#COVID19 Ufafanuzi: Muuguzi aliyemchoma chanjo Mhe. Rais Samia na viongozi wengine kutovaa mipira ya mikono (gloves)

Mbona daktari aliyemchoma sindano Uhuru Kenyatta alivaa gloves kwa nini nyie mnaleta dharau na afya ya mkuu wa nchi?
 
20210729_081043.jpg
 
Kwa mujibu wa taarifa hapo juu, Gloves sio lazima kuvaliwa wakati wa kuchoma chanjo ya COVID-19.

Hivyo tunapenda kuwatoa hofu wananchi kuwa Mhudumu aliyewachoma chanjo Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na viongozi wengine alikuwa anatekeleza majukumu yake kwa kufuata taratibu zote ikiwemo kusafisha mikono yake kwa kutumia vipukusi kabla na baada ya kutoa huduma.

#Jikinge, wakingeWengine
Chukua hatuaView attachment 1871870View attachment 1871871

PIA SOMA:

- #COVID19 - Ikulu: Imekaaje viongozi kuchomwa chanjo ya Corona bila wauguzi kuvaa gloves?
Upumbavu kabisa.Yaani mnatuletea Drective kutoka CDC kama jibu.Yule alikuwa ni RAIS wa nchi AFYA yake ni kipaumbele.Acheni SIASA kwenye afya ya RAIS.Kubalini kwamba walikosea.Tena screenshot
 
Kwa mujibu wa taarifa hapo juu, Gloves sio lazima kuvaliwa wakati wa kuchoma chanjo ya COVID-19.

Hivyo tunapenda kuwatoa hofu wananchi kuwa Mhudumu aliyewachoma chanjo Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na viongozi wengine alikuwa anatekeleza majukumu yake kwa kufuata taratibu zote ikiwemo kusafisha mikono yake kwa kutumia vipukusi kabla na baada ya kutoa huduma.

#Jikinge, wakingeWengine
Chukua hatuaView attachment 1871870View attachment 1871871

PIA SOMA:

- #COVID19 - Ikulu: Imekaaje viongozi kuchomwa chanjo ya Corona bila wauguzi kuvaa gloves?
Ahsanteni sana wizara ya Afya kwa kuwa nanyi katika JF ili tuweze kupewa habari kutoka wizarani kwenu, lakini nasi tuna vijiswali tunaomba kujuzwa.
1- Chanjo tulizoletewa nadhani ni kama milioni moja, idadi ya wananchi tukadirie ni milioni 55, je tutarajie kupata chanjo za kutosha huko mbeleni?
2- Kwani mpaka jamii ifikie Herd Immunity inabidi asilimia kadhaa ya watu wake wawe wameshachanjwa je kwa hapa Tanzania mnapanga asilimia ngapi ya watu wachanjwe ili tufikie hiyo herd immunity?+-
3- Na hiyo chanjo itakuwa ni ya dose moja tu au zaidi?
4- Kutokana na kuwa aina mbalimbali za chanjo na inavyoonyesha kuna baadhi ya nchi zinakubali aina kadhaa ya chanjo na kuzikataa aina nyingine, sisi kama Tanzania nasi tutakuwa na uchaguzi huo wa chanjo au ndiyo kila tutakayoletewa tutaipokea?
5- Watu kusainishwa fomu ya serikali kutowajibika ikiwa chanjo italeta madhara, huku si kuwatia hofu na kuwavunja moyo watu, na ikitokea hivyo watu wamedhurika watakimbilia wapi?
6- Chanjo ni hiari lakini katika baadhi ya kada wao watalazimika kuchanjwa, uhiari upo wapi?
Maswali yapo mengi, na tujaribu kutoleta siasa katika jambo hili, kwani hili jambo ndiyo litapelekea kuonyesha Tanzania tunaelekea wapi kama taifa.
 
Mi Tanzania huwaga sielewi wanatushauri tusikusanyike ila wao wanatukusanya mfano leo kwenye uzinduzi sikuona umuhimu wa kujaza watu kuja kushuhudia uzinduzi, ivi kulikua haiwezekani mh Raisi akapata chanjo yeye na mumewe au watu wachache mbele ya kamera the anatoa hutuba kuhamasisha watu wengine wafuatilie kupitia media
Nimiongoni mwa maajabu 7 ya dunia

Sent from my TECNO WX3 using JamiiForums mobile app
 
Kwa mujibu wa taarifa hapo juu, Gloves sio lazima kuvaliwa wakati wa kuchoma chanjo ya COVID-19.

Hivyo tunapenda kuwatoa hofu wananchi kuwa Mhudumu aliyewachoma chanjo Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na viongozi wengine alikuwa anatekeleza majukumu yake kwa kufuata taratibu zote ikiwemo kusafisha mikono yake kwa kutumia vipukusi kabla na baada ya kutoa huduma.

#Jikinge, wakingeWengine
Chukua hatuaView attachment 1871870View attachment 1871871

PIA SOMA:

- #COVID19 - Ikulu: Imekaaje viongozi kuchomwa chanjo ya Corona bila wauguzi kuvaa gloves?
Nilitegemea hili lingeonekana pia kwenye GUIDELINE ya wizara kuhusiana na masuala ya UVIKO-19 maana miongozo ndio inayotumika kwa sehemu kubwa katika kutoa huduma za afya na hivyo inapaswa kuwa comprehensive kwa kiasi cha kutosha na uvaaji gloves kama PPE (Personnel Protective Equipment/kifaa kinga) ni sehemu ya IPC (Infection Prevention and Control).
 
Mleta mada kapandisha Uzi na kula nduki,maswali yenu mkaulize bibi zenyu Kwa nyumbi hi mbombi Hii

Dadeq this is Tanzania!
🏃🏃🏃
 
Wizara ya Afya Tanzania tafadhali toleeni ufafanuzi na hili la gwajima kuepusha mkanganyiko zaidi.. Kumbukeni impact yake kwenye hili sio nzuri.. Tafadhalini msikae kimya.. Mnapaswa kutoa ufafanuziView attachment 1872358
Huyu jamaa mtata, tuone TISS na umahiri wao watafanyaje maana ametoa accusations za conspiracy eti wao wanachanja fake wakitambua madhara ya hiyo vaccination. The porn star Gwajiboy has real guts.
Yaani hapo ni amemtuhumu bibi wa Hijab na system nzima kwa nia ya kudhuru umma kwa sababu ya fedha.
 
Hilo zoezi la jana labda kama lengo lilikuwa ni ku promote chanjo lakini aingii akilini doze yenyewe ni 1 millioni halafu ukampige chanjo Majaliwa, Gwajima, Jokate na wengineo under 60 wenye afya zao watu ambao wakipata COVID wanaweza ata wasijue.

Halafu uache wazee wenye 65+ na watu wenye magonjwa kama kisukari na tia maji tia maji wengine ambao wakipata COVID risks za kuishia hospitali na kuondoka ndio kubwa zaidi especially maeneo yenye baridi.

Nina uhakika hili zoezi halina strategy watu wamejiagizia chanjo lakini hakuna utaratibu sahihi wa kutoa hizo chanjo kutokana na priority za risks watu walizonazo.

Chanjo ni salama lakini zina side effects zake ndogo ndogo kwa baadhi ya watu; binafsi nilidungwa AstraZeneca huku kijijini kwetu bega baada ya masaa kadhaa liliuma kwa siku mbili mkono walionidunga ila niliambiwa side effects zote kabla ya chanjo so sikuwa shocked. Chanjo ya pili sijapata side effects na wengine ya kwanza poa ya pili wanapata side effects. Hiyo ni kwa chanjo zote ata waliopigwa Pfizer wengine walipata homa.

Kwa nini nasema hivi knowing jinsi watanzania wanavyopenda kuzusha kuna watu watakumbana na worst side effects ya hizo chanjo na kutumiwa kama case study kupotosha ilhali chanjo ni salama mwisho wa siku.

Halafu hakuna sababu za kulazimishana asietaka aachwe, kasheshe siku akikumbana na COVID especially wale ambao ni vulnerable group.
 
Mkuu kwani huyo mtoa huduma alikuwa anatoa huduma kwa wagonjwa? Wagonjwa wanapewa tiba na si chanjo
Kama wana ukimwi je?, Au haina shida hiyo. Usisahau damu inabeba magonjwa mengi tu yajulikanayo na yasiyojulikana pia.
 
Back
Top Bottom