#COVID19 Tarafa ya Mihambwe wamuunga mkono Rais Samia chanjo covid-19

wandamba

JF-Expert Member
Apr 29, 2014
510
839
Na Mwandishi wetu Mihambwe

Wakazi Tarafa ya Mihambwe wamehasika vilivyo kwa hiyari yao kupata chanjo ya Uviko 19 (Corona) mara baada ya kuelimishwa na huduma kusogezwa jirani na Wananchi.

"Nashukuru sana kupata chanjo ya Corona, niwaombe Watanzania wenzangu tuendane na Dunia ilivyo, na sidhani kuna Mtanzania ama kiongozi yeyote yule anataka kuwatesa Wananchi. Tuchanje ili kupunguza madhara ya ugonjwa huu." amesema Ndaile Abdallah Ulaya mkazi Kijiji cha Dinyeke.

Muuguzi Asha Kasembe amewahimiza akina Mama na Wananchi wote wapate chanjo kwani ni salama na inaimalisha kinga za mwili na kupunguza vifo na inapunguza makali.

Pia Afisa Tarafa Mihambwe Emmanuel Shilatu ameungana na Rais Samia kupambana na ugonjwa huu kwa kuwapa elimu Wananchi, kuwahamasisha na wanaoridhia wanapata chanjo bure.

"Dunia ipo kwenye mapambano ya Uviko 19 nasi Tarafa ya Mihambwe tunaungana na Rais Samia kupambana na ugonjwa huu kwenye vijiji na vitongoji kuwaelimisha, kuwahamasisha na tumeona Watu wengi wamejitokeza kwa hiyari yao kupata kinga kutokana na huduma ya chanjo kuwafikia jirani nao. Nazidi kusisitiza Wananchi wa Tarafa ya Mihambwe tuendelea kuchukua tahadhari ya ugonjwa huu wa Corona kwa kuvaa barakoa, kunawa mikono kwa vitakasa mikono, kuepuka mikusanyiko na kupata chanjo ya sindano ya Corona" alisisitiza Gavana Shilatu.

Katika zoezi hilo Mamia ya Wananchi wamejitokeza kupata chanjo ya Corona na zoezi hilo litakuwa endelevu ndani ya Tarafa ya Mihambwe.


FB_IMG_1632943996431.jpeg
FB_IMG_1632944008075.jpeg
FB_IMG_1632944013106.jpeg
FB_IMG_1632944000494.jpeg
 
Tatizo ni umasikini, wamepewa chumvi na sabuni ili wakusanyike na kuchanjwa, umasikini ni mbaya sana, unaweza kula hata mavi.
 
Back
Top Bottom