Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,391
- 39,484
2008-07-02 09:46:16
Na Simon Mhina
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Bw. Freeman Mbowe, amedai kwamba kinachotokea sasa hivi ndani ya CHADEMA ni mpango maalum wa kukiua chama hicho ili kisionekane katika uchaguzi mkuu 2010 na sio ruzuku inayotolewa na Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa nchini.
Akizungumza na Nipashe jijini jana, Mwenyekiti huyo alisema sio siri kwamba CHADEMA ni tishio kwa mafisadi, ambao wamejipanga vilivyo kutoa upinzani mkubwa kwenye uchaguzi huo.
Alisema kuna njama za kuidhoofisha CHADEMA kabla ya mwaka 2010.
``Wameshajua kwamba huenda janga la ufisadi likawa agenda kubwa sana katika Uchaguzi Mkuu ujao, na hakuna asiyejua kwamba CHADEMA ndio wameibua tatizo hilo na sisi na wabunge wetu ndio tumelishikia bango, sasa kuna njama inafanywa ya kufa na kupona kuhakikisha kwamba tunakosa nguvu,`` alisema.
Mwanasiasa huyo alisema sio siri kwamba tayari kuna watu ndani ya CCM hasa kundi la mafisadi, ambao tayari wameshaanza kupanga mikakati kwa ajili ya uchaguzi huo.
Alisema kwa madai haya hana maana ya kumtuhumu Makamu wake aliyesimamishwa kwamba anashirikiana na mafisadi hao, lakini ukweli kuhusu kila jambo, utafahamika.
``Na moja ya mkakati huo ni kuhakikisha kwamba kabla ya uchaguzi huo nguvu ya CHADEMA inapungua,`` alisema.
Hata hivyo, kiongozi huyo alionya kwamba hakuna mgawanyiko wowote ndani ya CHADEMA kama ambavyo baadhi ya vyombo vya habari vinashabikia.
Alisema ruzuku ya chama hicho inatumika kwa mlingano sawa mikoani kwa mujibu wa mahitaji na bajeti ya chama.
Bw. Mbowe, alitoa ufafanuzi huo, kufuatia madai kwamba ruzuku ya CHADEMA inaishia makao makuu na kwamba wale wanaohoji na kutaka isambae zaidi ili kujenga chama chao wanaonekana nuksi.
Mwenyekiti huyo alisema kwa kiasi kikubwa shughuli za makao makuu ya chama hicho, zinaendeshwa kwa kujitolea.
Alisema viongozi wa juu wa CHADEMA, akiwemo yeye, Katibu Mkuu na Naibu wake, wanafanya kazi kwa kujitolea.
``Mimi siku zote sijawahi kupokea mshahara wala posho kutoka CHADEMA, gari ninalotumia ni langu binafsi, dereva namlipa mimi kila kitu najihudumia mwenyewe. Vilevile Katibu Mkuu na hawa akina Zitto hawapokei malipo yoyote kutoka CHADEMA,`` alisema.
Bw. Mbowe, alisema yeye amekuwa akitoa fedha zake binafsi kwa ajili ya kukisaidia chama na wakati mwingine kukikopesha bila riba wala masharti yoyote, pale ambapo kinapungukiwa.
Aliwataka wanachama wa CHADEMA na wale wa kambi ya upinzani na viongozi wake, wasisononeke kutokana na kuchafuka kwa hali ya siasa ndani ya chama hicho, kwa vile hapakuwa na njia nyingine ya kusawazisha mambo.
Alisema hatarajii kwamba hatua ya Kamati Kuu kumsimamisha uongozi Makamu Mwenyekiti, Bw. Chacha Wangwe itazua mtafaruku wowote.
Alisema hatarajii hali hiyo kwa vile Bw. Wangwe, alishirikishwa katika hatua hiyo muhimu.
Bw. Mbowe, alisema hali ya CHADEMA imetulia na kuna mshikamano wa hali ya juu kati ya viongozi wote, vikao vya chama na wanachama.
Alisema wamelazimika kuchukua hatua hiyo, ili kusawazisha mambo ndani ya chama kabla ya uchaguzi mkuu ujao.
``Tulikuwa na wasiwasi na baadaye tumethibitisha kwamba kilichokuwa kinaendelea ndani ya chama lengo lake ni kudhoofisha CHADEMA katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2010,`` alisema.
Hata hivyo, Bw. Mbowe, alisema njama zozote za kusambaratisha chama chake hazitawezekana, kwa vile umma wa Watanzania umeshajua vita iliyopo mbele yao ya ufisadi, ambayo kwa kiasi kikubwa imeshikiwa bango na CHADEMA.
Makamu Mwenyekiti aliyesimamishwa, Bw. Chacha Wangwe, amekuwa akidai kwamba mbali na ruzuku, sababu nyingine ya kutoelewana na wenzake ni yeye kuhoji chama chao kutokuwa na sura ya kitaifa kutokana na nafasi nyeti kupeana watu wa mkoa mmoja.
My Take:
- Kwanini Chadema isiwalipe viongozi wake? Hicho chama siyo taasisi ya dini au NGO, huu mtindo wa kulipa fedha za wao wenyewe na wengine kutolipwa ni mtindo mbaya. Hata mtindo wa Mbowe kutoa fedha yake mfukoni kwa ajili ya Chadema siyo mtindo mzuri kwani unamfanya aonekane kama ana maslahi zaidi ya mtu mwingine. Chama kiendeshwe kama Chama. Hata kama chama hakiwezi kuwalipa inavyopaswa ni muhimu kuwa na token payment hata kama Shs. 10,000 kwa mwezi kwa viongozi lazima walipwe, wasifanye kazi za chama bure.
- Kama Bajeti ya Chama ni ndogo kuliko mahitaji yake, ni lazima wajifunze kufanya mambo ndani ya bajeti. Kama ni kuanzisha miradi n.k wafanye hivyo lakini wasifanye vitu ambavyo hawana uwezo wa kuvigharimia. Katika hili wanaweza kuanzisha miradi ya Chama. Hili linawezekana kwa kuanzisha kampuni ya Chama (Holding Company) na wanaweza kuangalia ni jinsi gani chama kinaweza kumiliki kitega uchumi. Kama mnapata karibu milioni 66 kila mwezi na fedha zote zinaishia kwenye matumizi na hazizalishi basi kuna tatizo la kiuwekezaji.
- Uongozi mkuu wa chama ujitoe kwenye kusimamia fedha na badala yake waajiri watu ambao wana weledi wa mambo ya fedha. Mhasibu Mkuu, Mkaguzi wa ndani, watunza fedha n.k na wataalamu wa Boharia. Wanasiasa wabakie kufanya maamuzi ya kisiasa. Na watumishi hawa walipwe kwa kiwango cha fani zao, na wasiwe na uhusiano wowote ule wa karibu na kiongozi yeyote wa juu wa chama hicho. Kabila, mkoa, rangi, au dini na jinsia don't count.
- Ruzuku ya Chama isipokelewe na kiongozi wa kisiasa, period. Fedha za ruzuku au fedha nyingine yoyote inaenda moja kwa moja kwenye akaunti ya chama na hesabu zake zinaeleweka na zinasimamiwa ipasavyo. Lazima waweke mfumo mzuri wa usimamizi wa fedha ili saa ya yoyote ijulikane wana fedha kiasi gani, ziko wapi, na zimetumika vipi.
- Viongozi wa kisiasa warudi kwenye kuimarisha chama, kwa kupika makada wa kisiasa, kufungua matawi ya chama n.k. Sikumbuki mara ya mwisho kusikia Zitto, Slaa, au Mbowe amefungua tawi la Chadema mahali popote ilikuwa lini. Chama hakijengwi kwa hotuba za Bungeni, au maneno ya magazetini, bali kwa kushawishi watu kukikubali na kuzielewa sera zake. Na njia pekee ya kuonesha kuwa watu wanawakubali ni watu kujiunga na chama hicho.
Madai kuwa watu wanaelewa kuwa Chadema inapigia kelele ufisadi zaidi n.k ni madai tu lakini ushahidi wa watu kuelewa unaonekana kwa watu kujiunga. Je tangia mambo ya ufisadi yaanze na tangia sakata la Zitto Chadema imejipatia wanachama wangapi, na kiasi cha watu kujiunga kina tofauti gani na kabla ya hapo. Kama hakuna tofauti kubwa na inayoonekana basi kuna tatizo mahali fulani.
Mengine.. nitawaandikia in private katika kulinda "heshima ya chama" chenu.