The Palm Tree
JF-Expert Member
- Apr 13, 2013
- 7,951
- 12,535
- Thread starter
- #101
kwingine nimekuelewa ila hapa...
endelea kutoa ufafanuzi wa kisheria...
je hati ikikosewa inatoa mwanya wa kuondolewa kwa kosa?
JIBU:
Absolutely, YES.
1. Kwa sababu, mashtaka hayo yanakosa sifa na vigezo vya kisheria kuitwa mashtaka na kesi hiyo inaishia hapo ktk hatua hiyo katika USO WA MAHAKAMA....
Hiyo ndiyo kazi ya Jaji/mahakama, yaani kuamua shauri kwa mujibu wa sheria...
2. Kwa polisi yaweza kuwa tofauti. Kama watakuwa bado wanadhani lipo kosa kwa mtuhumiwa huyo, ni jukumu lao kufuata sheria na taratibu za kipolisi kuanzisha mashtaka upya...
Kumbuka, HATI YA MASHTAKA [charge sheet] ndiyo sura nzima ya kesi/shauri lililofika mahakamani...
Kuikosea kwa namna yoyote ile, kwa Justice system iliyo serious & fair, basi hiyo inakuwa ni hatua ya kwanza kumpa faida (advantage) mshtakiwa kuupiga TKO upande wa mashtaka..
Haya ndiyo makosa wayafanyayo mara kwa mara waendesha mashtaka wa serikali ya Tanzania aidha kwa makusudi au kwa kutojua au kwa sababu ya nature ya kesi zenyewe wanazozipeleka mahakamani kuwa za hila, siyo halisi...