UDSM mwaka huu kuna nini?

Nadhani mkuu hukunielewa
Hata hivyo mtoa mada pia alitakiwa abainishe bayana wazi wazi

Hizo kozi za engineering na capacity zake hapo udsm ndio tungejua shida nini?

Sasa sio kila mtu amesoma udsm kwamba anajua ila wangeweka capacity ndio tungejua kwanini watu wanakosa hapo.

Pia entry qualification ndio tungejua

Lakini kwa ufahamu wangu unakuta kozi inahitaji watu 150 na wameomba watu 500 hapo hakuna namna ila kuomba vyuo vingine tu basi ndio solution.
 
Ukweli ni kwamba capacity ya vyuo vikuu huu mwaka iko limited sana na TCU inejisahau kua ufaulu uneongeza kwa kiwango kikubwa.
Mfano TCu anabana vyuo vikuu kwa ratio ya 1:50 students per staff ukijiuliza hii inawezekanaje? Hata shule za sekondari hazifanyi hivi.
Kwahiyo unaweza kuta kwa mihemko yao wanataka somo moja linalochukiwa na wanafunzi mfano 600 one subject ifunzwe na walimu 12 how is it possible? Na hapo ndo wanakuja na issue ya capacity

Hii mada ililetwa hapa wiki kadhaa watu wakafanya mzaha.
Subiri uone these year wanafunzi wengi sana watakosa vyuo kwa uzembe na mihemko ya watu wacheche kwenye hizi taasisi za serekari zinazo simamia vyuo vikuu.

Zaidi nadhani unaposema Ratio nadhan hawa jamaa hawajui kitu mfano udsm darasa au hall linaweza beba wanafunz 800 par once mwali akafundish vizur na ikaeleweka course.

Mifumo yetu ya elimu ya juu inaongozwa na watu ambao hawako updated wanadhani mambo ya mwaka 1900 huko yako applicable 2025.

Pia hawakufanya tathimi ya ongezeko la mashule ya kata amabayo yamemwaga wanafunzi wengi na ufaulu uko juu.

Tukiendelea hivi tutajikuta tuanzima ndoto za vijana wengi sana kwa ukorofi wa watu wachache pale TCU
 
Qualifications za kusoma kozi yoyote UDSM ni D mbili tu. Sasa kama capacity ni kudahili wanafunzi 100 na waombaji ni 1000 utawachuja vipi hao ubaki na 100?
Hii issue ya capacity bila kujua madhara yake itasumbua sana mwaka huu vijana wengi watakosa vyuo.TCU ametoa very low capacity kwa vyuo mwaka huu na amafanya mabadiliko ya mitalaaa kwa mihemko ikiwemo kufuta fani mbalimbali.

Mfumo wetu wa elimu umebaki kua wa kuchokonolewa kila mara subiri inyeshe tujue oanapovuja
 
UDSM ndiyo Cambridge au MIT yetu. Wanaoenda pale ni top ya top layer. Kwa vile siku hizi ni kawaida kukuta form 6 darasa zima lina one za point 3 PCM, PCB, CBG...hakuna namna. Aende hata UDOM au MUST huko siyo lazima UDSM....
 
Cocastic kumbe ukipigwa mboko vizuri unamwaga pwenti point pwenti.
Hapa nakupa misumari yako, maua badae😁
 
Hoja yako bado aina mashiko hata kidogo issue ya capacity lazima izingatiwe .

Kwa sababu zifuatazo.
1. Mazingira ya kijifunzia mfano computer,laboratory,workshops.
2.kuna baadhi ya kozi awawezi soma watu wengi kwa sababu zina demand more practical. Sasa uwezi kuwa na watu 600 wote wapige pratical itakuwa ngumu.

Kweny upande wa vyuo kila siku vyuo vinaongezeka sema wanafunzi wengi wanaona kusoma udsm ndio kila kitu .
Tanzania miaka ya 90S na sasa hivi kunaongezeko la vyuo na vingine vimepanda adhi kutoka vyuo vya kati mpk vyuo vikuu.

Ni kweli kunaongezeko la ufaulu lakn pia kunaongezeko la vyuo pia.

Kwenye issue ya cut off point hapo wanafunzi ndio wakupewa lawama kwa sababu .mfumo ndio unachakata kwa hiyo wanafunzi wangetakiwa kuweka effort kweny kusoma .
 
UDSM wanafanya mambo ya kizamani sana.

Wasichojua ni juwa dunia ya sasa ufaulu unaongezeka sana one zipo kibao sawa ila sasa sio nyingi kama inavyosemwa

Wote hawawezi kusoma hapo sawa ila hata huyo mwenye 1.5 kweli?? Anakosa??
Ndo nimeshangaa hapo, mtu mwenye 1 ya 5 anakosa nafas UDSM. LOL
 
Pa1 na hayo yote, bado watu hawaitaki DIT au MUST, wanaitaka UDSM
 
Hivi ni kumbee? Nilikua sijui hili aiseee!
Umenisanua hapa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…