UEFA: Real Madrid, Villarreal zaingia nusu fainali, Chelsea, Bayern hoi

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
960
2,618
FQLEmghWUBoX_IR.jpg
Timu za Real Madrid na Villarreal zimefanikiwa kufuzu Hatua ya Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuziondosha mashindanoni Chelsea na Bayern Munich katika mechi za kuamkia leo Aprili 13, 2022

Chelsea ambayo ilifungwa mabao 3-1 katika mchezo wa kwanza, ilipambana na kufikisha mabao 3-1 katika dakika 90, baada ya dakika za nyongeza, mfungaji Karim Benzema aliipitisha Madrid kwa bao nzuri, matokeo yakawa 3-2, jumla Madrid ikipita kwa mabao 5-4.

Bayern Munich imepata sare ya bao 1-1 dhidi ya Villarreal ikiwa nyumbani, hivyo kuondolewa kwa mabao 2-1 kwa kuwa katika mchezo wa awali Villareal ilishinda bao 1-0

Kwa matokeo hayo Villarreal itacheza na mshindi wa mechi ya Benfica na Liverpool wakati Real Madrid inasubiri mshindi wa mchezo wa Manchester City dhidi ya Altetico Madrid.

Mechi za kwanza za Nusu Fainali zitapigwa Aprili 26/27 na marudio ni Mei 3/4, 2022.
FQKyUsUXsA0Hqc1.jpgSource: Daily Mail
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

5 Reactions
Reply
Top Bottom