Leo nimekumbuka historia hii kama kumbukumbu:
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam almaarufu kama UDSM kilianzishwa mwaka 1961 kikiwa na kitivo kimoja tu cha Sheria. Kilianzia Lumumba na sasa Mwalimu Julius Nyerere Mlimani Campus kikiwa na Koleji na Shule Kuu mbalimbali.
Tangu kuanzishwa kwake,Kitivo cha Sheria kimetoa wahitimu wanne tu waliokuwa na ufaulu wa Daraja la Kwanza(yaani First Class-GPA ya 4.4 hadi 5.0).
Hao ni Dr.Ringo William Tenga,Prof. Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi, Dr.Asha-Rose Mtengeti Migiro na Prof. Hamudi Ismail Majamba. Hawa wanastahili sifa.Wanastahili kuitwa 'the Big Four'.Tangu mwaka 1992,hakukuwa na Daraja la kwanza lingine.
Wengine tulijaribu lakini tukashindwa.Tukaishia na Daraja la Pili la Juu (Upper Second Class). Ikumbukwe kuwa,Kitivo cha Sheria ndicho kinachochukua wanafunzi wanaofaulu zaidi,'the Cream of the Nation' kwa masomo ya sanaa(lakini kwasasa TCU wanaleta hata daraja la pili).
Juhudi ziongezwe kwa wengine kupata Daraja la Kwanza kitivoni hapo.Wapo watakaoweza. Wajiunge na wastahili hao. Mazingira ya kujisomea UDSM yanaboreshwa kila kukicha. Inawezekana hata kwa wengine.
Huyu jamaa vp,inferiority au? na hapo UDSM mazingira yaliyoboreshwa ni yapi?tafuta tafsiri sahihi ya mazingira bora ya elimu, acha politics na kusifia ujinga.akuna maboresho yeyote ukizingatia karne tuliyopo na dunia ya kiutandawazi. Swala la perfomance ni pana linaanzia kwenye malezi na sio selection au TCU.
MImi thina mengi thana ila mpaka leo ninajutia kimbelembele changu cha kuthoma UD miaka hiyo. The college is so outmoded, si mshauri mtu akasome pale hususan katika dunia ya leo yenye vyuo kibao tena vyenye contemporary programmes, kuliko hizo zao za kizee. UDSM is full of Drama, i hate it and i will always hate UDSM, samahanini lakini!
Kweli kabisa. Mazingira ya UDSM ni mabaya. Kwanza ni pachafu pachafu, pachakavu, na kuna upungufu wa vifaa.
ha ha ha ha ha ze best of the Best Mlimani..ha ha ha ha ha ha ha
Wewe acha sifa za kizamani, UDSM sio best of the best tena siku hizi! UDSM imebaki kuwabania tu wanafunzi, wanapofika kwenye soko la ajira ambalo lina zingatia GPAs wanapata tabu kweli kweli! maana wapo wengine kutoka kwenye vyuo vingine wana GPAs kubwa kweli! though katika uelewa wa mambo graduates wa UDSM wapo kamili si mchezo kama mimi hapa, samahani kwa kujisifia kidogo, lakini ndio hivo soko la ajira linavotaka GPAs then baadae wanakuja kuevaluate uwezo wa mtu so wenye lower Performances wanaachwa zinapofanyika shortlist though kiukweli wanakuwa ni wazuri sana.
Haya ukija kwenye suala la scholarship ndio kabisa most of them zinazingatia GPA so asilimia kubwa ya wanafunzi wa UDSM huishia kuziona tu then hawana la kufanya huku wenzao wa vyuo vingine wakifanikisha mambo yao kiulaini, maana scholarship zinapokuja hazijali wewe ulisoma wapi wala hawajui kama UDSM wanawabana wanafunzi wao na kwamba mwanafunzi anaweza kuwa na GPA ndogo ila anauelewa mzuri wa mambo! wao hawajui kuhusu hilo. may be utaishia kuwasimulia marafiki zako tu kuhusu uwezo wako na kiwango chako cha ufaulu.
Pengine imefika wakati kutoka na mazingira magumu yakiusomaji wanayoyapitia pamoja na na aina ya wahadhiri waliopo hapo UDSM, wanafunzi waliosoma hao wapewe special treatment hususan kwenye masuala ya ajira kama zilivyo taaluma nyingine ngumu, mfano mzuri ni fani ya udaktari, kutokana na ugumu wake hata scholarships zinapotoka hazihitaji vigezo kama first class au upper second class kwani ni vigumu sana kufikia madaraja hayo.
Lakini kiukweli wanafunzi wengi wa UDSM wanateseka sana huku kwenye dunia ya ukweli, mpaka inafika hatua mtu anajuta kwa nini alisoma maana akitazama wenzake waliosoma waliosoma vyuo vingine kiulaini wanafanikisha mambo yao kwa urahisi.
So wewe kama ni muhadhiri wa UDSM na umesoma ujumbe huu hebu wafikishie wenzako wote basi na uwaambie kuwamnawatesa vijana wenu huku kwenye ulimwengu wa ajira! na ikiwezekana mbadili mtazamo wenu! sio kila mtu anayesoma hapo anataka kuwa Tutorial Assistant wengine wana malengo yao tofauti so msiwabanie!
Hizo grade ni number tu, ila kwenye tasnia ya sheria tanzania hakuna na itachukua muda mrefu kuwapata kama wafuatao, James Mwalusanya (RIP), Kawa Lugakingira (RIP), Buxton Chipeta, Dan Mapigano, wote 4 walikuwa majaji. Prof. Maina Chris Peter, Twaha Ulimwengu (General Ulimwengu) Tundu Lissu, na Halima Mdee, hao uliowataja na first class zao ni sawa na Sofia Simba na masters yake ya Law japo hawezi kuongea sentence 2 za kiingereza
Hivi hiyo sheria ina ugumu kiasi gani hadi watu wasifaulu na first class honors hapo UDSM?
Haswa ndio maana kila kukicha tunawakazania watoto wetu kwenda shule.
kozi ngumu duniani katika za sanaa ya kwanza ni sheria na kwa sayansi ya kwanza ni engineering
Tena sheria hata chini ya mti unafundisha. Unachohitaji ni mitabu yako.
It's not like you need a very sophisticated lab or something.
Tumebaki kukariri kwamba prestigious careers = lawyers and doctors, wakati Bill Gates a dropout kawezesha mambo kwenye medicine ambayo madaktari wachache wanaweza ku accomplish.
And I am not talking about his software tentacles!
Hapo umenena mkuu,suala ni application hivyo vyeti ni mbwembwe tu!umenikumbusha yule mama aliyekuwa akiomba kura bungeni"ee my daily bread is engineering"