Kubwajinga
JF-Expert Member
- Jan 23, 2008
- 2,193
- 299
Udini hapa nautafsiri kuwa ni wingi wa watu wa dini moja kwenye ngazi fulani ya uongozi ukilinganisha na ngazi nyingine. Katika pita pita yangu na kuchunguza nimegundua kuwa asilimia 65.78 ya uongozi wa Kamati Kuu ya CCM ni watu wa dini moja. Kama udini ni wingi wa watu wa dini moja kwenye ngazi fulani, tunaweza kusema kusema kuwa Kamati Kuu ya CCM ina udini? Je kuna sababu yoyote ya msingi ya kwanini watu 25 kati ya 38 wawe ni wa dini moja? Je imeshindindikana kwa CCM kutafuta njia ya kuweza kugawa nafasi hizi kwa kuangalia uwiano wa dini?
Nikiwa mtu mwenye maslahi ya pekee kwenye CCM naona jambo hili si zuri na litazua manung'uniko yasiyo ya lazima. Kama kikundi, taasisi, au jumuiya fulani ina watu wenye sifa moja inayolingana, sifa ambayo inawatofautisha na watu wengine hasa ya vitu kama kabila, rangi, au dini basi mahali hapo ni pa kuangaliwa kwa karibu.
Katika siasa, tukitumia "Wangwe's Doctrine" kuwa endapo asilimia 50 ya watu wenye sifa hizo wakakutwa mahali pamoja ni ukabila/ukanda basi ni wazi mahali ambapo pana asilimia 65 ya watu wenye kulingana sifazao kutofautishwa na wengine basi napo patakuwa na tatizo, in this case udini (yaani idadi ya watu wa dini moja mahali pamoja ambayo haina maelezo ya kuridhisha).
Mkuu MJJ,
Sijasoma article yako iliyofilisika kiuchambuzi kama hii. Kama nia ilikuwa ni ku-dilute issue ya ukabila ndani ya CHADEMA kama ulivyoiita, the "Wangwe Doctrine", basi imekufanya uchemshe zaidi.
Nilipokupongeza kwa kutimiza posting 10,000 nilikushauri ujaribu kuondoa ideologies zinazokufanya uache kufikiria sawia, lakini naona inashindikana. Chambua mambo kama unaweza, la kama haiwezekani, mwachie Mushi ku-raise unqualified issues.