"Changamoto ya Uadilifu na Maadili katika Utumishi wa Umma ni tatizo kubwa sana kwa nchini Tanzania"

covid 19

JF-Expert Member
May 9, 2014
4,886
10,616
Katika jamii ya Kitanzania, suala la uadilifu limekuwa changamoto kubwa sana, na hizi dhiar za mwenezi, Mheshimiwa Paul Makonda, zinztoa mfano mzuri wa hili. Mheshimiwa Makonda amekuwa akionekana kupokea kero nyingi zinzogusa sekta tofauti tofauti hiki ni kielelezo cha jinsi mifumo ya serikali imeshindwa kudumisha uadilifu. Matendo yake yamezua mjadala mkubwa kuhusu uwajibikaji na maadili kwenye utumishi wa umma.

Tofauti na jukumu la kuleta maendeleo na ustawi wa jamii, watendaji wengi wamekuwa akifanya maamuzi ya upendeleo na kukiuka misingi ya haki na uadilifu. Kuna ushahidi mwingi wa matumizi mabaya ya mamlaka na ufisadi katika utendaji wao.

Hii inaonyesha jinsi tatizo la uadilifu limepenya kwenye ngazi za uongozi nchini Tanzania. Ni dhahiri kuwa kutokuwepo kwa uwajibikaji na uadilifu kunakwamisha maendeleo ya taifa na kuhatarisha imani ya umma kwenye mifumo ya serikali.

Kwa hiyo, ni muhimu sana kwa serikali na jamii kwa ujumla kuchukua hatua za dhati katika kurekebisha hali hii. Hatua za kisheria, kama kuimarisha mifumo ya uwajibikaji na kujenga taasisi imara za kupambana na ufisadi, zinapaswa kuchukuliwa. Vilevile, elimu na uhamasishaji kuhusu umuhimu wa uadilifu na maadili katika uongozi a watendaji ni muhimu.

Kwa kufanya hivyo, tunaweza kuanza safari ya kujenga jamii yenye uadilifu na maadili, ambayo itawezesha maendeleo endelevu na ustawi wa wote. Ni wakati wa kuchukua hatua thabiti kuhakikisha kuwa uadilifu unakuwa msingi wa utawala na uongozi nchini Tanzania.
 
Bahati mbaya ndio zao la jamii yetu.Utitiri wa dini haujasaidia ni vyema turudie kwenye mkono wa chuma.
 
Haiwezekani shina lioze matawi yachanue
Ukosefu wa uadilifu na maadili katika utumishi wa umma unasababishwa na serikali iliyopo madarakani kwao rushwa na ufisadi ni mambo ya kawaida.
 
Ni tatizo kama litaendelea kuchukuliwa poa tutakuwa taifa la ajabu sana huko tuendako..
 
Back
Top Bottom