Baada ya Jaji Luvanda kutupa mapingamizi yote yaliyotolewa na Mawakili wanaomtetea Mbowe na wenzake, Mbowe amesimama na kumtaka Jaji Luvanda ajiondoe kuendesha kesi hiyo kwani ameonyesha upendeleo na taarifa zinasema ana maelekezo ya kupindisha sheria ili amfunge Mbowe na wenzake.
Jaji Luvanda amesema hati ya mashtaka ni batili amewashauri Mawakili wa serikali wakaibadilishe, Mawakili upande wa utetezi wamegoma wamemwambia kama hati ya mashtaka ni batili basi futa kesi Jaji akakataa ila amekubali kujiondoa kuendesha kesi.
====
Jaji Elinaza Luvanda wa Mahakama Kuu Divisheni ya Uhujumu Uchumi na Makosa ya Rushwa na aliyekuwa anaisikiliza kesi ya Uhujumu Uchumi namba 16/2021 yenye mashtaka sita yakiwemo ya Ugaidi, amejitoa kusikikiza kesi hiyo.
Sababu ya kujitoa katika kesi hiyo ni kutokana na mshtakiwa wa nne katika kesi hiyo, Freeman Mbowe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema Taifa, kuieleza mahakama hiyo kuwa yeye na washtakiwa wenzake watatu hawana imani na Jaji huyo katika kutenda haki dhidi ya kesi yao.
Kesi imehairishwa mpaka jaji mwingine atakapopatikana. Pia awali Jaji Elinaza Benjamin Luvanda alikataa kutoa uamuzi wake leo juu ya mapingamizi ya upande wa utetetezi mpaka atapopata hansard / kumbukumbu za majadiliano ya Bunge kuhusu sheria ya ugaidi.
Wote walikubaliana kuwa kesi hii ina masilahi mapana kwa umma wote waliopo ndani ya Mahakama na nje.
Hoja 3 za upande za upande wa utetezi zilikuwa zinashambulia madhaifu na kasoro ya hati ya mashtaka. Hoja ya kwanza ilikubaliwa na jaji wakati hoja ya pili ilikubaliwa kwa nusu yake na jaji wakati hoja ya tatu ya kutupiliwa mbali au kufutwa kesi, jaji aliikataa.
Na kwa msingi huo mtuhumiwa Freeman Mbowe kwa niaba ya wenzake akasimama na kusema hawana imani na Jaji Elinaza Benjamin Luvanda kuendelea kusikiliza kesi hiyo, na mheshimiwa Jaji E.B Luvanda akaafiki ombi hilo na kujiengua kusikiliza kesi hii.
Source : Mwananchi Digital
UPDATE: Jaji Luvanda akubali
Jaji Elinaza Luvanda aliyekuwa anaisikiliza kesi ya Uhujumu Uchumi nyenye mashtaka 6 yakiwemo ya ugaidi, amejitoa kusikiliza kesi hiyo, sababu ya kujitoa kwake, ni kutokana na mshtakiwa wa nne katika kesi hiyo, Mhe. Freeman Mbowe na wenzake kuwa hawana imani na Jaji huyo.
Pia soma >
Mahakama ya Uhujumu Uchumi: Mvutano mkali kesi ya Mbowe na wenzake. Hatma ya kesi kujulikana Septemba 6
. "Jaji Mwenzangu Luvanda" Machozi ya samaki majini hayatakufikia wewe na kizazi chako mpaka cha nne, tekeleza maagizo
. CHADEMA tusimpe vitisho Jaji Luvanda, mpaka sasa hajapendelea pande yoyote. Kibatala na jopo lake walichemka