Safari hii naona mmeamua kufuata kanuni mnaozijua ninyi maana kila tulichoaminishwa hamfanyi.
1. Mwanafunzi wa div 1 ya A zote anakosa scholarship ya SAMIA na mkopo hakupata. Sasa hizo kauli zenu vipi?
2. Mwanachuo anasomea " degree za kipaumbele" anakosa mkopo kwa 0%. Hata mia. Udaktari, ualimu nk. Sasa mnawapa akina nani?
3. Muelewe wapo wanafunzi wanaosomeshwa na wafadhili kwa kiwango cha sekondari. Ninyi mkiona tu jina la shule ya private.. hakuna mkopo.
4. Wengine wamesoma sekondari za kata mwanzo mwisho. Nao hakuna mkopo. Sasa mnatumia vigezo gani?
5. Mnapokataa maombi ya mkopo wa mwanafunzi...mpeni sababu ya kukataliwa badala ya kukaa kimya kama hamjapokea maombi. Kama sababu zenu ni za msingi zitajeni ili uwe msingi wa kukata rufaa.
6. Sasa mwanafunzi anakataje rufaa wakati hamjampa sababu ya kukataliwa ombi lake la mkopo?
7. Tunahitaji uwazi kwenye bodi..majina yawekwe wazi kwenye ukurasa wa bodi tujue nani kapewa. Hili ni muhimu kwani mwanafunzi anaweza pewa mkopo na chuo kikakaa kimya au akamwambia mzazi hajapewa mkopo. Ndo maana vyuoni wanafunzi wana matumizi makubwa mpaka unashangaa.
Siri ya nini?
8. Mwanafunzi anapopewa mkopo, wadhamini wake wajulishwe na kiasi cha mkopo kila mwaka badala ya kuwahusisha wadhamini wakati wa kudai deni la mkopo....huu ni udhaifu wa kimfumo.