Uelewa Mdogo wa Misingi na Maadili ya Uandishi wa Habari sababu kubwa ya kushuka kwa viwango vya tasnia hii

Nengay

Member
Aug 26, 2022
39
65
Tasnia ya uandishi wa habari katika nchi zinazoendelea mfano Tanzania inakumbwa na changamoto nyingi ambazo zinatajwa kila siku mfano, citizen journalism ambayo imempa nafasi kila mtu kuweza kuhabarisha watu popote alipo kupitia simu yake ya mkononi.

Ambapo kwa upande wangu Changamoto kubwa inayosababisha kuingiliwa sana kwa tasnia hii katika utendaji na utekelezaji wa majukumu yake ni "UELEWA MDOGO WA MISINGI NA MAADILI YA UANDISHI WA HABARI" kwanza

• Pamoja na kutungwa kwa sheria, kanuni na maadili " code of conducts" yatakayomwongoza mwandishi kuishi na kutenda katika misingi ya kazi yake bado taratibu hizi hazifatiliwi katika upande na kiwango cha kuweza kuongeza ustawi na ufanisi katika tasnia hii.

• Kufuatia agizo la kuongeza elimu kwa waandishi wasiokuwa na elimu ya kutosha ni sawa lakini Elimu pekee yake isiwe kigezo cha kumfanya mtu awe mwandishi wa habari kuwe na ufuatiliaji wa utendaji wao pamoja na kuwa na elimu. "JOURNALISM ITS ALL ABOUT RESPECT OF HUMANITY AND INTEGRITY" kupata nafasi ya kuisemea umma/jamii ni dhamana kubwa iheshimiwe.

• Maadili ya uandishi wa habari hapa nchini na duniani kote yanamtaka mwandishi asitoe habari yoyote ya kusababisha maafa "harm" kudhalilisha, habari isiyo kamili, isiyo linganifu au isiyo sahihi kwa mantiki hii mwandishi anatakiwa kutazama kwa jicho pevu achanganue kati ya MAADILI YA UANDISHI WA HABARI NA MAADILI YA JAMII YAKE kwa mfano, katika jamii zetu suala la mapenzi ya jinsia moja ni haram , kwenye suala hili mwandishi hatakiwi kuendeshwa na hisia binafsi na jamii ilihali jambo hili kwetu haliruhusiwi lakini sasa limetokea na linaendelea kukua HAAMAANISHI UJIO WA TARATIBU ZISIZO ZA KWETU ZIVUNJE MAADILI YA UTENDAJI WA TASNIA YOYOTE.

Kwenye suala la ushoga mwandishi hatakiwi kumshambulia mtu kwasababu ni shoga anatakiwa afanye kazi yake kama maadili yanavyomtaka kama anapinga ni sawa lakini akapingie kwenye page yake sio kwenye vyombo vya habari, Waandishi wanalalamika tasnia haieshimiwi inaingiliwa sana lakini wao wenyewe hawaitendei haki tasnia hii na ndio maana kutofautiasha kati ya mwandishi na mtu asiye mwandishi ni kazi sana.
 
Changamoto kubwa ni njaa Kwa waandishi ndio maana wengine wamefikia hatua ya kujitoa utu.
 
Ajira zenyewe kwenye media ziko wapi kiasi cha kumfanya mwandishi apate mshahara mzuri kuweza kuendesha maisha yake tu ya kawaida? Tatizo hakuna proper standard employment kwenye media nyingi wanaokoteza watu tu ili mradi wanajua kuongea sana, kuchezesha muziki, kupiga picha na mengine ya kuzugia kuwa kuna media ipo inafanya kazi. Hata ukisoma sana media gani itakuajiri bila kuwa mbunifu wa vipindi na namna ya kuandika habari/makala? Wengi ni waandishi wa kujitegemea wa hapa na pale wasiokuwa na uhakika wa malipo ya kazi zao kwenye media wanazozifanyia kazi. Laumuni mitandao ya kijamii iliyokuja, watu wanajiandikia, kupiga picha na kutoa taarifa bila kuwa na mafunzo ya uandishi wa habari na maadili yake
 
Changamoto kubwa ni njaa Kwa waandishi ndio maana wengine wamefikia hatua ya kujitoa utu.
Maslahi ya waandishi ni mabaya sana lkn ile kazi inahitaji moyo wako pale kwa ajili ya jamii
 
Back
Top Bottom