Ufanye nini brake zikifeli na uko katika mwendo kasi?

Ufanye nini brake zikifeli na uko katika mwendo kasi?

Nimefuatilia coment nyingi za watu humu, inaonyesha ni jinsi gani wabongo siku hizi tulivyowaelewa kwa asilimia kubwa.

mie la kwangu ni hili:
Ukiwa una drive hauwezi kukanyaga breki kama hakuna sababu
Kwa mujibu wa mtoa mada anasema "kama upo 120kh na breki zikafeli weka Neutral
gari itaendaa kisha itasimama taratibu'

Sasa basi tuanzie kutafuta mazingira ya eneo ulipo
1. Morogoro road
2. Pugu road
3. Mandela road
Kwa mfano upo maeneo tajwa hapo sio rahisi kwa kuwa maeneo hayo yana msongamano wa magari. na kama ulitaka kushika breki kwa kuwa mbele kuna gari au kivuko au chochote kilichosababisha ushike breki ni lazima usababishe ajali.

1. Sekenke
2. Kitonga
3. Wami
Hapo kama ni hili tatizo limekutokea mbinu ya kufanya ni hii alioisema PRONDO
TAHADHARI:
Kwa uhalisia kwa hapa bongo ili uende spidi kubwa ni kuhatarisha usalama wako
Kagua chombo chako vizuri kabla ujaanza safari.
Mengine yakijitokeza basi iwe bahati mbaya kweli.
 
fumba macho
1484904348007.jpg
 
Mathalani upo katika speed ya 120/hr na ghafla breki zikafeli (automatic cars)

A. Utumie Hand Brake?
B. Uzime gari?
C.U jam gari katika Neutral?

JIBU:

Ukitumia mbinu A gari litasimama ghafla na ku skid upande kisha kubingilika hatimae ajali

Ukitumia mbinu B gari itajam mfumo wake wote usukani et al

C ndilo jibu sahihi...Weka gear lever yako katika Neutral kisha endelea kutafuta balance...ukiweka neutral maana yake ume disengage drive train na engine power kwa hiyo automatically gari litapunguza mwendo.

Nimeleta hili baada ya kusoma makala iliyobainisha kuwa miongoni mwa vyanzo vya ajali za private cars sababu ni kufeli engine

Ushauri wa ziada: Hakikisha kila baada ya kilomita 5000 mfumo WOTE wa brake unakaguliwa...ukihitaji msaada wa kiufundi usisite
ukiona gari haishiki brake,tafuta tu pori au chaka zuri ukaliingize gari lako huko,au kwa lugha nyingine kula chocho tu.Ya nini kuhatarisha maisha ya wengine ukijaribu kujiokoa,kata kushoto ingia porini huko ukafe mwenyewe,ukipona basi Mungu mkubwa.
guys,be brave.Chagua kufa kishujaa protecting others.Chagua kupunguza casualties.Kwa mawasiliano zaidi wa namna ya kuchukua uamuzi huu w kishujaa,ni PM.Nitakujenga kisaikolojia uweze kujitoa muhanga
 
Kumbuka nimesema ukiwa kwenye mwendo mkubwa kama 120 per hr,kumbuka kwa mwendo huo action yoyote nje ya Neutral ni kupinduka hata hizo gia unazozitaja ukizi engage wakati say ukiwa 120 gari itasimama ghafla na ku skid,kumbuka hapa sizungumzii manual,I think wewe ndo unawadanganya watu kwa kuwaambia warisk zaidi kwa kuendelea Ku engage gia nyingine...
Mkuu bado ushauri wako si sahihi sanaaa.
Nina experience na hiki kitu na ukombozi pekee ulikuwa ni kuhama kutoka D mpk D2 mpk speed ilipopungua (40km/hr) ndipo nilipoanza kupandisha jino moja moja la hand brake ili kusimama na kuzuia kabisa gari.
 
ukiona gari haishiki brake,tafuta tu pori au chaka zuri ukaliingize gari lako huko,au kwa lugha nyingine kula chocho tu.Ya nini kuhatarisha maisha ya wengine ukijaribu kujiokoa,kata kushoto ingia porini huko ukafe mwenyewe,ukipona basi Mungu mkubwa.
guys,be brave.Chagua kufa kishujaa protecting others.Chagua kupunguza casualties.Kwa mawasiliano zaidi wa namna ya kuchukua uamuzi huu w kishujaa,ni PM.Nitakujenga kisaikolojia uweze kujitoa muhanga
Hahahahahhahaaa mkuu umetishaaa[emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Utauwa watu kwa ushauri mbovu. Ukiweks neutral gari inakuwa nyepesi na mara ingine inaongeza mwendo.

Unachotakiwa kufanya ni kuondoa mguu kwenye accelerator na kama gari ni manual punguza mwendo kwa kubadili gear yaani toa namba tano weka nne then tatu,mbili, moja.

Kama ni auto zipo zenye mfumo P R N D 3,2,1 hapo toa D weka 3,2,1 kama ni zile za P R N D 2 L achia mafuta mwendo ukipungua weka 2 then L.
Wewe ndiye umeelezea kitaaluma kuliko huyu mleta hoja otherwise ukifuata ushauri wake unaua watu au wewe mwenyewe. Kumbuka pia ukiweka neutral kuna uwezekano wa steering kujam na kukutupa usikotarajia
 
eeeh mi naona tu humu semina elekezi kibao za kuwafanya watu kuwa ngangari barabarani.Ni vema tukachukua uamuzi mgumu
Tatizo likitokoa ujuzi ndo utakuja hapo hapo.
Kwan mara ngapi tunasibia baharia kafa maji afu wasiojua hata kuogelea wamekutwa ufukweni.
Hahahahahhaa mie nilikuwa napita 2 huku mkuu
 
Mathalani upo katika speed ya 120/hr na ghafla breki zikafeli (automatic cars)

A. Utumie Hand Brake?
B. Uzime gari?
C.U jam gari katika Neutral?

JIBU:

Ukitumia mbinu A gari litasimama ghafla na ku skid upande kisha kubingilika hatimae ajali

Ukitumia mbinu B gari itajam mfumo wake wote usukani et al

C ndilo jibu sahihi...Weka gear lever yako katika Neutral kisha endelea kutafuta balance...ukiweka neutral maana yake ume disengage drive train na engine power kwa hiyo automatically gari litapunguza mwendo.

Nimeleta hili baada ya kusoma makala iliyobainisha kuwa miongoni mwa vyanzo vya ajali za private cars sababu ni kufeli engine

Ushauri wa ziada: Hakikisha kila baada ya kilomita 5000 mfumo WOTE wa brake unakaguliwa...ukihitaji msaada wa kiufundi usisite
Wala hilo siyo jibu"kwani ukiweka neutral gari linakua jepesi sana,, tena linakua na kasi ya ajabu,,,labda ufanye hivyo ukiwa tambalale na si mteremkoni....Maana utakufa hakika,,,ushauri wangu angalia mtaroni kama ni salama then unaipack hapo vizuri kabisa
 
Kwa kuongezea
Achia mafuta
Washa taa za dharura
Piga honi ya mojakwa moja
Ikishindikana toa gar elekezea mlimani,
Kama gar haina airbags na unajua unaenda ku hit kilima inamisha kichwa pale miguu ilipo
Kama linaenda kuporomoka bondeni, basi chomoa mkanda,ruka kwa kujiviringa kwa uelekeo wa gari...

Tusiombee hilo
hahahaaaa kama muvi
 
Gari zote ndoto ambazo hazitumii upepo ziwe manual au auto unaweza kusimama kwa kutumia gia pamoja na handbreak. Kinachotakiwa ni wewe kutokupanic na kujua ni kiasi gani unakanyaga au kivuta handbreak yako.kwani kiwango unachovuta au kukanyaga ndicho kiwango kinachobana tairi, usilogwe ukazima au kuweka free. Kutumia gia nako kunategemeana na ujuzi wa dereva mwenyewe kwenye utumiaji wake kwani unaweza kumletea madhara zaidi kama hutakuwa makini.
Kama ni gari kubwa tumia stop engine ikisaidiana na gia na kama ni suala la upepo tafuta sehemu ya kulilazia maana hakuna ujanja
 
Sasa huku kudanganyana, kwa hiyo ukiwa unashuka mlima mkali utaweka neutral ili gari ipunguze mwendo!!???? Sijui hiyo gari yako aina gani?!!!?
Hii inategemea mazingira uliyopo na muundo wa gari hivyo hapa hakuna jibu sahihi
True
 
Wewe ndiye umeelezea kitaaluma kuliko huyu mleta hoja otherwise ukifuata ushauri wake unaua watu au wewe mwenyewe. Kumbuka pia ukiweka neutral kuna uwezekano wa steering kujam na kukutupa usikotarajia
Tatizo tunasahau kuwa driving pia ni kama professional nyingine. Mtu aliyepata mafunzo sawia ya kuendesha, akichanganya na experience ana chances kubwa kuepuka ajali kwenye emergencies kama hiyo na nyinginezo. Kwanza kabisa, ukiendesha chombo cha moto weka 99% ya akili yako kwenye kuendesha. Ukiwa na safari ndefu au mwendo mkali kuanzia 80km/h, basi concentration yako iwe 100%. Ukiweza hilo hakuna emergency inaweza kutokea ukashindwa kujaribu kuicontrol kabisa. Kuendesha kitaalamu na kiusalama Zaidi ni kuwa na matarajio (anticipation) kama ilivyo kwenye mpira wa miguu, tarajia mtu au mnyama kuvuka barabara, tairi kupasuka ghafla n.k.
 
Vipi ukirudisha kwenye D2 ama L nini kitatokea?
Kama uko makini, hand brake is the safest way to pull you out of danger. Just do it in a different manner, with your finger pressing the release button continuously and you pull the handle in a way that does not lock your rear wheels. Automatic cars do change gears to the lowest as speed is decaying.
 
Kwanza kabisa hutakiwi kupanik kwa kuwa ndio wakati wa kutumia ujuzi wa elimu ya udereva uliyosoma kabla ya kupewa leseni.
 
Hicho ndicho unaweza kukifanya braking system iki stall am telling you this from expertise perspective wewe unaweza kutumia njia unayoona inafaa,ain't necessarily so for you to consider my advise lady

Mkuu gari ikiwa tambalale na hakuna magari mengine mbele yako wala ya kupishana nayo hii inaweza saidia....ila kilimani au ndo upo barabara za sehemu kama ya dar......haa mkuu utaswaga wengi tu.
 
Na haya magari yetu yanatumia mfumo wa umeme na upepo likibuma breki kila kitu hakifanyi kazi tena kwa akili yangu ngumu kama jiwe naangalia wapi kuna gema kubwa huko huko nalielekeza kitakachotokea ni mipango ya Mungu mimi huwa ni muoga sana wa kusababisha ajali bora nikajifie mwenyewe huko mtaroni sitaki kuliliwa na watu nigonga
 
Back
Top Bottom