kwi kwi kwi,
labda ccm ni "chama cha wazanzibar" kama "chadema kilivyo chama cha wachaga" au "cuf kilivyo chama cha wapemba" kama wengine wanavyosema hapa.
Kama A
Kama idadi = 6
Kilichoangaliwa = majina
Kinachowaunganisha = Mkoa wa Kilimanjaro
Chama = Chadema
Hivyo = Ukabila sababu ya idadi tu;
Na B
Idadi 28
Kinachoangaliwa = majina
Kinachowaunganisha = dini
Chama = CCM
Hivyo = Udini sababu ya idadi tu;
Hivyo ndani ya Chadema kuna ukabila, ndani ya CCM kuna udini:
Lakini A inakubalika lakini B inakataliwa.
Kwani A iwe kweli na B iwe uongo wakati kinachoangaliwa ni kile kile majina na idadi na siyo factors nyingine zozote?
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com
press@ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425
Bi Kirembwe
Utakataa wewe lakini CCM ndiyo haswa nia yao baada ya kuona wanabanwa sasa lazima kutafuta njia za uongo .Ndiyo maana nimewahi kuonya hapa kabla kwamba kuna hii habari ya mahubiri ya ukabila kila na kusema ni NGO wanadhani sisi hatuoni .CCM ni mabingwa wa kuacha issue na kueneza uongo na sasa wame kwama.Tunaona majibu toka kwa wale wanao sema CCM ni Chama cha Umma na Chadema ni one man party .
Mwkjj,Sijali anayeniongoza ni nini kwa kadiri ya kwamba anakula kiapo cha kulinda na kuitetea Katiba yetu na anaongoza kwa misingi ya sheria zetu.
Bikirembwe.. point ambayo nimekuwa nikiiweka ni kuwa ukabila au udini si idadi ya watu. Ukiangalia idadi tu.. unaweza kuhukumu mambo mengi tu.. tribalism, sexism, and all the other isms out there. Mtu anapokubali ukabila Chadema kwa sababu ya idadi, hana budi kukubali mambo mengine vile vile, ndio maana wengine tunapinga hii sentiment ya ukabila, au udini kwa sababu ya idadi tu.
Binafsi sijali kina nanai wananiongoza as long as wamepata nafasi hizo freely, fairly, and transparently. Sijali anayeniongoza ni nini kwa kadiri ya kwamba anakula kiapo cha kulinda na kuitetea Katiba yetu na anaongoza kwa misingi ya sheria zetu. Mtu yeyote anayetaka kuleta hoja ya ukabila au udini kwa sababu tu idadi ya watu fulani haimpendezi na anashindwa kuonesha intellectual honesty ya kuangalia all logical explanation nawapinga.
Tusikubali kuangalia ukabila au udini kwa kuangalia namba, kwa sababu ukifanya hivyo tu mtu mwingine atakuja na namba nyingine na kudai kitu kingine.
I hope unapata point yangu.
Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com
Hivi kweli email ya ikulu ni ya Yahoo?? Mbona vituko.
Kubwajinga, hata mimi siamini macho yangu.
Sikiliza, hawa Wazee wetu ni incompetent wa kutupwa.
Ni hivi ndio nchi imekuwa ikiendeshwa karne zote hizi toka uhuru.
Ni siku hizi ndio tunaanza kushitukia madudu ya tunavyo run hii Jamhuri.
Majuzi tulishuhudia hoja ikipindishwa kwamba suala la Meremeta halipaswi kuzungumziwa na wabunge wa kitanganyika kwa kuwa ni la "usalama wa taifa". Je kuwaachia vijana wa silicon valley waratibu mazungumzo ya ikulu sio breach ya national security? Hiki ni kichekesho cha mwaka!!!!
... Incompetency ya kiasi hiki haistahili kuvumilika...
Tunataka feza irudi kama ni Chama cha kidini au cha kikabila ,hilo ni lao na chama chao wao ndio wanaochaguana na kupigiana kura na hizo ni siasa za ndani na jukumu la kukijadili chama ni la wanachama wenyewe wakae washauriane na kupata suluhu ,ila kwenye maslahi ya Taifa tutakiandama kama chama kinachotawala Nchi hii ya Tanzania Bara na Tanzania Visiwani ,na tutakiandama kwa maslahi ya taifa tutakua nae yule ambae anajali maslahi ya Taifa au kwa msemo wa siku hizi Maslahi ya Taifa ni nambari one , hivyo hata akija Baniani na kuyageuza maisha ya Mtanzania kuwa bora na ya kupigiwa mfano basi huyo ndie atakae kuwa Chaguo na hata akiwepo malaika na akawa anahujumu mali na hazina ya Taifa hili huyo atakuwa hatufai na ni adui japo yupo pembeni mwa bwana Mungu ,hivyo hao CCM hatuwatazami dini au kabila zao tunatazama wanachokifanya na kutenda juu ya Taifa hili huru lililo na utajiri wa kila fani kwa kila kigezo tutawahoji kutokana na maslahi ya Taifa na wananchi wake kama ndani yake wamo wanaolifisidi Taifa hili kwa maslahi yao binafsi basi hao ni maadui wa leo na kizazi kinachokuja wechilia mbali dini zao ,sisi wananchi hazituhusu kabisa kwani kila mtu atabeba mzigo wake ,hivyo tunawaandama CCM kwa vile wao ndio wapo kwenye usukani kuliendeleza Taifa hili wanapovuruga na kuona hawafai tutawashika mashati hata kama wamebeba tasubihi na misalaba au masanamu ,ili watueleze ilikwenda kwenda je hata hali ya nchi ikakumbwa na matukio ya wizi wa mabilioni na lini fedha hizi zitarudishwa na washiriki kutiwa hatiani ,haiwezekani mambo yaishe kwa kujiuzulu tu ,hilo halikubaliki katika kiwango cha kulinda maslahi ya Nchi , CCM ikiwa imeshindwa kuithibiti hali hiyo na kuachiana kwa kuwa ni watu wa dini moja au kabila moja au itikadi moja ,WaTanzania walio wengi hawatakubali hilo lipite tu hivi hivi na kila kukicha chemchem ya madi inakuja juu na siku ikilipuka basi maeneo yake ni kwenye ikulu zote za Tanzania Jumba la wabunge na vile vile kukisakama Chama cha CCM kiachie madaraka haraka iwezekanavyo ,itakuwa hakuna kulala kama mna udini ni wenu ndani ya Chama chenu wengine hayawahusu tunataka feza muirudishe. CCM jadilianeni wenyewe kuhusu chama chenu na jipangeni safu mtaklavyo halafu muwakamate wezi wetu warudishe vijisenti hivyo hivyo na umasikini wetu tutagawana kwa kila penye mahitajio.
Naona hii ndiyo thread pekee nitakayoanza kuchangia kwani hata MEGAPAYNE MWENYEWE KANIKARIBISHA HAPA!
Ndugu zangu kuna watu wananichongea ili nifungiwe hapa kwasababu ya kitendo changu cha kupinga hoja za udini na ukabila!
Sasa nimepewa warning...Na mimi nimemwomba mod huyo anipe list ya watu ambao hawataki nichangie thread zao ili kuepuka kufungiwa...Na kwa hivyo basi...Kuna watu kama Mafuchila na Megapayne na wengineo ambao najuwa hawana noma nikichangia mijadala hii bila matusi wala kwenda personal!
Once again nashukuru MegaPAYNE kwa ukarimu wako na pia sasa ni muda wa kujiandaa na NONDOZ ili kieleweke!
Pia kama kuna yule asiyetaka nichangie kwenye thread yake naomba ani PM kabla ya kwenda kunichongea ili nifungiwe.