Udhalilishaji aliofanyiwa Profesa Assad kwa maelekezo ya Ndugai ni wa kuhuzunisha sana

Kama vile Kuna kaukweli ndani Yake,!!

Paschal Mayala mbona hakupigwa picha alipoitwa Bungeni?

Mbona CAG kapigwa picha nyingi na video juu tangu anaingia Hadi anatoka?
 
Wengi walishaitwa kwenye hiyo kamati,


Mbona picha zao wakiwa wanakaguliwa mf, Wamevua mkanda,Viatu mbona hazionyweshwagi?

Kwanini huyu zimeonyweshwa bila kipingamizi?
 
Ndungai siku ya kufa Moroni utakuwa peke yako,

Hautakuwa na walinzi, Jiandalie Maisha mazuri ya Mbinguni.Acha drama za walimwengu
 
Mkumbuke TU kuwa siku ya kufa,

Motoni kila mtu atakuwa peke yake.

Hatakuwa na walinzi,

Jiandalie Maisha mazuri ya Mbinguni.

Acha drama za walimwengu
 
Huwa nakelwa na wazushi na wanaoandika vitu vya uongo . Wewe ulishawahi kuingia bungeni wakati wowote ule? Ulishawahi kusikia sakata la wabunge na mawaziri kugoma wasikaguliwe na mashine bungeni na liliishaje ? CAG ni mkubwa kuliko waziri wake anayevua mkanda ,viatu, saa nk na kukaguliwa ? Koma kuandika uzushi haukusaidii chochote .
Yaani ukiangalia wanavyomtweza CAG utasema ni Rais.Kila sehemu kuna taratibu zake, Huko bungeni huwez ingia tu bila kukaguliwa. Kwa waliowah hudhuria vikao vya bunge wanajua hili.Huku kwa watu wa kawaida kuna scanner mbili na unatoa kila kitu.Kwamba Asad ana excuse gani ya kutokaguliwa?

Nokia ya kitochi yuzingi jamii foramu
 
Nilianza kupata wasiwasi kuhusu mahusiano ya Proffesor na serikali pale alipotoa takwimu kisha baada ya siku moja akazikana.
 
Jana CAG alihojiwa na Kamati ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge. Kinachosikitisha ni namna ambavyo Prof. Assad alitendewa na ungozi wa Bunge. Nina taarifa za uhakika za maelekezo ya Ndugai yeye binafsi kwa walinzi na watendaji wa Bunge ya kumdhalilisha Assad. Mfano , kwa hadhi yake Assad alitakiwa kuingia viunga vya Bunge akiwa ndani ya gari, lakini jana alishushwa nje na kuingia kwa miguu. Pili, Ndugai alielekeza Assad akaguliwe kwenye mashine za usalama akiwa amevua viatu kinyume kabisa na utaratibu wa viongozi wakuu kuingia bila kupitia mashine za ukaguzi kwa hadhi yao.



Tatu, ndugai akatoa maelekezo kuwa Assad apigwe picha za kutosha akiwa ndani ya viwanja vya Bunge ili kuendelea kuonyesha Umma kuwa yeye ni mbabe. Na la kushangaza zaidi gazeti kama Mwananchi ambalo siku za nyuma lilikuwa na weledi linatumia picha ya Assad akiwa na kandambili katika ukurasa wake wa mbele kuendeleza udhalilishaji huo.

Ndugu zangu, CAG kikatiba ni nafasi muhimu sana, yeye ndiye anayeidhinisha pesa yote toka mfuko mkuu wa Serikali ( japo katika awamu hii Rais amegoma, na amevunja katiba), udhalilishaji huu anaofanyiwa Assad una baraka za Ofisi Kuu ya Nchi kwa nia ya kumuintimidate Assad hasa katika kaguzi zinazoendelea. Ndugai kutekeleza maelekezo ya IKULU bila tafakari ni aibu kubwa.

Nyie watu achene ujinga wa kuleta fyoko fyoko kila dakika. Mnamambo ya kufanya .Kila mtu maarufu akiitwa pale bungeni anapigwa picha.. Hoja zako zote ni dhaifu sana .Kupigwa picha hata kama angepigwa moja inatosha sana kuonesha kwamba amitikia wito. Harafu kusema kwamba apigwe picha nyingi ili ndugai aonekane mbabe ni uongo. .CAG mwenyewe tu aliitisha press ili kutuambia. Sasa sijui nini unachotaka ndugu yangu.

CAG kavaa ndala? Kwa hiyo spika ndio alomvalisha, embu tusijaze server la JF. Uhuru wa kujieleza ndio unatoka mashudu hivi kweli?


NB - Huu zi nimechangia kwa sasabu ya upuuzi tu.
 
Bora wewe uliyetuambia ukweli ulivyo.

Huwa nakelwa na wazushi na wanaoandika vitu vya uongo . Wewe ulishawahi kuingia bungeni wakati wowote ule? Ulishawahi kusikia sakata la wabunge na mawaziri kugoma wasikaguliwe na mashine bungeni na liliishaje ? CAG ni mkubwa kuliko waziri wake anayevua mkanda ,viatu, saa nk na kukaguliwa ? Koma kuandika uzushi haukusaidii chochote .
 
Hahaha kuna watu walitengeneza ukuta humu, niliwaambia Prof.Assad atauvunja aende kuhojiwa. Wakakataa wakasema eti wewe humjui Prof vizuri, hatokwenda.
Sasa kaenda na kahojiwa.
Kuna msemo humu kwamba hakuna mkate mgumu kwa chai. Kila mtu analinda maslahi yake. Asingeenda Magufuli ange mfukuza, mtasema hawezi, mara katiba hairuhusu. Mangapi yamevunja katiba na maisha yanaenda?! Nyie mnasoma saana katiba, wenzenu wanatumia ILANI yao. Mnapishana kila siku.
Best comment of the century

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom