MIKURUPUKO YA BAKWATA NA USHABIKI WAKE KISIASA NCHINI HUENDA UKAZAA TAASISI NYINGINE IMARA ZAIDI KUJUMUISHA WAISLAMU WA MATABAKA YOTE NCHINI
Wala haikua lazima kiasi hicho kwa taasisi hii ya BAKWATA kudhaalilisha Uislamu nchini kwa kukurupukia tu matukio bila hata kuyatthmini kiundani kwanza.
Kuna uwezekano Wanaharakati maarufu kama Sheikh Ponda Issa Ponda na wengine wengi tu wakapinga vikali mno hii taabia ya hivi karibuni ya baadhi ya BAKWATA kuligeuza KIMBILIO LA CCM wakati wa shida za kukataliwa kisiasa.
BAKWATA na mikurupuko yake ya kuaibisha Waislamu SAFI nchini kama vile kwa huyu Mzee wa Kanisa Katoloki pale Wazo-Tegeta, Mama Fatuma Joseph Kimario, huenda ikageuka BOMU LA HATARI sana kuliangamiza taasisi hii tuliokua tukiiheshimu saana nchini.
Kwa kweli pengine taasisi nyingine ya maana zaidi na yenye Uwakilishi wa kweli wa WAUMINI WA KIISLAMU (wala si CCM) nchini huenda ikaibuka na kuungwa mkono kuchukua nafasi yake hivi karibuni.