Udini wa kutisha UDOM!

Status
Not open for further replies.
Kyatsavapi,Semenya,

..binafsi nadhani shule au hospitali ikiwa na huduma nzuri na za viwango watu hawatajali inamilikiwa na madhehebu gani.

..binafsi nafahamu Waislamu safi tu wamesomesha watoto wao shule za Kanisa.

..pia nafahamu sasa hivi kuna shule moja ya Waislamu inafanya vizuri na wananchi wa kila dhehebu wanapigana vikumbo kuandikisha watoto wao hapo.
 
Bnhai hebu nipe mwanga kidogo hivi hayo machapisho (publications) matatu yanayomtoa mtu mwenye masters kwenye u-assistant lecturer na kuwa lecturer wanaya-assess vipi? Maana kuna wakati unaweza ukatoa chapisho ukiwa na co-authors wengine 2 yaani mko watu au zaidi. Asante.
Swali zuri.
Hili ndio tatizo la Tanzania sasa hivi na watu wengi tumejaribu kulipigia kelele lakini inaonekana watu wanajifanya hawasikii. Hapo Tanzania kama utaandika peke yako basi unapewa credit moja. Mkiwa watatu hiyo moja inagawanywa kwa tatu kwa hiyo unajikuta unapata one third. To me, I dont see if this is realistic. Research inahitajika sharing of ideas na ndio watu mnatengeza kazi bora zaidi. Kwa Ulaya kinachofanyika ni kwamba, jarida utakalochapisha ndio linaonyesha wewe ni nani. Kama umechapisha kwenye star 4 au vinginevyo. Na wao hasa vyuo vyao vinakuwa ranked kutokana na wapi wanachapisha.
Lakini hapo nyumbani mtu anaweza kuandika kitu cha ajabu na usipokaa sawa anaita publications tena kwenye kijarida anakuwa promoted.
 
Kyatsavapi,Semenya,

..binafsi nadhani shule au hospitali ikiwa na huduma nzuri na za viwango watu hawatajali inamilikiwa na madhehebu gani.

..binafsi nafahamu Waislamu safi tu wamesomesha watoto wao shule za Kanisa.

..pia nafahamu sasa hivi kuna shule moja ya Waislamu inafanya vizuri na wananchi wa kila dhehebu wanapigana vikumbo kuandikisha watoto wao hapo.
kaka melielezea hilo kwa mchangiaji mmoja kuwa, sababu ya shule za wahindi kuwa na wahindi tu, ni mambo mawili kwanza wa TZ wenyewe ni wachache wanaopeleka watoto wao kwa shule wahindi coz of kipato au maranyingine hulka...na hivyohivyo kwenye vyuo vya taasis ya kidini hulka na mgongano wa mawazo potof ya kidini..ila nikamwekea angalizo kuwa...kama shule ikiwa inakiwango bora atawaona tu watanzania wakienda shule za kihindi mfani ni shaaban robert na mzizima zamani, na sasa feza boys ya Mbezi
 
From UDOM website:
Chancellor :BW Mkapa
Chairman of University Council : Mohammed Ghalib Bilal
Vice Chancellor : Prof. Idris Kikula
Deputy VC Planning,Finance
Administration : Prof Shaaban Mlacha

Tutajaza!!!!!!

waungwana ili kuwa wakweli na wawazi tujaribu ku compare na UCLAS na UDSM na MUCHs.
Chancellor :
Chairman of University Council :
Vice Chancellor : Prof.
Deputy VC Planning,Finance
Administration :

sasa tukijua kutoka hivyo vyuo vitatu vikuu ndipo tutapoweza sema kuna UDINI au la
 
Hatuhitaji kucompare tulihitaji facts kwa mleta mada naona amepotea. Haya mengine hayajengi, tuna mambo mengi zaidi ya kuanza kufuatilia dini za viongozi wa taasisi
 
Comparison yako haitaleta ufumbuzi wowote ule kwa sababu watu wa dini na makabila tofauti.

Kuna kipindi hapa hapa JF zilizolewa hoja kuwa Taasisi ya computer pale mlimani imejaa waHaya.
 
Hatuhitaji kucompare tulihitaji facts kwa mleta mada naona amepotea. Haya mengine hayajengi, tuna mambo mengi zaidi ya kuanza kufuatilia dini za viongozi wa taasisi

Namsupport mtoa comment hapa juu tukianza na ubishi wa udini tutakuja wa ukabila, tutakuja urangi mwisho wa siku utabakia wewe peke yako mtoa mada tuache majungu na malawama tufanye kazi
 
Hatuhitaji kucompare tulihitaji facts kwa mleta mada naona amepotea. Haya mengine hayajengi, tuna mambo mengi zaidi ya kuanza kufuatilia dini za viongozi wa taasisi
aisee ni moja ya majibu mazuri kabisa
hongera sana
inaonekana unabusara nyingi kaka
tunahitaji watu wenye mawazo kama yako na si kama ya mtoa mada...
u impressed me
thanks sana kaka
 
Jamani naomba kuelimishwa hapa huyu Chancellor B.W.Mkapa ana marupurupu na mshahara hapo chuoni?
mkapa cheo chake ni cha heshima yeye anakuja kwenye awards ceremony, hajui hata nini kinaendelea

mtendaji mkuu ni vice chancellor- kwa hiyo malalamiko yote yapelekwe kwa vice chancello
 
mkuu acha kuwa mdini, hata kama ni kodi zetu kwani ikiwa muslim university kuna tatizo kaka
afu mekwambia uchunguze na st joseph st agustin na st jones mbona navyo vina idadi ya wakristo wengi, achilia mbali chuo cha kikristo cha tumaini ya Lushoto...me naona hauna hoja kaka..hivyo vyuo vimejengwa kwaajili ya kitu flani na si public university kama SUA< MU<UDSM au UDOM....
unapokataa kuwa shule ya kuhindi watanzania wengi hawawezi kuaford nakushangaa sana na nakuona ni mnafki mkubwa sana..wa TZ wengi hawana uwezo wa kusoma shule za wahindi, au kwaajili unadanganyika na wafrica shaaban robert na mzizima na feza...mbona nasisi wahindi hawaji shule zetu..kuna vitu ambavyo vipi duniani haviwezi kuwa sawa kaka...tuache FITNA za kijainga...
DONT PANIC Mzee!
Mimi si mdimi wala mbaguzi, na nasikitishwa na discrimintion hiyo popote duniani.
Arguments zako as usual are shallow.
Historically kutoendelezwa kwa sehemu nyingine katika nchi hii ni kutokana na muitikio wa wananchi wake katika suala la elimu(siyoilmu!)
Si jambo la kushangaza kuwa wenzetu waarabu tunaowahehimu sana katika suala la elimu(elimu dunia), hwakuwaendeleza sana raia wa sehemu walizo kaa.
Tofauti na sehemu nyingine ambazo elimu iligombaniwa.
Siyo siri kuwa Kisarawe,Kilwa,Bagamoyo,Dar es salaam, sehemu za Tabora, kigoma na nyinge nyingi zilizokaliwa na waarabu hazikujiendeleza sana kielimu(elimu dunia).Na hii haina maana kwamba sehemu nyingine ziko mbali kielimu ,la hasha.
Sasa mtu unapo taka kufukia mashimo haya ya kimaendeleo kwa kufanya mabadiliko ambayo si endelevu, kukwama ni lazima.
Ili kuendeleza sehemu hizi lazima tuanzie shule za msingi, sekondari hadi vyuo vikuu.Must start from the grass roots.
Cha kusikitisha bado kuna sehemu nyingi nchini mabapo ni lazima umtishie kifungo mzazi ili ampeleke mwanae shuleni!!!!
Sehmu hizo mkuu Semenya unazifahamu fika!
Sasa ukianza kutupiga kodi ili dini fulani wacatch up na wae at par, thats superficial.
Sasa kwa vile vyo vya kikiristo ni vingi sana kazi kwako bwana Semenye ni wewe na wenzako kupata na kuanzisha vyuo vingi tena sana katika sehemu hizo, tena kwa msaada wa wezetu wenye mafuta mingi uarabuni-wasilete tende tu!
 
kaka we majibu yko ndo shalo
na inaonekana hauna uwezo mkubwa sana wa kufikiri
kwanza muslim university haipewi ruzuku na serikali
ni vyuo vya serikali tu vinavyopewa ruzuku
ukisema majengo hamna chuo cha binafsi au private kilichojenga maeneo yao, yote ni yakununua, sema muslim walipewa na serikali.....ambapo hata st jones pia walipewa...after all section 4 of the land act and the village land act inasema land ni ya serikali...so si laajabu kaka.

nakubaliana nawe unaposema waarabu walishndwa kueneza elim, ila ufinyu wako wa mawazo unaonekana hapohapo, pia wazungu waliendeleza weusi kielim walipo taka kuwatumia, mfano South Africa kuna majimbo kama Limpopo na mpumalanga hawakusomesha weusi kabisa kama waarabu ambapo hawakusomesha wa Tanganyika katika hayo maeneo ulio yataja..
pili upeo wako mdogo unapojichanganya na kuona kuwa serikali imechukua hatua ya kuweka na kuendeleza kila mtu kielim kwa kuweka sheria kila mtoto aende shule rather than kuiendeleza dini moja
pia ufinyu wa mawazo yako ni pale unaposema muslim inapata kodi ya wananchi, inamaana hujui kuwa private institutions hazipewi ruzuku..tafta budget ya eli ya juu then nioneshe wapi private institution wamepewa ruzuku..

mada ilikua muslim wanachukua waislam wengi kuliko vyuo vyote nikakujibu nikakwambia umeona data za st agustin st joseph na st jones
usikurupuke kaka
labda nabishana na mtu nilie mzidi upeo kielim sina hakika, maana hapa tu inaonekana niko hatua tatu mpaka ishirini kama za ussain bolt akiwaacha na kuwagaragaza wenzie
Regards
 
mkuu napangua hoja zako mbili kama ifuatayo na kwania nzuri tu
mmoja ya wahindi kuwa shule inawahindi tupu ni kwasababu zifuatazo, moja kama ni shule ya wahindi inawezekana imeshawishi wahindi wengi kwenda, pia kama ni gharama sana watanzania wengi hawawezi ku aford, tatu kama ni mpya basi hatuijui kitaalima sana ila ikiwa inafanya vizuri wa TZ watakuja, mbona hatusemi shule za wa TZ ambazo hakuna muhindi wala waarabu

kuhusu muslim university, kile ni chuo kimewekwa kaajili ya muslims, mbona kuna shule za seminari za sekondari kama visiga na st marrian hazichukui waislam,ni kwasababu zimejengwa kwa madhumuni ya wakristo, pia nakuomba uangalie idadi ya wanafunzi wanao chukuliwa st agustin, na kile chuo cha kikristo st jones, pia anagalia na st joseph cha dar...ukiangalia wengi ni christians kama asilimia 90..

unanua ni nini, pia wananchi wakisha jua ni chuo cha kiislam au cha kikristo mtu haendi kwenye chuo imani ikiwa tofauti

so hapo kuja na kitu kipya kaka

kwa ajili watu weusi ni more than 95% of TZ population
 
nilikua namfafanulia kuwa tusilalamike tuu, pia mbona kuna hospitali na mashule mengi tu ya wahindi weusi wanasoma
kama mimi mesoma primary shule ya wahindi
inatokea kuwa shule inawahi tu, mara nyingine ndo dhumuni la hilo shule, ukizingatia wako wachache...waache wawe na shule zao.nasi tunazo zetu nyingi mpaka idadi siziju

TUFUNGGE MJADALA JAMANI MWENYE HOJA YA THREAD HII KASHINDWA KULETA USHAHIDI ACCORDINGLY...na we have to dismiss these claims forthwith.
 
mkuu napangua hoja zako mbili kama ifuatayo na kwania nzuri tu
mmoja ya wahindi kuwa shule inawahindi tupu ni kwasababu zifuatazo, moja kama ni shule ya wahindi inawezekana imeshawishi wahindi wengi kwenda, pia kama ni gharama sana watanzania wengi hawawezi ku aford, tatu kama ni mpya basi hatuijui kitaalima sana ila ikiwa inafanya vizuri wa TZ watakuja, mbona hatusemi shule za wa TZ ambazo hakuna muhindi wala waarabu

kuhusu muslim university, kile ni chuo kimewekwa kaajili ya muslims, mbona kuna shule za seminari za sekondari kama visiga na st marrian hazichukui waislam,ni kwasababu zimejengwa kwa madhumuni ya wakristo, pia nakuomba uangalie idadi ya wanafunzi wanao chukuliwa st agustin, na kile chuo cha kikristo st jones, pia anagalia na st joseph cha dar...ukiangalia wengi ni christians kama asilimia 90..

unanua ni nini, pia wananchi wakisha jua ni chuo cha kiislam au cha kikristo mtu haendi kwenye chuo imani ikiwa tofauti

so hapo kuja na kitu kipya kaka

Sidhani kama Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Morogoro hawakupewa waislamu ili kiwe cha waislamu tuu. Chuo kilipewa jumuia ya waislamu wakiendeshe kwa faida ya watanzania wote. Vyuo vinavyokuwa kwa ajili ya dini moja ni theological institutes ambazo lengo lao kutoa watu watakaohudumia katika dini hizo. Kwa hali hiyo, muislamu hawezi kupokelewa Makumira seminari maana kule wanafundisha watu wanaotarajiwa kuwa mapadiri. Sijawahi kusikia kuwa hicho Chuo Kikuu cha Morogoro lengo lake ni kutoa mashehe, ustadh, maimau au makadhi! Kwa hali hiyo kilitakiwa kuwa kwa ajili ya wote bila kujali dini yao. Hivyo hivyo kwa hizo shule za wahindi. Hawawezi wakatumbulika kisheria kama watasema kuwa asie mhindi asithubutu hata kuomba! hatujafika huko.

Hauwezi ukasema shule ni kwa ajili ya wakristu tuu halafu ukasema kuwa asilimia 90 ni wakristu. Kingekuwa cha wakristu peke yake basi hata hao asilimia kumi wasingeona ndani. Sijawahi kusikia shule ambayo inaendeshwa na kanisa ( ambayo si seminari) inayokataa wanafunzi wasio wakristu (waislamu, wahindu, mapagan, rastafarians, mabaha'i, n.k). Nimefundishwa na wamisheni na darasani walikuweko wasio wamisheni. Tofauti ni kuwa mbele ya darasa palikuwa na msalaba. Kama hilo halikusumbui ruksa. Kama vile kama hauoni tatizo kuvaa hijab ingawa ni mmisheni kwa nini ukataliwe kujiunga na shule inayoendeshwa na waislamu?

Huu ubaguzi mnaotaka kuuleta ni hatari mno. Utatufikisha pabaya maana watoto wetu hawatajuana kama tunavyojuana sisi.

Amandla.......
 
waungwana ili kuwa wakweli na wawazi tujaribu ku compare na UCLAS na UDSM na MUCHs.
Chancellor :
Chairman of University Council :
Vice Chancellor : Prof.
Deputy VC Planning,Finance
Administration :

sasa tukijua kutoka hivyo vyuo vitatu vikuu ndipo tutapoweza sema kuna UDINI au la

Kwa nini usiwaweke tuu kama walivyofanya kuhusu UDOM? Tatizo liko wapi? Watu wameishadai kuwa uongozi wa juu wote wa hivi vyuo ni wamisheni. Wawataje basi ingawa jina si ushahidi kamili.

Amandla........
 
Sidhani kama Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Morogoro hawakupewa waislamu ili kiwe cha waislamu tuu. Chuo kilipewa jumuia ya waislamu wakiendeshe kwa faida ya watanzania wote. Vyuo vinavyokuwa kwa ajili ya dini moja ni theological institutes ambazo lengo lao kutoa watu watakaohudumia katika dini hizo. Kwa hali hiyo, muislamu hawezi kupokelewa Makumira seminari maana kule wanafundisha watu wanaotarajiwa kuwa mapadiri. Sijawahi kusikia kuwa hicho Chuo Kikuu cha Morogoro lengo lake ni kutoa mashehe, ustadh, maimau au makadhi! Kwa hali hiyo kilitakiwa kuwa kwa ajili ya wote bila kujali dini yao. Hivyo hivyo kwa hizo shule za wahindi. Hawawezi wakatumbulika kisheria kama watasema kuwa asie mhindi asithubutu hata kuomba! hatujafika huko.

Hauwezi ukasema shule ni kwa ajili ya wakristu tuu halafu ukasema kuwa asilimia 90 ni wakristu. Kingekuwa cha wakristu peke yake basi hata hao asilimia kumi wasingeona ndani. Sijawahi kusikia shule ambayo inaendeshwa na kanisa ( ambayo si seminari) inayokataa wanafunzi wasio wakristu (waislamu, wahindu, mapagan, rastafarians, mabaha'i, n.k). Nimefundishwa na wamisheni na darasani walikuweko wasio wamisheni. Tofauti ni kuwa mbele ya darasa palikuwa na msalaba. Kama hilo halikusumbui ruksa. Kama vile kama hauoni tatizo kuvaa hijab ingawa ni mmisheni kwa nini ukataliwe kujiunga na shule inayoendeshwa na waislamu?

Huu ubaguzi mnaotaka kuuleta ni hatari mno. Utatufikisha pabaya maana watoto wetu hawatajuana kama tunavyojuana sisi.

Amandla.......
pole mkuu kuna shule nyingi tuu TZ za kikristo ambazo hazichukui waislam,marrian girls, visiga seminary, st francis na nyingine nyingi...na pia kuna baadhi ya shule za kiislam hazichukui wakristo mfano almuntazir..ila wahindu wanakubaliwa hapo...ukibisha na hapo basi tena
nashangaa unapokataa kuwa muslim Uni haijaletwa kwaajili ya kuendeleza muslims, mfano jinalenyewe na sheria inayo iestablish chuo ipo wazi
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom