UDOM madai ya kuwazika yasiyotekelezeka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

UDOM madai ya kuwazika yasiyotekelezeka

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Candid Scope, Apr 28, 2011.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Apr 28, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Madai ya Chuo Kikuu cha Dodoma naweza kusema ni sawa mafisadi wanaotafuta njia za mkato kujinufaisha katika maisha yao. Haiingii akilini mwangu na sioni msukumo wa kudai kila mwanachuo apate laptop computer na kama kuna aliyewaahidia ni itikadi za siasa za kufikirika na wala si za kutekelezeka.

  Ningesoma shule na chuo nchini Tanzania tu ningehadaika kwamba labda hayo madai ni ya msingi kwa wanachuo. Lakini uzoefu wangu kitaifa na kimataifa jinsi mfumo wa mahitaji ya kielimu vyuoni hilo la Chuo Kikuu cha Dodoma ni jipya na la pekee kabisa. Labda kuna kitu kingine nyuma yake, lakini kama dai la msingi laptop computer ni hadithi ya kufikirika isiyotekelezeka.

  Vyuo vyote duniani hata katika mataifa tajiri kunakuwa na computer laboratory ambayo ni huru kwa kila mwanafunzi kutumia. Tena katika mataifa tajiri gharama za uendeshaji laboratory vyuoni huingizwa katika gharama za ada ya chuo na zinaonyeshwa wazi katika mchanganua wa general exp. and credit hour tuition fee. Mwanachuo aingiapo computer lab anakuwa na kitambulisho kinachomruhusu kutumia computer lab maana yake amelipia fee, kama hakulipia computer lab hakuna kitambulisho cha kumhalalisha kuingia computer lab. Hali kama hiyo Tanzania tungewapiga mawe viongozi.

  Mwanafunzi binafsi kuwa na computer ni jukumu la mwanafunzi mwenyewe, mlezi au mzazi wake ndio wenye kubeba gharama, na wala sio chuo. Sasa hilo la Chuo Kikuu cha Dodoma kudai kila mwanafunzi apewe laptop computer na chuo au serikali ni kali ya mwaka na ni mzigo ambao chuo au serikali haiwezi kubeba gharama hizo.

  Kuna mambo ya msingi ya kusikiliza na kukubali, lakini katika hili hapana, ni nje kabisa ya taratibu ya vyuo, na ni jambo la kuwazika kwa wenye upeo mdogo hitaji lisilotekelezeka. Bora waangalie mambo mengine ya msingi badala ya kupoteza muda na kudai personal laptop computer kutoka serikalini. Wanapoteza muda wao wa kusoma ndio maana baadaye tutapata viongozi vilaza kama tunavyoshuhudia siku hizi.
   
 2. LINCOLINMTZA

  LINCOLINMTZA JF-Expert Member

  #2
  Apr 28, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 1,640
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Siasa zimeingia kila idara sasa hivi hata uhalisi wa mambo hauangaliwi kabisa. Je tutafika?
   
 3. kingxvi

  kingxvi JF-Expert Member

  #3
  Apr 28, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 883
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  wewe hujui unachowaza ni jambo ambalo waliahidiwa na bodi ya mikopo kwaajiri ya special faculty kila mwanafunzi wa college ya informatic laki 8 kwaajiri ya kununua vifaa vya kujifunzia kwa vitendo na mbona walipogoma mara ya kwanza majina yalitoka kila mwanafunzi apewe elfu 50 ? Waligoma kuchukua maana ni tofauti na makubaliano na bodi wangechukua vipi hela pungufu! Inavyoonekana hela imechakachuliwa
   
 4. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #4
  Apr 28, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,284
  Likes Received: 19,437
  Trophy Points: 280
  mkuu Candid Scope , umesema vyema , na mimi toka post ya kwanza ya hawa vijana kusema kuwa wameahidiwa laptop na ndio maana wanagoma mimi niliwaambia wazi wazi kabisa kuwa in capitalist economy no free luch, na kwamba hayo madai yao ni ya kufikirika tu na serikali kama ya Tanzania haiwezi na haitaweza kuwapa laptop , wakawa wanajibu kwa jazba , but wa kulaumia hapa ni huyo mtoa ahadi aliyewaahidi wasomi wetu laptop na wao wakaamini
   
 5. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #5
  Apr 28, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Utafiti wangu umefikia kugundua wengi wa wanachuo walio na computer au simu hutumia gharama kubwa ya internet katika social activities badala ya malengo ya kutumia kwa ajili ya elimu.
  Facebook ilivyowateka wanachuo wengi huwezi kuamini ni lini wanatuliza akili kuibua masomo toka mitandaoni.
   
 6. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #6
  Apr 28, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Kama Wizara ya Elimu ingekuwa makini katika kutatua matatizo sugu ya elimu ya msingi na vyuo nchini, bora ingejitahidi kuboresha mazingira ya madarasa, lab na vifaa vya elimu vinavyoadilimika kuliko wanafunzi wanavyopata elimu kinadharia bila vitendo, hayo niko pamoja na wanavyuo kudai maboresho ya haraka.

  Kila chuo kiwe na lab za uhakika katika masomo na computer, hivyo wanafunzi watapata elimu ya uhakika kinadharia na kivitendo. Utaratibu mzuri ukiwapo chuoni na hakika hata computer lab zilizopo zinaweza wasaidia wanafunzi vizuri.

  Ninachopendekeza mwanachuo asiwe na tight schedule ya siku nzima, bali mfumo wa kupishanisha vipindi ili wasigombaniane computer lab.
  Hata matajiri vyuo vyao havipo na lab computer za kutosheleza wanafunzi wapate kwa mkupuo, bali upishanishaji wa vipindi madarasani na kuwapa muda kuwa free wakati wengine wako madarasani hutoa fulsa nzuri ya kupata nafasi kwenye computer lab.

  Serikali pia ijaribu kuongeza zaidi kitengo cha computer reserch kwanye maktaba za mikoa na wilaya ambako wanafunzi wengi ndiko wanakofanyia uainishi kivitendo, kwa hiyo wasio na uwezo wa kuwa na computer zao maktaba ingekuwa ukombozi wao, kwani hata kama kutakuwa na kulipia kidogo ni nafuu kuliko kutumia commercial computer cafe.

   
 7. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #7
  Apr 28, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  huyo aliyewahadi na ninyi mliosadi hiyo ahadi na kuanzisha migomo kudai hiyo ahadi wote ni wanyonyaji kwa taifa ili.
  hakuna nchi inayotumia pesa yake vibaya kama TANZANIA, kwa uchumi huu inaingia akili kweli hii ahadi kuwa kipaumbele kwa taifa lisilo na zahanati za kutosha maana nina hakika hao wapewe laptop wasipewe wanakua mabomu tu, maana wanaonyesha awajui wanachosoma na hawana mbinu na kujifunza ila ni masharobaro tu hawa
  , lakini pia hawa WENZETU WA IT NA MA COMPUTER TECHNOLOGY wa UDOM wanatuambie ni lini walifanya utafiti wa kutosha na kuona kwamba hizo laptop za lakini 8 zinaweza kukidhi mahitaji ya mwanafunzi serious wa IT?, au wanazitaka kwa ajili ya kufacebook.
  PC kamwe haiwezi kumsaidi mtu yeyote kusoma kwa vitendo kama APPLICATION (software, au soft material) husika hazipatikani hapo chuoni,
  hii ndio kesi kubwa maana hapa Tanzania application ni mgogoro, vyuo vyetu bado vinafundisha kwa njia za kijima na pc hazina software za kutosha ,wao wadai kuwe na pc za kutosha vyuoni na sio kujaribu kuleta usharobaro kwenye pesa ya umma,
  lakini pia serikali huu ni wakati wa kujali taaluma zote na sio kujifanya tunajali sana masomo ya sayansi na kuwapa kisogo wengine matokeo yake ndio haya watu wanapata ajira wanamtukuza aliyewapa hiyo ajira badala ya kulitumikia taifa, maana walishajengewa misingi kwamba walichosoma sio kitu mihimu katika jamii.
   
 8. Viper

  Viper JF-Expert Member

  #8
  Apr 28, 2011
  Joined: Dec 21, 2007
  Messages: 3,665
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Kiongozi umenena na kumaliza kabisa... sikujuwa kama mgomo wao ilikuwa ni personal laptops .. walizo ahidiwa na MWANASIASA ... Tehtehtehe
   
 9. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #9
  Apr 28, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,970
  Likes Received: 2,965
  Trophy Points: 280
  Chuo gani Tanzania wanatoa kias hicho?????. Ni wapumbavu, badala walilie waalimu wanalalamikia vitu vya kusadikika?????!!!!!!!!!!!!. Hawawezi kufikiria wanadanganywa kama watoto.
   
 10. Mhadzabe

  Mhadzabe JF-Expert Member

  #10
  Apr 28, 2011
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 1,643
  Likes Received: 710
  Trophy Points: 280
  Navyofahamu mimi kauli ya Waziri mkuu ni kauli ya serikali, kama aliahidi ni jukumu la serikali kutimiza. Sioni kama imekuwa dhambi kwa wana chuo kudai walicho ahidiwa na serikali walioichagua. Laptop kitu gani kwa M90 za zaidi ya wabunge mia3? Hivi unajua hata zilizopo comp lab hazifanyi kazi afu eti unasoma comp sc? Kudai hayo ni dhambi kweli?
   
 11. Mhadzabe

  Mhadzabe JF-Expert Member

  #11
  Apr 28, 2011
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 1,643
  Likes Received: 710
  Trophy Points: 280
  Hata katika hizo so called social activities zinatoa elimu pia? Elimu haipatikani kwa lectures na seminars tu kama unavyo fikiri. Nadhani hata hapa kua JF unapata elimu pia tena nadhani iliyo bora zaidi hata kuliko unazopewa na na ma T.A au Lecturers
   
 12. Sooth

  Sooth JF-Expert Member

  #12
  Apr 29, 2011
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 3,773
  Likes Received: 4,494
  Trophy Points: 280
  Kuna taarifa kuwa Bodi ya mikopo ilikuwa inatoa karibu milioni 20 kwa ajili ya kiti cha kung'olea meno kwa wanafunzi wa meno (dentists) Muhimbili ili wakimaliza wakajiajiri. Hzo pesa zilikuwa zinafika chuo lakini zinapotelea hewani, wanafunzi hawapewi. Tatizo ni kukosekana kwa uwazi (transparency) ktk taasisi nyingi za serikali.

  Ni kweli nchi za ulaya wanafunzi hawanunuliwi laptop, lakini mazingira yapo tofauti. Huku kwetu wanafunzi wengi wa IT wanakuja kutumia kompyuta kwa mara ya kwanza akiwa chuoni, tena aombe Mungu chuo kiwe na kompyuta za kutosha. Ulaya watu wengi wanazaliwa kompyuta na internet connection ipo nyumbani. Net ya uhakika muda wote. Ndio maana ulaya kuna 'teenager hackers'- kompyuta wanacheza nazo kila siku. Huku kwetu, until recently, kompyuta ilikuwa mama mkwe hata kwa wanafunzi wa IT.

  Kama kweli tumedhamiria kuboresha kiwango cha elimu yetu, sio dhambi wala ajabu mtu kununuliwa laptop ya laki 8. Prof. Luhanga aliwahi kuahidi kompyuta kwa kila graduate UDSM, ingawa haikutekelezwa, ilikuwa ndoto nzuri. Rwanda wanagawa laptop (simple laptop) kwa kila mtoto.

  Kiujumla suala la faculty requirements ni vichekesho, maana kuna chuo watu walikuwa wananunuliwa tai (elfu 50), jiulize kama tai inamchango wa moja kwa moja kwa mwanafunzi. Miaka ya 2002-2006 (engineering-udsm) walikuwa wananunuliwa shati, buti, ovaroli, kifaa cha kuchorea, vitu ambavyo ukiuliza bei waliyonunuliwa unaweza ukashangaa.
   
 13. Sooth

  Sooth JF-Expert Member

  #13
  Apr 29, 2011
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 3,773
  Likes Received: 4,494
  Trophy Points: 280

  Maoni kama haya yanaturudisha nyuma kiteknolojia, ni kama kuua panya kwa risasi. UDSM waliwahi ku-restrict internet access (like 2yrs ago) toka saa 2:00 asbh mpaka saa 10:00 jioni kwasababu wafanyakazi(hasa admnistrative aka supportive staff) walikuwa wanachat na kutumia yahoo muda wa kazi. Huu ulikuwa ni uamuzi mbaya sana hasa kwa academic institution. Hela zenyewe za kununulia vitabu librali hatuna, tumebaki na vitabu vya mwaka 66. Kwanini uzuie intaneti access ambapo mwalimu na wanafunzi ataweza kudownload vitabu (latest), papers na lecture notes?

  Tunatumia muda mwingi (social media) kwasababu ni vitu vipya kwetu (hata ulaya vijana hawabanduki kwenye social networks-fcbk,twitter etc), naamini with time mtu anazoea na kuendelea na mambo mengine. Mbona chat service sio maarufu kama ilivyokuwa hapo awali? Lakini hata kutumia fcbk na social media zingne sio kitu kibaya. Watz wengi wameshawishika kutumia kompyuta kwa sababu ya social networks. Leo Jose Mara wa Kimara (Mwanamziki) ana blog yake ambayo anaitumia kwa biashara. Huyu ni aina ya watu ambao ungedhani asingesumbuka sana na mambo ya kompyuta, lakini kwa kuelewa nguvu yake, amejiunga. Naamini kuna watz wengi wamejifunza kutumia kompyuta sababu ya fcbk. Kujua kutumia kompyuta ni muhimu sana kwa soko la ajira la sasa.
   
 14. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #14
  Apr 29, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Ngondya kama umefika ulaya unajua dhahiri kuna wenye nacho na wasicho nacho, la sivyo jaribu kutembelea ndio utaelewa kwamba si watoto wote wanaochezea computer home ila ni wale wa class ya juu na wenye kipato kizuri vinginevyo ni malala hoi wa kutupwa. Ukifika Airport usijeshangaa wamejipanga watu kukuomba pennies wapate kununulia McChicken huko McDonalds. Huenda kama una akili nzuri ya utundu na ugunduzi bongo afadhali kuna uwezekano mkubwa kuliko ulaya ukakofananisha.

  Tusidanganye watu kuwa watu wa ulaya kila mtu ana computer na watoto wanachezea computer toka utotoni. Kuna wenye uwezo ambao watoto wanachezea electronic stuff tangu utotoni. Kula maskini wa kutupwa watoto wao hutegemea computer za mashuleni, na baada ya shule wanaenda public library huko kuna vitengo vya computer za watoto na za watu wazima.

  Hapo juu nimedokeza hilo kwamba serikali ijaribu kubuni upanuaji wa Maktaba ya mkoa na wilaya ambapo kungeongezwa computer lab for public use, ambazo zitasaidia wale wasio na uwezo wa kuwa nazo. Maana umilikaji wa computer nao ni gharama hasa kama unataka kuwa na network, bora kuchangia kidogo public kadiri uwezo unavyoruhusu.

  Tuachana na nadharia, tunachotakiwa kufanya ni upembuzi na ukomavu wa kupima mazingira yetu, uchumi wetu, familia zetu, nk. Kwa mtazamo huo kila mmoja wetu jibu analo.l
   
 15. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #15
  Apr 29, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,284
  Likes Received: 19,437
  Trophy Points: 280
  jinunulie sasa
   
 16. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #16
  Apr 29, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,284
  Likes Received: 19,437
  Trophy Points: 280
  pesa hakuna imeenda kwenye bajeti ya vitafunio under ccm/ any more qns?
   
 17. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #17
  Apr 29, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Kipi ni priority kwako, madawati, text books and science lab or laptop computers?
  Vyuo vingi havina vifaa vya kutosha vya science lab, kuna upungufu mkubwa mno wa text books, kuna ukame kubwa wa wahadhiri, sasa wanachuo wanachoona muhimu kwao kwanza ni laptop. Tufahamu kwanza wengi wa wanavyuo ni bado watoto ambao hawajafikiria vipaumbele kwanza, na tunatakiwa kuwaelimisha.

  Kitu cha kwanza kuwaelimisha wanachuo hawa ni ustahimilivu kwani hata siku moja chuoni hutajisikia ni peponi, ila peponi utatengeneza mwenyewe ukishahitimu utakapopambana na ulimwengu baada ya kuingiamo. Kwa sasa ni rahisi kumnyoshea kidole fulani, lakini ukishaanza mapambano baada ya kuhitimu huna wa kumnyoshea kidole, ila kuichukulia hali halisi ilivyo au unapambana na hali halisi ujikwamue.
   
 18. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #18
  Apr 29, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,284
  Likes Received: 19,437
  Trophy Points: 280
  kwa hiyo tukiWAununulia laptop zenye hard disc 20GB na 125 MB of RAM mtazichukua?? NYIE NI MNATAKA BORA LAPTOP AU ELIMU BORA?
   
 19. p

  papachu Member

  #19
  Apr 29, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  unajua usilo lijua ni sawa na usiku wa giza ungeonana na wachuo na kuwauliza madai yao ungewaonea huruma,kwani hizo pesa walisha ingia mkataba na bodi ya mikopo na mwisho wa siku watazilipa.jiuiliza 50000 utanunua nini chuo kina computer 50 wanafunzi 12000.madai makubwa si lapotop bali kuna mengine kama akuna walimu wanasoma kwa nadharia kuliko vitendo,wanaosoma enginnering udom ni sawa na yule anyesoma social sceince kwani awanatofauti katika njia za ufundishaji.ukitaka kujua matatizo ya hawa wanafunzi fika hapo chuoni utayajua mengi
   
 20. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #20
  Apr 29, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Kipa umbele cha maandamano ni laptop computer, na hilo ndio nisilokubaliana nalo kwa vile sio priority nikilinganisha na mengine niliyoyaainisha hapo juu.
  Kwa nchi maskini kama Tanzania kiashi cha computer walizonazo University of Dodoma kinaridhisha kwa idadi ya wanafunzi waliyonayo, kinachotakiwa ni utaratibu mzuri kama nilivyoainisha hapo nyuma. Vyuo vya Tanzania ratiba ni kama za shule za msingi, wanachuo wako madarasani siku nzima na hawapishanishwi madarasa kwa uwiano ili kuwapa fursa wengine kutumia computer lab, na wapatapo mapumziko ni wanafunzi waote hapo ndio kasheshe kumbaniana computer.

  Uongozi wa vyuo ubuni mbinu kuendesha vyuo na ratiba za vipindi darasani kisayansi, si mradi watu wanaingia madarasani bila kufikiria zaidi juu ya ratiba ya research na labs pract.

  Chuo nilichowahi kusoma nje ya nchi ambacho ni cha Serikali kulikuwa na idadi kubwa zaidi ya wanachuo kuliko Dodoma, na computer lab ilikuwa na idadi kama hiyo lakini ilitutosheleza kwa vile kulikuwa na utaratibu mzuri wa ratiba ya darasani na matumizi ya lab kwa mpangilio. Hilo tunahitaji wazungu waje kutufundisha wakati chuoni hapo kuna wahadhiri walipitia vyuo kama nilikopitia na wanajua nini wangefanya kuboresha matumizi ya computer lab.
   
Loading...