Ufanye nini brake zikifeli na uko katika mwendo kasi?

Ufanye nini brake zikifeli na uko katika mwendo kasi?

Utauwa watu kwa ushauri mbovu. Ukiweks neutral gari inakuwa nyepesi na mara ingine inaongeza mwendo.

Unachotakiwa kufanya ni kuondoa mguu kwenye accelerator na kama gari ni manual punguza mwendo kwa kubadili gear yaani toa namba tano weka nne then tatu,mbili, moja.

Kama ni auto zipo zenye mfumo P R N D 3,2,1 hapo toa D weka 3,2,1 kama ni zile za P R N D 2 L achia mafuta mwendo ukipungua weka 2 then L.
Fantastic Prondo,
Huyu jamaa angeua watu! Kuiweka gari ktk neutral state ikiwa katika mwendo mkali tena ktk mtelemko ni balaa jingine! Maelezo yako hapa ndiyo ya kuaminika na kutumika.
 
Mkuu ukiweza gari free kwenye mteremko Mkali Wakati haina break utakuwa umejitengenezea ajali ya makusudi kabisa, cha msingi Kama ni out wewe toa mkono wa gia kutoka alama D, na weka drive 2 Ingine utakuwa nzito ukiona bado inakuzidi peleka kwenye gia ya taratibu zaidi yenye alama low hapo utakuwa umepunguza Kiwango kikubwa cha mwendo na kitakacho fuatia wewe kufanya ni kutumia handbrake kwa kuvuta nusu jino mpaka gari itasimama
Mkuu sklful sijasema kwenye mteremko hii ina apply kwenye plain surface kumbuka remedy pekee ktk mwendo huo ni ku disengage na ndipo acceleration itashuka alternatively unaachia acceleration pedal...mteremkoni ni kesi nyingine mkuu...naona ukaamua unitusi kabisa
 
Sasa huku kudanganyana, kwa hiyo ukiwa unashuka mlima mkali utaweka neutral ili gari ipunguze mwendo!!???? Sijui hiyo gari yako aina gani?!!!?
Hii inategemea mazingira uliyopo na muundo wa gari hivyo hapa hakuna jibu sahihi
Sasa umedanganywa nn sasa?tunaongelea normal roads sijua una matatizo gani mpaka kuleta miteremko yako
 
Mimi nikiwa kwenye mwendokasi, sitakuwa na la kufanya zaidi ya kusubir dereva acontrol gari yke vzr. Na kwa sababu mabasi ya mwendokasi yana njia zake rasmi kama kutoka Kimara mpk kariakoo, ni rahisi kupunguza ajali. Cha muhimu ni abiria kusali ili kuombea maisha yenu, na kumuombea dereva afanikiwe kusimamisha gari.

Mkisema abiria wote muende pale kwa dereva hamtatosha.
Hehehehe dah aiseee
 
Mkuu sklful sijasema kwenye mteremko hii ina apply kwenye plain surface kumbuka remedy pekee ktk mwendo huo ni ku disengage na ndipo acceleration itashuka alternatively unaachia acceleration pedal...mteremkoni ni kesi nyingine mkuu...naona ukaamua unitusi kabisa
Pole Mkuu ila kwa sehemu yoyote hatakama ni tambarare kuweka Free hujaisaidia gari kupunguza mwendo mkuu gari unatakiwa iwe na gear wewe unatakiwa kuachia mafuta pekee gari itakuwa nzito hivyo itakupa msaada free ni hatari Katika matumizi ya Dreva samahani kwa lugha bandia nilotumia awali
 
Hapo hakuna jibu ila ukiona breki zimefeli fungua mlango wa kushukia kulia kwako toa mguu nje biga gaga mkuu lazima isimame
 
Mkuu sklful sijasema kwenye mteremko hii ina apply kwenye plain surface kumbuka remedy pekee ktk mwendo huo ni ku disengage na ndipo acceleration itashuka alternatively unaachia acceleration pedal...mteremkoni ni kesi nyingine mkuu...naona ukaamua unitusi kabisa
Vitu vingine mbona rahisi. Endesha gari mpaka 80kph kwenye tambarare halafu
1.toa mguu kwenye mafuta kitakachotokea immediately gari ya manual itaslow down then mwendo utakuwa mdogo kiliko gear itazima na kusimama. Gari auto itatoa gear yenyewe mpaka lowest gear then itakuwa inatembea kwa nguvu ya idle rpm.

2.ukiweka neutral gari auto or manual itazidi kuwa nyepesi na itaenda mbali sana mpaka momentum yake iishe.
 
Wewe mtoto unataka kuuwa watu ukiliweka neutral linachanganya balaa ngoma ikibuma breki tuliza akili kwa kasi ya kipanga angalia ni wapi pakuilekeza ukalimwage huko maana hakuna namna imagine unatoka Bugando hospital unashuka halafu ngoma ibume kinachofuata hapo utajaza mwenyewe any way kila mtu na akili yake ya udereva
 
Utauwa watu kwa ushauri mbovu. Ukiweks neutral gari inakuwa nyepesi na mara ingine inaongeza mwendo.

Unachotakiwa kufanya ni kuondoa mguu kwenye accelerator na kama gari ni manual punguza mwendo kwa kubadili gear yaani toa namba tano weka nne then tatu,mbili, moja.

Kama ni auto zipo zenye mfumo P R N D 3,2,1 hapo toa D weka 3,2,1 kama ni zile za P R N D 2 L achia mafuta mwendo ukipungua weka 2 then L.
imenibidi nipite tena nilidhani nausingizi mleta mada anataka kumaliza watu.. asante sana RRONDO
 
La
Mathalani upo katika speed ya 120/hr na ghafla breki zikafeli (automatic cars)

A. Utumie Hand Brake?
B. Uzime gari?
C.U jam gari katika Neutral?

JIBU:

Ukitumia mbinu A gari litasimama ghafla na ku skid upande kisha kubingilika hatimae ajali

Ukitumia mbinu B gari itajam mfumo wake wote usukani et al

C ndilo jibu sahihi...Weka gear lever yako katika Neutral kisha endelea kutafuta balance...ukiweka neutral maana yake ume disengage drive train na engine power kwa hiyo automatically gari litapunguza mwendo.

Nimeleta hili baada ya kusoma makala iliyobainisha kuwa miongoni mwa vyanzo vya ajali za private cars sababu ni kufeli engine

Ushauri wa ziada: Hakikisha kila baada ya kilomita 5000 mfumo WOTE wa brake unakaguliwa...ukihitaji msaada wa kiufundi usisite
Labda kama brake zimefeli uki mlimani au tambalale..zikifeli ukiwa katika mtelemko ukiapply c haiwezi kusaidia..pia umesahau kama gari ni manual trans inaweza ukajaribu kupangua gear let say kutoka namba 6 kwenda namba 4 na kama ni auto unapeleka gear kwenye L ama 2 itapunguza speed na kuepuka madhara makubwa.
 
Sure mteremkoni hii haifai ukiwa tambarare uka apply hii inasaidia...kumbuka ukiweka free na ukaacha kupress excelerator utakuwa umesaidia kupunguza speed to your safety...hata akili ya kawaida inagoma kwamba uweke neutral mteremkoni
 
Mleta mada acha kuaminisha watu kitu ambacho sio kweli; ushauri namba3 utaleta maafa badala ya manufaa. Nashangaa unavyoitetea kwa nguvu pamoja na kupewa maelezo ya kutosheleza na watu wengine. Acha hizo, hakuna ajuaye kila kitu. Kama ww ulifanikiwa siku hiyo haifanyi hiyo kuwa general rule. Naamini uzoefu wako katika hili si wa kutosha.
Kuweka neutral kutaongeza spidi tu Na si vinginevyo. Sasa sijui utalimudu vp gari kama spidi itaongezeka
 
Vw auto ilizima wakati nashuka mlima mkali mbeya, brake pedal ikaji-lock, starring nayo ikaji-lock kwa sababu Ile gari inatumia umeme kila sehemu. Nilichofanya ni kuvuta hand-brake taratibu mpaka gari ikasimama. Kuanzia siku hiyo naziogopa sana gari ambazo hazina traditional hand-brake ya kuvuta kwa mkono kwa sababu nisingeweza kucheza ule mchezo.
 
Back
Top Bottom