Mahakama Kuu yatupilia mbali pingamizi la Freeman Mbowe na wenzake, kesi kuendelea ikipangiwa Jaji mwingine

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
47,797
2,000
Kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili mwenyekiti wa Chadema mh Mbowe inaendelea leo kwenye mahakama ya mafisadi.

Pia soma > Mahakama ya Uhujumu Uchumi: Mvutano mkali kesi ya Mbowe na wenzake. Hatma ya kesi kujulikana Septemba 6

Mungu ampe wepesi mwanasiasa huyu nguli, amen

Mbowe.jpg

Freeman Mbowe akiongea na Mawakili wake

----
UPDATE: MAHAKAMA KUU YATUPILIA MBALI PINGAMIZI LA MBOWE
Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi imetupilia mbali pingamizi la Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na wenzake

Mbowe na wenzake walikuwa wakipinga Hati ya Mashtaka yanayowakabili wakidai ina kasoro za kisheria, hivyo kuomba Mahakama iitupilie mbali.

Pia soma > Jaji Elinaza Luvanda ajiondoa kuendesha kesi ya Mbowe baada ya washtakiwa kudai hawana imani naye
 

LESIRIAMU

JF-Expert Member
Feb 12, 2008
7,155
2,000
Kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili mwenyekiti wa Chadema mh Mbowe inaendelea leo kwenye mahakama ya mafisadi.

Pia soma > Mahakama ya Uhujumu Uchumi: Mvutano mkali kesi ya Mbowe na wenzake. Hatma ya kesi kujulikana Septemba 6

Mungu ampe wepesi mwanasiasa huyu nguli, amen

View attachment 1926049
Freeman Mbowe akiongea na Mawakili wake
Nadhani ni vyema mawakili wa Mbowe, wamshauri amkatae huyu jaji. Simuamini kabisa. Huyu na hakimu Simba wako kukandamiza haki.
 

SINGLE WINDOW

Senior Member
Sep 2, 2021
135
250
Hivi mawakili wa mbowe kwanini wasiachie kesi iendelee? hivi kuichelewesha kwa mapingamizi siyo kumuumiza mtuhumiwa kweli? mawazo yangu tu sijui sheria.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom