JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,316
- 5,479
Chelsea ambayo ilifungwa mabao 3-1 katika mchezo wa kwanza, ilipambana na kufikisha mabao 3-1 katika dakika 90, baada ya dakika za nyongeza, mfungaji Karim Benzema aliipitisha Madrid kwa bao nzuri, matokeo yakawa 3-2, jumla Madrid ikipita kwa mabao 5-4.
Bayern Munich imepata sare ya bao 1-1 dhidi ya Villarreal ikiwa nyumbani, hivyo kuondolewa kwa mabao 2-1 kwa kuwa katika mchezo wa awali Villareal ilishinda bao 1-0
Kwa matokeo hayo Villarreal itacheza na mshindi wa mechi ya Benfica na Liverpool wakati Real Madrid inasubiri mshindi wa mchezo wa Manchester City dhidi ya Altetico Madrid.
Mechi za kwanza za Nusu Fainali zitapigwa Aprili 26/27 na marudio ni Mei 3/4, 2022.
Source: Daily Mail