naomba tuishie hapa, unaongea na mtu as if hawajui. siwabagui, ninawapenda waislam,nizaliwa magomeni, nimekulia magomeni, kuna mengi sana nayafahamu. ndugu zangu wengine wameolewa kwa mashehe wa kiarabu kabisa....wengine wamebadili dini kutoka ukristo kuwa uislam, na ninao hadi sasa hao ndugu wengine tuliokuwa wano tangu utoto. hivyo najua ninachongea.
cha msingi ni kwamba, jueni kuwa, ukianza kuwabagua wenzio ujue unatafuta na wewe kubaguliwa. hata hivyo to be frank, tz hatujafikia mahali pa kwua wadini kiasi hicho maofisini, pamoja na kwamba udini upo sana huko mtaani, na kwasababu ni nature ya kiumbe yeyote yule kubagua wasio wa kundi lake, tunatakiwa kufundisha watu wapunguze tu ubaguzi ila kuuacha kabisa haitakuja itokee kwasababu watu wanazaliwa na hiyo roho. pande zote mbili, wakristo na waislam, kuna element kadhaa, ili uishi vizuri tujitahidi kucontrol tukiheshimu wengine na kujua kuwa huwezi kulazimisha mtu dini asiyoitaka, na nchi hii ni ya kwetu sote na ni secular.