTL. Uligubikwa na mizengwe tangu mwanzo kwa hiyo benki hiyo iliendelea kuiwekea ngumu IPTL; huku baadhi ya vigogo nchini wakiendelea kuupigia debe mradi huo kwa nguvu zote.

Oktoba 1997, Benki hiyo iliishinikiza serikali ya Tanzania kutia saini mradi wa gesi wa Songas uliofadhiliwa na serikali ya Canada baada ya kuona serikali inataka kuutelekeza na kuukumbatia mradi wa IPTL. Lengo la mradi huu lilikuwa kuipatia Tanzania umeme rahisi.

Ingawa ulibuniwa kabla ya ule wa IPTL na serikali ya Canada kulipia dola milioni 200, serikali ilijifanya kuufumbia macho huku ikiendelea kuijengea jina IPTL na kutoa msamaha wa kodi na upendeleo mwingine. Kama isingekuwa hila za IPTL kwa kushirikiana na baadhi ya vigogo nchini, Tanzania ingekuwa imeanza kuvuta umeme wa gesi tangu mwaka 1997.

Ujanja wa IPTL ulijidhihirisha zaidi Desemba 1997 pale ambapo, kupitia taarifa yake yenyewe, ilidanganya kwamba kitendo cha kubadili aina ya mtambo wa SSD uliokusudiwa kujengwa Tegeta na kujenga mtambo duni na rahisi wa aina ya MSD, kwa gharama zile zile, eti kilifahamika mapema na kuidhinishwa na TANESCO yenyewe.

Taarifa hiyo ilipingwa vikali na Mkurugenzi Mtendji wa TANESCO, Baruany Luhanga kwamba ni ulaghai wa hali ya juu wa IPTL.

Kwa upande wake, IPTL ilidai kwamba mtambo wa awali katika mkataba (PPA) aina ya SSD haukukusudiwa bali uliokusudiwa ni aina ya MSD na kwamba hili lilikuwa kosa la uchapishaji. IPTL waliendelea kusisitiza uhalali wa gharama za ujenzi kwa dola milioni 163 na kukataa kwa jeuri kutoa ushahidi wa hati za awali kwa madai kwamba tenda hiyo ilikuwa ya wazi na kwamba hati hizo zilikwishapotea.

Ni kutokana na ubabaishaji huu wa IPTL kwamba Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Maji na Madini, Patrick Rutabanzibwa alilazimika kumshauri Rais afute "biashara" hii na IPTL na kwa bahati nzuri aliuona ukweli huu ingawa hakuweza kuufuta mradi huo, na badala yake alionya juu ya "mchezo mbaya" wa IPTL kwa Watanzania.

Hapo, Katibu Mkuu huyo alifanikiwa kumshawishi Rais aagize mkataba huo ushughulikiwe kwa njia ya usuluhishi na kituo cha kimataifa cha usuluhishi wa migogoro ya uwekezaji (International Centre for the Settlement of Investment Disputes for Arbitration)- ICSID, mjini London, Novemba 1998.

Wakati wa kusikilizwa kwa mgogoro huo, kitu cha kushangaza ni kwamba yule muunganishi wa dili zote kati ya IPTL na vigogo serikalini alikiri waziwazi (Mei 8, 2000) kwamba baada ya mvua kubwa za El-Nino kunyesha mwaka 1997, hapakuwa na haja tena ya mradi wa IPTL. Mahakama ilibaini kuwa mradi rahisi wa mtambo wa MSD uliongezwa bei kinyemela kwa dola milioni 24; lakini ikaamua mkataba uendelee kwa sababu mabadiliko kutoka mtambo wa SSD yalifanyika mapema kwa vigogo serikalini na TANESCO kuridhia.

Kufikia hapo, kuna maswali mengi ya kujiuliza juu ya uhalali wa mradi huu wa IPTL. Maswali kama je; licha ya Benki ya Dunia kuonya juu ya athari za mradi huu kwa uchumi wa taifa, kwa nini viongozi serikalini waliruhusu uendelee?

Ukweli mwingine uliojidhihirisha ni kwamba chini ya mkataba wa awali ,IPTL ilitakiwa kujenga nyumba 37 kwa dola milioni 7.6 lakini zilipunguzwa hadi 10 na gharama za ujenzi huo (dola milioni 7.6) zikaongezwa kwa zaidi ya asilimia 130. Hata hivyo, nyumba zilizojengwa ni sita tu!

Akitoa ushahidi kwenye ICSID, mmoja wa wanasheria wa TANESCO alibainisha wazi kwamba haikuhitajika mtaalamu wa majengo kutambua kwamba nyumba sita za ghorofa moja zisingeweza kugharimu dola milioni 7.6 sawa na Shilingi bilioni 7.6.

Ushahidi uliopo unabainisha pia kwamba kampuni ya Nartsila iliuza mtambo wa umeme kama huo (MSD) kwa nchi zingine za Kiafrika kwa dola milioni 60 tu. Kwa hiyo, kwa kuongeza gharama mara mbili, IPTL na Nartsila (kwa njama za pamoja) walijihakikishia faida kubwa kuweza kurejesha fedha zao kabla hata mradi huo haujaanza kufanya kazi.

Kwa kuwa serikali ilifahamu fika juu ya uwezekano wa kutumia vyanzo mbadala kuweza kujitosheleza kwa umeme, kwa nini ilighairi kuvitumia vyanzo hivyo na badala yake ikaendelea kuupigia debe mradi wa IPTL?

Tumeona kwamba ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Maji na Madini pamoja na Mkurugenzi Mtendji wa TANESCO, Baruany Luhanga ndio pekee waliojitoa mhanga kuzungumza kwa uwazi na ukweli juu ya "mchezo mchafu" wa IPTL hapa nchini. Je vigogo wengine walilionaje hilo na walichukua hatua gani?

Tumejifunza nini kwa sakata hili? Tuyaangalie kwa ufupi tu maoni ya baadhi ya viongozi kuhusu sakata hili.

Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa serikali iliupitia mkataba wa IPTL na TANESCO kwa niaba ya serikali na kuona ulikuwa "unakubalika kabisa kabisa".

Hata hivyo, kinyume chake washauri wa TANESCO (Canada and Hunton and Williams walitoa taarifa ya uwazi na ukweli kwamba mradi wa IPTL ulikuwa haufai, ulikuwa mradi wa kipindi kirefu wakati tatizo uliolenga kutatua lilikuwa la kipindi kifupi, ulikuwa wa gharama kubwa bila sababu na tatu ulizidi mahitaji halisi ya umeme nchini kwa hiyo watumiaji na walipa kodi wangevikwa gharama za kuzalisha umeme wasiouhitaji. Aidha, gharama zake ziliongezeka na kuwa kubwa kupindukia ili kuinufaisha IPTL.

Vilevile washauri hawa walibainisha kwamba mkataba uliwapendelea mno IPTL na kuifunga nchi shingoni kulipia huduma zisizohitajika. Aidha mkataba haukuweka ukomo wa muda wa kukamilisha ujenzi na kwamba gharama zilizopaswa kulipwa na TANESCO zingelijadiliwa baada ya mradi kukamilika. Aidha kutokuwapo muda wa kukamilisha mradi ilikuwa ni kuiumiza TANESCO kutokana na kupanda kwa gharama.

Hatuwezi kusema kwamba ziara ya Waziri wa Nishati na Madini nchini Malaysia, Februari 1997, haikuwa ya manufaa kwa nchi; lakini tunashangazwa sana na tamko lake baada ya kurejea kutoka ziara hiyo kwamba haikuwa vibaya wala ukinzani (contradiction ) kwa miradi ya IPTL na Songas kuendeshwa kwa pamoja wakati akifahamu fika kwamba kuendesha miradi yote ingeathiri uchumi duni wa nchi.

Jumuiya ya kimataifa kwa upande wake ilishindwa kuvumilia sakata hili. Katika kikao cha ushauri kati ya Tanzania na mashirika ya wafadhili ya kimataifa, Desemba 1997 na Mei 2000, mjini Dar es salaam, mara mbili mjumbe wa Umoja wa Ulaya (EU), Peter Christiansen alitoa hisia zake kwa kusema "Umoja wa Ulaya unasikitishwa na hali ya serikali ya Tanzania kukaa kimya kwa vitendo vya viongozi wake wa ngazi za juu wa chama na serikali kuhusishwa na (mchezo mchafu) sakata la IPTL.

Naye mwandishi wa shirikisho la Reuters, Mark Dodd Julai 1998 alisikitika kuondoka nchini bila mahojiano na Rais Mkapa amuulize mantiki ya uhalali wa mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na Waziri wa Madini na Nishati kutia sahihi mkataba wa IPTL ambao IMF tayari iliueleza kuwa "ni mzigo usiotakiwa kwa uchumi wa taifa na kwa walipa kodi wa nchi hii."
 
Ni Lini Huyu Bwm Atakamatwa Ili Ahojiwe Juu Ya Haya Machafu Aliyoyafanya Alipokuwa Rais Wa Tanzania? Hivi Huyu Mtu Tulimkosea Nini Watanzania Mpaka Akaamua Kututenda Hivi? Mbona Nyerere Alituhakikishia Kuwa Ni Mr Clean? Ugumu Anaouona Jk Sasa Hivi Kuongoza Hii Serikali Ya Sasa Unatokana Machafu Yaliyokithiri Aliyoyakuta Humo. Lakini Kila Chenye Mwanzo Ni Lazima Kitakuwa Na Mwisho. Sisi Acha Tuendelee Kupiga Tu Kelele Ipo Siku Mungu Atatusikia
 
IPTL sends 26 workers packing

2008-03-06 09:58:25
By Correspondent Gadiosa Lamtey

Independent Power Tanzania Limited (IPTL) has terminated the services of 26 of its 70 workers with immediate effect, The Guardian has authoritatively learnt.

The management of the Dar es Salaam-based private company has blamed the matter on what it has described as long-running failure by the government to pay for the electricity the firm has been generating.

It has further defended the off-loading of the workers as part of a strategy to keep afloat by cutting production and running costs following the government�s failure to settle an entire year�s power bill.

The government contracted IPTL, a joint venture between Malaysia�s Mechmar Corporation and Tanzania�s VIP Engineering and Marketing Ltd, to generate emergency power in 1996.

The firm was required to construct a 100-Megawatt power plant as an independent power producer for 20 years under a contract stipulating that the government would pay a monthly 3bn/- in capacity charges.

The termination letters the workers were served with yesterday at the firm`s premises at Tegeta in suburban Dar es Salaam are signed by IPTL plant manager Jaakko Kaihua.

However, the retrenched workers told this paper shortly after they were presented with the letters that the ``cost-cutting strategy`` given by the management as the reason for their laying off was an excuse too lame to convince anyone.

They said in separate interviews that they believed they were victims of the recent announcement by the government instructing all private employers to raise the minimum wage.

Last year the government announced new private sector minimum wages, the lowest being 65,000/- for housemaids and the highest 350,000/- for the mining sector.

Another reason, they said, was a long-standing dispute pitting them against the management over a voluntary contract agreed upon by the two parties and was lined up for conclusion and signing in the middle of this month.

Under the agreement, the company would have raised the minimum wage from 165,000/- to 350,000/-. That would have included transport allowance, leave passage, and a package of other allowances to help the workers attend to various social needs.

The management presented each of the retrenchees with between 400,000/- and 600,000/- and a three-month medical insurance cover, which most of those affected said was too little and did not reflect the value of the service they had rendered to the company.

A trade union leader at the company, Mwinyi Uweje, said it was unfair for the management to pay the retrenches ``such a paltry sum`` after they had served the firm for up to seven years. However, he would not say whether there would be any further action to ensure that justice was done.

Contacted for clarification on retrenchees` claims and complaints, Kaihua and IPTL human resources manager Hilda Makoye, chose to remain tight-lipped.

Energy and Minerals Minister William Ngeleja was not reachable by phone to comment on the IPTL management`s charges that the government had defaulted on the payment of the capacity charges for a year.

The government`s power generation contract with IPTL and several similar ones with other private companies are at the centre of controversy that has raised a nationwide outcry.

This is partly over the requirement that the government pay the firms hefty amounts of money even when they actually do not generate any power.

SOURCE: Guardian
 
When are we going to terminate the damn contract? I don't know what is wrong with in our government.

I cant believe it.
 
IPTL sends 26 workers packing

2008-03-06 09:58:25
By Correspondent Gadiosa Lamtey



The management of the Dar es Salaam-based private company has blamed the matter on what it has described as long-running failure by the government to pay for the electricity the firm has been generating.

The Government should stick to its guns!
Why pay for a null and void contract?
 
Huyu Rugemalira na wajanja wanzie wa Ki-Malaysia wanatufanya watanzania wote mabwege kweli
 
When are we going to terminate the damn contract? I don't know what is wrong with in our government.

I cant believe it.

Someone said that the contract cannot be terminated, for there are some serious consequences!
Let's die for good!
 
Govt angered by IPTL staff retrenchment

2008-03-08 09:45:41
By Gadiosa Lamtey


The government has angrily accused the Independent Power Tanzania Limited (IPTL) of violating its directive for employers not to sack employees on the ground that they cannot pay the recently announced minimum wages.

Labour, Employment and Youth deputy minister Hezekiah Chibulunje told The Guardian on Thursday in Dar es Salaam that the government had ordered employers not to terminate workers until a study to determine optimum minimum wages had completed its job.

``IPTL has violated a government directive, and this is a breach of the law because the order was made for the benefit of the people,`` he said.

Chibulunje said that private sector wages will remain as published in Government Notice no 223 of 2007.

Last year the government announced new private sector minimum wages, the lowest being 65,000/- for housemaids and the highest being 350,000/- for the mining sector.

He advised the 26 sacked IPTL workers to make a follow-up on their benefits from the employer.

IPTL terminated the services of 26 of its 70 workers on Wednesday as the management of the Dar es Salaam-based private company blamed the matter on what it described as long-running failure by the government to pay for the electricity the firm has been generating.

It has further defended the off-loading of the workers as part of a strategy to keep the company`s operations afloat by cutting production and running costs following the government`s failure to settle an entire year`s power bill.

The government contracted IPTL, a joint venture between Malaysia`s Mechmar Corporation and Tanzania`s VIP Engineering and Marketing Ltd, to generate emergency power in 1996.

The firm was required to construct a 100-megawatt power plant as an independent power producer for 20 years under a contract stipulating that the government would pay a monthly 3bn/- in capacity charges.

The termination letters the workers were served with at the firm`s premises at Tegeta, on the city`s outskirts, were signed by IPTL plant manager Jaakko Kaihua.

However, the retrenched workers told this paper shortly after they were presented with the letters that the cost-cutting explanation given by the management as the reason for their being laid off was simply an excuse.

They said in separate interviews that they believed they were the victims of the recent announcement by the government instructing all private employers to raise the minimum wage.

Another reason, they said, was a long-standing dispute pitting them against the management over a voluntary contract agreed upon by the two parties and was lined up for conclusion and signing in the middle of this month.

Under the agreement, the company would have raised the minimum wage from 165,000/- to 350,000/-. That would have included transport allowance, leave passage, and a package of other allowances.

The management gave the retrenchees between 400,000/- and 600,000/- and a three-month medical insurance cover, which most of those affected said was too little and did not reflect the value of the service they had rendered to the company.

A trade union leader at the company, Mwinyi Uweje, said it was unfair for the management to pay the retrenches such a `paltry` sum after they had served the firm for up to seven years.

However, he would not say whether there would be any further action to ensure that justice was done.

SOURCE: Guardian
 
Upuuzi tu! Walitegemea nini? Ndiyo maana kwa wenzetu mishahara inapangwa baada ya majadiliano ya waajiri na waajiriwa. Serikali haina nafasi humo. Hawa ndiyo wanaokubaliana ni mshahara upi ambao hautawaathiri pande zote mbili. Katika soko huria hauwezi kumzuia mwajiri kupunguza wafanyakazi wakati gharama za uendeshaji zimeongezeka. Kitanda tulitandika wenyewe, sasa twaogopa nini kukilalia?
 
kaaz kweli kweli.... Unajua kwenye "Mass workers" ndio mambo kama haya yanaonekana (tukumbuke Arusha kule kwenye Sunflag??, Urafiki etc na hili la IPTL)......

Kwanza wajue kuwa tayari tunavyoongea kuna mamjamaa wameshawatimua wale mabinti wa ndani "Hauzigeli" na "Mahauziboi" ambao walikuwa na kimbelembele cha kudai mshahara mpya (65,000 mwanangu, si utani).... Swala ni kwamba sijaona popote ambapo Serikali iliweka "Fall back option" kwa watu kama hawa ambao wali/wame potza ajira kutokana na sakata zima la mishahara mipya....

Kingine cha muhimu kwenye hili ni lile lile la mikataba "feki" na isiyoangalia maslahi ya wananchi.... Tunasema tunaita/karibisha wawekezaji ili kuja kuwekeza kuinua uchumi.... Sasa kama humuangalii mwananchi wako, ni uchumi upo unategemea kuuinua????

Kwa kweli sijui tuendako manake tutokapo twapajua lakini huko mbele sijui ni wapi tuendako...... Eee Mola tusaidie Wazalendo wa Tanzania....
 
Mwanakijiji Waaache Anakula Matapishiyake Mwenyewe::::::
Aulize Mwenzake Aliesaini Mikataba ,,mi Nashauri Iapigwe
Semina Kamilifu Ya Hawa Mawaziri Juuu Ya Kusaini Mikataba Na Nini Kinachotakiwa Kuangalia Kabla Ya Kusaini Else Hata Waliopo
Wataendelea Kula Matapishi Ya Waliopita Kama Hawatakuwa Makini Nini Kinachotakiwa Kwenye Mkataba
 
Ufisadi ukishangaa la Richmond la IPTL je?

Joseph Mihangwa Machi 12, 2008
Raia Mwema

Katika sehemu kwanza ya makala yetu katika gazeti hili toleo namba 16 la Februari 27-5 Machi 2008, tulieleza jinsi mkataba mbovu wa miaka 20 wa kuuziana umeme kati ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na kampuni ya kimataifa ya kuzalisha umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) ulivyofikiwa kwa hasara ya taifa

Tulieleza kwamba wakati mkataba huo ukipigiwa upatu kwa nguvu zote na baadhi ya vigogo serikalini, tayari Benki ya Dunia ilikuwa imejitolea kusaidia kununua mitambo miwili ya megawati 75 kila mmoja ili kuokoa hali ya umeme nchini na kufanya mkataba wa TANESCO /IPTL usihitajike.

Lakini vigogo wa serikali waliziba masikio na kuendelea na IPTL. Wakati huo TANESCO ilikuwa ikiwadai wateja wake deni la dola 55m pamoja na serikali ya Zanzibar.

Isitoshe kabla ya mradi wa IPTL, Benki hiyo ilijitolea kufadhili kupitia serikali ya Canada mradi wa gesi wa SONGAS ambao ulikuwa nafuu zaidi na tayari Canada ilikuwa imelipa dola milioni 200 za Marekani lakini bado serikali ilifumba macho na kuendelea na IPTL.

Tuliona pia jinsi gharama za ujenzi zilizokadiriwa kufikia dola za Marekani milioni 126.39 zilivyoongezwa kinyemela kwa zaidi ya asilimia 33, na jinsi mitambo iliyokusudiwa (SSD) yenye thamani ya dola milioni 163.5 iliyobadilishwa na kusimikwa mitambo hafifu (MSD) kwa bei hiyo hiyo ambapo bei halisi ilitakiwa kuwa dola miloni 85.7 ingawa mtambo kama huo (aina ya wartsila ) uliuzwa kwa dola million 60 kwa nchi nyingine za kiafrika ikiwamo Kenya.

Haifahamiki kwa nini mradi wa IPTL ulitetewa kwa nguvu zote na vigogo katika kipindi ambacho tatizo la umeme lilikuwa la muda mfupi tu na hata baada ya kumalizika ikiwa ni pamoja ka ukweli kwamba tayari kulikuwa na mradi rahisi mbadala kama vile mradi wa SONGAS na kusimikwa kwa mitambo wa megawati 75 Ubungo, Dar es Salaam (1995) na ule wa kihansi wa megawati 180.

Inadhaniwa kuwa kama isingekuwa hila za viongozi dhidi ya mradi wa Songas na kuipendelea IPTL Tanzania ingeanza kutumia umeme wa gesi tangu mwaka 1997.

Mradi wa IPTL ambao ulionekana dhahiri kugubikwa na ufisadi kwa ngazi na kwa kiwango chote, uliendelea licha ya serikali kutahadharishwa na washauri wa TANESCO, Kampuni ya Acrea (Canada) na Kampuni ya Bunton and Williams (U.K) kwamba ulikuwa haufai ulikuwa wa kipindi kirefu (miaka 20) kwa tatizo la muda mfupi gharama kubwa (asilimia 130 zaidi ya gharama za kawaida bila sababu ulizidi mahitaji ya umeme hivyo kwa lengo la kuinufaisha IPTL.

Jumuiya ya kimataifa yenye mapenzi sana kwa Tanzania pamoja na kutahadharisha kushauri na kusikitika kuhoji uhalali na mantiki juu ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na Waziri wa Madini na Nishati kutia saini mkataba huo (badala ya watendaji wanaostahili) licha ya mradi huo kuelezwa na Shirika la Fedha la Kimataifa (IFM) na Benki ya Dunia (WB) kuwa ni"mzigo usio wa lazima kwa uchumi wa taifa na kwa walipa kodi wa nchi hii."

Ofisi ya Mwanaheria Mkuu, ndiyo iyoupitia mkataba wa IPTL/TANESCO sambamba na ushauri wa Acrea na Bundon Williams ambapo mmoja wa wanasheria wa Serikali (Mary Mdosi) aliandika maoni yake kwa ufupi "ushauri wao (Acress/Bundon) uchukuliwe tu kama sehemu ya usshauri wetu juu ya mkataba huu kwa kiwango ambacho hakipingani na kilichoandikwa humu."

Ofisi ya Mwanasheria Mkuu, Waziri wa Nishati na Madini (William Shija na baadaye Dk Abdallah Kigoda (Feb 1977) na Edgar Maokola Majogo (2000) na Waziri wa Fedha (Daniel Yona) walisimama kidete kuhakikisha mkataba wa IPTL unapita na ilipendekezwa wakati mmoja kwamba Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Patrick Rutanzibwa ambaye aliapa kutokukubaliana na IPTL na kumjulisha Rais Benjamini Mkapa "uchafu"ndani ya mkataba huo afukuzwe kazi.

Nayo Taasisi ya Kuzuia Rushwa (PCB wakati) huo ilifuatilia kwa karibu mwenendo wa sakata hili na ilifikia mahali Mkurugenzi wa Oporesheni wa taasisi hiyo, Edward Hosea achukue hatua za kuwakamata baadhi ya wahusika lakini inasemekana alirudishwa nyuma kufanya hivyo na nguvu zilizokuwa juu yake.

Kuna wakati pia Rais Benjamini Mkapa alipoingia madarakani alitamka kuwa asingependa kuona mkataba huo wenye kuwaumiza wananchi na taifa kwa ujumla lakini haifahamiki kwa nini aliunyamazia ukaendelea.

Inasemekana baada ya kubaini kwamba serikali ilikuwa imejinyonga kwa mkataba huo, aliamua kunyamaza na nyundo ya mwisho iliyomnyamazisha ilikuwa 1998 alipolalamikiwa na Waziri Mkuu wa Malaysia, Mohamed Mahathir juu ya yeye kutaka kuingilia mkataba huo walipokutana kwenye kikao cha wakuu wa nchi na Jumuiya ya Madola mjini Edinburgh kwa misingi kwamba Malaysia na Tanzania zilikuwa nchi mbili zilizounganishwa na kushabihiana ndani ya ushirikiano wa nchi za dunia ya tatu (south-south Commission) ambapo Mahadhir alitia msukumo mkubwa kwa wawekezaji wa kimalaysia kuwekeza barani Afrika.

Kuna taarifa pia kuwa nchi hiyo ilifadhili kwa kiwango kikubwa kampeni za chama cha African National Congress (ANC) cha Afrika kusini katika uchaguzi wa 1994.

Huku ikionekana dhahiri kwamba mkataba huo ulijaa mizengwe kwa hasara ya taifa huku jumuiya ya kimataifa ikitishia kusitisha misaada kwa Tanzania, Rais Mkapa alibaki njia panda, kisha akaelekeza mgogoro huo uwasilishwe kwenye Baraza la Usuluhishi wa Migogoro ya Uwekezaji (ICSID) mjini London hasa baada ya Katibu Mkuu, Rutabanzibwa kushikilia kwamba mkataba huo ufutwe (the African, Novemba 27, 1998).

Ni katika baraza hilo baadhi ya mambo yenye kuashiria ufisadi ndani ya mkataba wa IPTL yalipobainika kama vile kwamba baada ya mvua za El-nino, Desemba 1997 hapakuwa na sababu tena za mkataba wa miaka 20 na IPTL. Maelezo haya ni kwa mujibu wa shahidi James Rugemelila wa VIPEN/IPTL ya Mei 8, 2000.

Ilidhihirika pia kuwa nyumba 37 zilizopangwa kujengwa zilipunguzwa kufikia 10, lakini zilizojengwa ni sita kwa gharama zilezile za mkataba ambazo nazo hata hivyo ziliongezwa kwa asilimia 130 (ICSID 2000-uk 41).

Vivyo hivyo ilielezwa kuwa mitambo iliyokusudiwa haikuwekwa badala yake ililetwa mitambo hafifu kwa bei kubwa zaidi (ICSID 200 uk 41-2).

Maelezo kwa njia ya kiapo ya mmoja wa watendaji wakuu wa wizara (Aprili 19, 2000, uk 3) yanaonyesha kuwa alipelekewa dola milioni 200,000 kuunga mkono mpango wa IPTL akazikataa lakini siku ya krismasi, 1994 alikuta nyumbani bahasha yenye 5000,000/- lakini akamrudishia mletaji.

Mwingine naye alieleza kuwa aliahidiwa kupitia mmoja wa watumishi wa ofisi ya mwanasheria mkuu kwamba kama angewasaidia kusukuma mkataba wa IPTL ukapita ungelipwa Sh milioni 100.

Mwingine aliieleza PCB kwamba aliahidiwa dola 20,000 (Tshs 20m/= akazikataa lakini alikiri kuwa baadaye alikubali na kupokea Sh 100,000/= tu kama "chai" ambayo gharama haiwezi kuchukuliwa kama rushwa.

Hawa walikuwa maofisa wa ngazi za chini tu. Vigogo walipata kiasi gani inahitajila uchunguzi wa kina kama ule wa Richmond.

Baraza lilikataa madai ya TANESCO kuhusu kuwapo kwa rushwa kutokana na ushahidi mdogo uliowasilishwa na ambao hata hivyo uliwasilishwa kwa kuchelewa.

Kulikuwa na taarifa kuonyesha kwamba PCB na Idara ya Upelelezi ya Makosa ya Jinai (OCD) zilikusanya ushahidi mwingi muhimu kuthibitisha vitendo vya rushwa lakini haukuwasilishwa baada ya serikali kukataa kwa hofu ya aibu ya "kuitwa taifa la wala rushwa" wala hapakuwa na ufuatiliaji tena.

Kwa sababu hii TANESCO ilishindwa kesi katika Baraza la Usuluhishi na Serikali ilitumia Sh milioni 7 katika kesi hiyo.

Wananchi na vyombo vya habari hazikukaa kimya juu ya ufisadi huu, lakini kwa sababu ya uhuru duni na kupuuzwa kwa vyombo hivyo hakuna lililofanyika kurekebisha hali.

Brigedia Jenerali (mstaafu), Joachim Buchard Ngonyani alinukuliwa akisema, IPTL ni kaburi la Watanzania tunataka wote walioidhinisha washughulikiwe" (the African, Agosti 3,1996). Hakusikilizwa.

Mbunge wa Dodoma mjini (wakati huo), Hashim Saggaf alishangaa kutohojiwa wote wanaohusika na mkataba huo waeleze kwa nini wametufikisha hapo (the East African Aprili 26, 1999), hakuna aliyemsikiliza.

Chini ya mkataba wa IPTL TANESCO itailipa IPTL dola 3.6m kama ada ya huduma ya mtambo (capacity charge) kama imezalisha au haijazalisha umeme na TANESCO imetumia umeme au haikutumia.

Juu ya ada hiyo TANESCO imetozwa dola tano za kimarekani kwa kila yuniti ya umeme kwa kuendesha mtambo nusu ya uwezo wake (inalipa dola milioni moja) kwa mwezi na kufanya malipo ya TANESCO kwa IPTL kuwa dola billion 4.5 kwa mwezi.

Gharama hizi za TANESCO ni mbali na zile za mradi wa umeme wa gesi wa SONGAS, Richmond (inayolipwa 12m kwa siku na ule wa Kiwira ambao kuanzia mwakani, TANESCO itatakiwa kuilipa kampuni ya utunzaji umeme ya Tanpower Resourses LTD inayodhaniwa kumilikiwa na Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamini Mkapa) Sh milioni 300 kwa siku na kufanya Tanzania kuwa na umeme ghali zaidi barani Afrika na kwa nchi zote za dunia ya tatu hali ambayo haiwezi kuvutia wawekezaji licha ya kuumiza wananchi.

Baada ya kufanikiwa kulindwa na kufumbiwa macho kwa ufisadi ndani ya mkataba wa IPTL mafisadi wameona mahali pa kuchuma bila jasho ni sekta ya umeme nchini.

Tumeyaona ya Richmond na mwakani yatafuatiwa na ya Tanpower Resources wakati IPTL wakiendelea kula. Ni kiasi gani hicho (kwa sana ) wanachoendelea kupora?

Hasara kutokana na mkataba wa IPTL kwa uchumi wetu ni kubwa mno. Kama tusingejiingiza katika mkataba huo wa kimagendo tungekuwa tayari tumeanza kutumia utajiri wetu wa umeme na kuokoa fedha za uagizwaji wa mafuta kwa ajili ya mitambo ya pale ubungo hasara kutokana na tatizo la umeme la 1997 lingeepukika kama mradi wa SONGAS ungetekelezwa badala ya kukimbilia IPTL.

Vivyo hivyo gharama kutokana na wawekezaji binafsi kwa kuleta jenereta za umeme wa dharura zingeepukika pamoja na shiringi billion saba zilizotumika kuhusiana na kasi ya TANESCO mjini London.

Tukishangaa la Richmond na la BOT (EPA) na hili la IPTL je? Uchumi wa nchi na maendeleo ya kijamii hawezi kupatikana kama tutaendelea kuongozwa na kikundi kidogo cha wasomi walafi, waliotekwa nyara na ubepari na mitaji ya kimataifa wenye ujasiri wa kifisadi, wasiotaka kukosolewa na kujirudi na kuwajibika kwa umma.

Ni kitu kimoja kwa wanasiasa na watendaji kunufaika kidogo kutokana na miradi ya uwekezaji inayorudisha ajira, bidhaa muhimu na kuchangia katika pato la serikali lakini ni kitu kingine tena kibaya na cha kiuaji kwa kikundi hicho kujishibisha kwa rushwa kutokana na miradi inayovunja sera kuu za kitaifa na kuwabebesha mzigo mkubwa wa ziada walaji walipa kodi wa nchi hii. Hawa ni wasaliti wa taifa.

Kwa kuendeleza uswahiba wa kuikumbatia IPTL na sasa Richmond, Tanzania imerudi nyuma miaka 30 ya Maendeleo wakati nchi nyingine zikikimbia na sisi tukitembea. Viongozi hawa wasio na soni wanataka kuacha majina gani? Wanataka makaburi yao kupondwa mawe na vizazi vijavyo?

Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango Malecela alitahadharisha Bunge hivi karibuni kwamba kiongozi bora na mwema ni yule anayesaka kutafuta jina zuri akiondoka.

Na vivyo hivyo mshairi Shaaban Robert ndivyo anavyosema katika shairi lake huru "jina" anaposema:

Mtu wa fikra njema, kwa watu huacha jina,
Na watu wajao nyuma, wakapenda kuliona,
Katika dunia nzima, likawa kubwa heshima
Na akili si kusema, lakini ni kufikiri,
Kwa kujua jambo jema, lisilokuwa na shari
Mvuka nguo chutama, endapo wajiadhari,
Na busara kutenda tendo, ambalo ni jema
Viumbe wakalipenda, ukapata na heshima
Maisha daima yenda, utaacha nini nyuma?

Basi tunasema ole kwa wasaliti hawa hali ni jambo la hatari, mwenye kiburi bila utulivu wa moyo; ndiye mchoyo kama kuzimu anayeshibishwa kama kifo. Ndiye hukusanya (vya watu) mataifa kwa maslahi yake mwenyewe.

Je hawatamdhihaki kwa nyimbo na kumsimanga wakisema; ole wake huyo anayejilimbikizia mali isiyo yake (ataachwa kupora vya masikini ) mpaka lini?
 
Back
Top Bottom