UEFA Champions League, Special Thread

UEFA Champions League, Special Thread

Status
Not open for further replies.
Usimuone Simba kalowana maji ukadhani Mbuzi, kawaulize wazee wa Serie A kilichowakuta.

Mambo ya kutoa sare yasifanye uione Barca imekwisha, kumbuka Messi alikuwa majeruhi sasa yupo fit.

safari hii bavarians wapo vizuri si wamasihala kabisa na ninavyowajua huwa hawaanziagi ugenini kule ugenini wanaenda kukutoa tena atatoka kama alivyomtoa psg just wait buddy..
 
safari hii bavarians wapo vizuri si wamasihala kabisa na ninavyowajua huwa hawaanziagi ugenini kule ugenini wanaenda kukutoa tena atatoka kama alivyomtoa psg just wait buddy..
Hata mimi ningependa iwe hivyo tatizo ni moja tu, huyu Simba amelowa maji tu.
 
sasa mbona hata tarehe ya games hamuandiki, chebi bwana ndio kuripoti nini sasa km vile haupo huko bwana, tupe tarehe sasa, tuanze ushabiki mapemaaaaa........mwezi wa tano ni kesho tu mazee!!!!!
 
Last edited by a moderator:
Usimuone Simba kalowana maji ukadhani Mbuzi, kawaulize wazee wa Serie A kilichowakuta.

Mambo ya kutoa sare yasifanye uione Barca imekwisha, kumbuka Messi alikuwa majeruhi sasa yupo fit.
Katika defence, wachezaji wengi wa Barca wanachezeshwa out of their natural positions, mfano Masch ni pure midfield, lakini anachezeshwa kama beki wa kati, Piqe pia ni kiungo, naye anacheza beki ya kati.
Hawa makeshift defenders wameanza kuonekana si lolote sasa ni kwa sababu tu ya tofauti ya mbinu za ufundishaji kati ya Pep na Tito. wakati wa Pep hawa wote walikuwa vizuri na ndo sababu ilikuwa vigumu kuona matobo kwenye backline.
Beki wa kati pekee anayeaminika ni Puyol, ingawa naye naturaly ni full back, sasa tatizo katika mechi ya PSG ni Adriano kucheza sentahafu, kwanza mfupi na pili ni winga na akawa anakabiliana na world class stricker, Zlatan. Ikabidi Alba asipande kama kawaida yake ili kufukia ubovu wa beki ya kati, hali kadhalika Busqet akalazimika kucheza chini zaidi, lengo ni lilelile kuficha ubovu.
Kama Tito angekuwa Pep nadhani Bartra angekuwa keshapata uzoefu kiasi cha kuweza kuwakabili watu kama Toni Kroos, lakini hatuoni kama huyu mtoto(20 yrs) anaaminiwa na kocha licha ya kuwa ni natural centre back na kafanya vizuri sana na timu za vijana za Spain.
So kosa kubwa kwa Barca ni kumnunua Song badala ya kuhangaikia beki wa kati.
 
Batra ni natural centre back na ana kiwango kikubwa,nashangaa kwa nini Tito/Roura hawampi nafasi huyu dogo wakati ni mzuri kuliko kuwachesha Mascherano/Adriano/Song ambao sio mabeki wa kati.Jose Mourinho ameamua kuwapiga benchi Cavalho na Pepe na kumpa namba kijana Rafael Varane ambae ameonyesha kiwango kikubwa sana.Batra inabidi apewe nafasi apate uzoefu ili aje kuziba pengo la Puyol ambaye majeruhi yanamsumbua sana
 
BONGE LA MECHI: Ni UEFA 2013 semifinal kati ya Bayern Munich na Barcelona.
Champions League, usiku wa leo Apr 23, 2013, itakuwa mechi nzuri na kali sana, kati ya vigogo wa soka duniani - Stay connected with JF Sports kupata Live Updates.
===
Uwezekano wa timu mbili kutoka Ujerumani au timu mbili kutoka Uhispania kukutana mwezi ujao katika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya Champions League bado uko hai, na majibu, dalili za nani zaidi zikaanza kuonekana baada ya matanage wa leo.

Ni baada ya timu za Uhispania na Ujerumani kutenganishwa katika droo iliyofanywa katika makao makuu ya shirikisho la soka ulaya UEFA ya nusu fainali.
Fainali itafanyika uwanja wa Wembley jijini London huenda ikawa pambano jingine la Ujerumani na Uhispania.
Bayern Munich ambao walishindwa katika fainali mwaka jana, na ambao tayari wamenyakua taji la Bundesliga, wanaangushana na viongozi wa La liga Uhispania.

Katika mchuwano mwingine, Borussia Dortmund watakabana koo na Real Madrid wakati wawakilishi wa miamba ya sasa ya soka barani Ulaya wakiumiza nyasi.

Mechi za mkondo wa kwanza utachezwa leo Aprili 23 na kesho 24, huku za mkondo wa pili ukichezwa Aprili 30 na Mei mosi.

Fainali itachezwa jijini London katika uga wa Wembley mnamo Mei 25.
===
 
Muendelezo mbaya wa barcelona wanapokua ugenini hivi karibuni unaleta presha kubwa ndani ya club hasa zaidi kwa wachezaji ambao ata hivyo watakua na kipenzi cha macho ya wapenda soka lione messi anapotarajiwa kushuka dimbani baada ya kupumzishwa kwenye mechi kadha za la liga!moja ya timu zenye uzoefu wa kutosha wa michuano hii ni buyern munich timu ngumu inayoweza kufanya itakalo kama utakuja kichwa kichwa wako nyumbani wana kila sababu ya kuondoka na ushindi ili kujiweka vyema kwa mechi za marudiano ambazo zinatarajiwa kua ngumu zaidi!barcelona inapokua kwenye kiwango chake hua ni timu hatari bila kujali inacheza wapi tatizo kubwa upande wao ni kuonekana wepesi wa kuruhusu magoli jambo ambalo ni hatari mno kwa timu zenye kariba ya buyern munchen!
 
Barcelona ni timu ambayo mpenzi yoyote wa mpira lazima ai admire-jinsi wanavyotandaza gozi is a sight to behold,yaani hawa barca wameipandisha soka to another level.Bayern wana ile german spirit,wana nguvu kazi ya kuuwezesha mpira kufika mbele,they may play bad but fighting spirit yao ikawapeleka across the line. mpira wa leo is to close to call-but all the best Barca cause brand yao ya football inatupa entertainment isiyo na kipimo
 
Kwa kuwa natamani sana kombe liende Spain basi nalazimika kuiombea mema Barca kama Yanga walivyoishangilia Simba dhidi ya Azam. Japo ni nafuu kwa Marid kucheza fainali na Bayern kuliko Barca.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom