Nifanye nini gari inaponizimia ghafla nikiwa kwenye mwendo mkali?

Complicator

JF-Expert Member
Aug 23, 2013
2,198
3,566
Wadau naomba kuuliza, sijawahi kuendesha gari automatic ila leo nimekutana na tukio la kuogopesha sana kiasi cha kuja omba ushauri.

Gari automatic ikizima ghafla inapoteza uwezo wa brakes na controll ya gari kwa ujumla,sasa leo katika kuendesha mteremkoni gari ikazima sababu ya matatizo ya engine, katika mwendo mdogo tu sababu kulikua na magari kadhaa mbele, sikugundua mapema kuwa imezima sababu engine yake haina mtetemo kabisa ila ghafla nikahisi nimepoteza controll, usukani mgumu na ninazikosa brake, naanza isogelea gari ya mbele kwa kasi bahati niliwahi hazard na wa mbele aliniona.

Nikajitahidi kucontrol gari hadi nikapaki pembeni,sasa nikawa nimeepuka ajali lakini mawazo yakanijia vipi kama ningekuweko mwendo mkali,si ina maana leo ingekua hadithi nyingine?!

Naombeni kuuliza,inapotokea dharura kama hii,dawa yake ni kufanya nini?!
 
Kwanza nikupe pole aisee.

Mimi nimeshawahi kunitokea kisanga kama hicho Ila nilichofanya nili-off gari alafu fasta nikaweka ON nikarudisha gear Kwenye neutral huku nafunga break ingawa ilisimama Kwa break za mbali (mara nyingi gari ikiwa ON mara baada ya ku-OFF mfumo wote wa gari unakuwa ON pia inakuwa rahisi kwa break na vitu vingine kuwa active).

Ila ukipagawa Kwa hiyo Hali ni rahisi kupata ajali maana akili yote inaruka na hapo ndipo utakumbuka gari za manual transmission haya yote yanakuwa rahisi kucontrol gari bila shida yeyote
 
Wadau naomba kuuliza,sijawahi kuendesha gari automatic ila leo nimekutana na tukio la kuogopesha sana kiasi cha kuja omba ushauri.

Gari automatic ikizima ghafla inapoteza uwezo wa brakes na controll ya gari kwa ujumla,sasa leo katika kuendesha mteremkoni gari ikazima sababu ya matatizo ya engine,katika mwendo mdogo tu sababu kulikua na magari kadhaa mbele...

Mkuu Pole sana.

Mimi niliwahi kuandika uzi wangu. Niliyoyazungumza humo yanafanana sana na yaliyokutokea leo.

Unaweza kuupitia...👇👇👇

Kuna umuhimu mkubwa sana kufanya check up ya mifumo ya umeme na electronics kwenye gari yako
 
Kwa gari automatic mara nyingi ni fuel pump failure, (pump ya mafuta inayokaa ndani ya tank) ikianza kufa ndio inaanza kule, cheki na fundi waifungue waicheki inaweza kua ni chanzo inapojizima aipeleki mafuta kwenye engine gari inazima tatizo.nilishakutana na tatizo la namna hiyo, zamani kidogo.
 
Wadau naomba kuuliza, sijawahi kuendesha gari automatic ila leo nimekutana na tukio la kuogopesha sana kiasi cha kuja omba ushauri.

Gari automatic ikizima ghafla inapoteza uwezo wa brakes na controll ya gari kwa ujumla,sasa leo katika kuendesha mteremkoni gari ikazima sababu ya matatizo ya engine, katika mwendo mdogo tu sababu kulikua na magari kadhaa mbele...
Cha kwanza usipanic, Vingine wataalamu wataendeleza
 
Kwa gari automatic mara nyingi ni fuel pump failure, (pump ya mafuta inayokaa ndani ya tank) ikianza kufa ndio inaanza kule, cheki na fundi waifungue waicheki inaweza kua ni chanzo inapojizima aipeleki mafuta kwenye engine gari inazima tatizo.nilishakutana na tatizo la namna hiyo, zamani kidogo.

Pump inazimaje tu wakati inapokea umeme?
 
Pump zinakufa japokua si mara kwa mara, hila zinafika muda zinaleta shida zinakua hazisukumi mafuta.
 
Mkuu naona watu wanajibu kisababishi badala ya nini cha kufanya.
Hebu ngoja nione kama na kumbuka general rule.

1. Usipack, hiyo ni changamoto tu. Sisi tunakuamini kuwa utatoka kwenye changamoto hiyo salama. Kwa hiyo huna haja ya kupanic

2. Kama ukivyofanya, toa ishara kwa madereva na wapita njia kuwa gari lako linahitilafu. Hapo kuna indicator, honi, mikono na nk.

3. Angalia mazingira yako, hapa angalia vitu ambavyo vinaweza kusaidia kulifanya gari lipunguze mwendo. Kumbuka kuwa hilo gari limezima kwa hiyo mfumo wa hydraulic utakua nao haufanyi kazi, vitu kama breaks and sterling hazitakua nyepesi kwa hiyo ni vyema kutafuta vizingiti natural au vipunguza speed.

4. Washa gari lako, Hapa sasa ndo sina uhakika napo kwa sababu mifumo inatofautiana.
Wakati unakoma kujaribu ulipeleka gari upande salama na kukanyaga break ili kulipunguzia kasi, jaribu kuwasha gari . Tunaambayo yanaweza kugoma sababu ulifanya hivyo kwenye d position, ikitokea hivyo angalia usalama alafu tumia shift/brake hamisha gear kwenda n. Kumbuka pia gari linaweza kuongesha kasi sababu d ilikua na ukinzani mkubwa kuliko ukinzani wa n.

Extra
Kama limewaka, shusha gear mpaka l au 1 then pambana na break na sterling sasa mpaka lisimame. Kama limegoma nenda kwenye kizuizi kalisugue gari mpaka lisimame huku unapambana na break.

Mwisho: hongera sana kwa kusimama salama, mshukuru Mungu alafu tafuta fundi tatua tatizo kabla hujafanya mazoezi ya kujiua
 
Mkuu

Kwanza pole kwa yaliyokupata. Pili unapaswa kujua magari mengi Kama sio yote ya siku hizi mifumobyake inaendeshwa kwa umeme hivyo gari linapozima mifumo yote haifanyi kazi kamainavyopaswa.

Nini ufanye ni kuweka switch baadhi ya mifumo itarudi kufanya kazi Kama kawaida hasa break na steering wheel.

Onyo Kama ni automatic usijaribu hata kidogo kuweka gia ya reverse au kuiweka kwenye parking, utajuta na unaweza kusababisha madhara makubwa.

Chanzo kikubwa Cha gari kuzima ghafla hasa ukiwa kwenye mwendo ni fuel pump kutofanya kazi vizuri. Sababu ya pili ni kulegea kwa pulley ambayo hufanya fan belt kutozungusha alternator ipaswavuo hivyo kuzalisha umeme mdogo au kwa interval(common zaidi usiku). Kulegea kwa terminal ya battery.

Sababu ingine ni kufa kwa throttle au can censor. Hivyo kutoruhusu umeme au mafuta.

Pole na ukipata tatizo Kama Hilo punguza panic. Washa gari ikiwaka tafuta fundi karibu akuangalizie hayo niliyoshauri
 
Inakuwaje pale inapozima kutokana na RPM kuwa chini sana, hususan gari ikiwa kwenye mwendo mdogo shida yaweza kuwa nini?
 
Back
Top Bottom