Leo katika ibaada ya ijumaa katika msikiti mkuu wa igunga mjini shekhe ama mtoa mawaidha amesema chadema na wakristo ni makafiri. Katika mawaidha hayo shekhe huyo alisikika kupitia spika za mskitini (Public annoucement system) akisema chadema ni chama cha kidi kwa sababu ya kumdharirisha mkuu wa wilaya ambaye ni mwislam. nami ni kiwa eneo ka msikitini nilisikia maneno hayo ya shekhe. Kweli shekhe katugawa wana igunga. Anadai kwa mwislam yeyote atakaye chagua chadema atalaaniwa. Baada ya ibaada wapo baadhi ya waislam wamechukizwa na hotuba ya shekhe huyo. Mbaya yaidi waislam wanashindwa kuelewa kama kuchagua chadema ni dhambi kwa kauli ya shekhe! je wachague chama kipi? Kwani katika vyama venye nguvu hapa ni chadema, ccm na cuf. Wagombea wote kupitia vyama hivyo wote ni wakristo. Kuna mgombea mmoja tu kutoka chama kimoja cha UDPD ambacho hakina mashiko kabisa hapa igunga hata kampeni bado hakijazindua. Sijui huu udini utatupekeka wapi? haya ni ya kweli nimeyackia mwenyewe na kama una dungu yako hapa igunga ambaye anafuatilia siasa kwa ukaribu please jaribu kumuuliza. Tunaomba dua zenu uchaguzi huu umalizike kwa amani.