Udhalilishaji aliofanyiwa Profesa Assad kwa maelekezo ya Ndugai ni wa kuhuzunisha sana

Huwa nakelwa na wazushi na wanaoandika vitu vya uongo . Wewe ulishawahi kuingia bungeni wakati wowote ule? Ulishawahi kusikia sakata la wabunge na mawaziri kugoma wasikaguliwe na mashine bungeni na liliishaje ? CAG ni mkubwa kuliko waziri wake anayevua mkanda ,viatu, saa nk na kukaguliwa ? Koma kuandika uzushi haukusaidii chochote .
Wewe ndio mpuuzi wa Mwisho, huyo unayesema waziri wa CAG ndio nani? Hao mawaziri si ndio wanatumbuliwa kila siku kutokana na report ya CAG? Acha kuandika upuuzi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugai anatumika vibaya, haya ni mambo ya kupita hapa duniani kwa hesabu ya haraka mtuma na mtumwa hakuna mwenye uwezo wa kuishi zaidi ya miaka 30 kwa sasa!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kudhalilishwa nintafsiri tu naamini kwa Prof kuvua biatu jambo la kawaida si huwa anenda swala tano hapo hawajamdhalilisha yeye bali wamejidhalilisha wao kwa kutokumpatia heshma yake kikatiba
Mkuu sioni udhalilishaji wowote hapo. Kukaguliwa ni suala la kawaida sana na wala katiba haijasema kwamba CAG asikaguliwe. Pale bungeni naambiwa ni wachache sana wasiokaguliwa.
Wabunge wote hukaguliwa na magari kunuswa
 
Jana CAG alihojiwa na Kamati ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge. Kinachosikitisha ni namna ambavyo Prof. Assad alitendewa na ungozi wa Bunge. Nina taarifa za uhakika za maelekezo ya Ndugai yeye binafsi kwa walinzi na watendaji wa Bunge ya kumdhalilisha Assad. Mfano , kwa hadhi yake Assad alitakiwa kuingia viunga vya Bunge akiwa ndani ya gari, lakini jana alishushwa nje na kuingia kwa miguu. Pili, Ndugai alielekeza Assad akaguliwe kwenye mashine za usalama akiwa amevua viatu kinyume kabisa na utaratibu wa viongozi wakuu kuingia bila kupitia mashine za ukaguzi kwa hadhi yao.

Tatu, ndugai akatoa maelekezo kuwa Assad apigwe picha za kutosha akiwa ndani ya viwanja vya Bunge ili kuendelea kuonyesha Umma kuwa yeye ni mbabe. Na la kushangaza zaidi gazeti kama Mwananchi ambalo siku za nyuma lilikuwa na weledi linatumia picha ya Assad akiwa na kandambili katika ukurasa wake wa mbele kuendeleza udhalilishaji huo.

Ndugu zangu, CAG kikatiba ni nafasi muhimu sana, yeye ndiye anayeidhinisha pesa yote toka mfuko mkuu wa Serikali ( japo katika awamu hii Rais amegoma, na amevunja katiba), udhalilishaji huu anaofanyiwa Assad una baraka za Ofisi Kuu ya Nchi kwa nia ya kumuintimidate Assad hasa katika kaguzi zinazoendelea. Ndugai kutekeleza maelekezo ya IKULU bila tafakari ni aibu kubwa.

Kaka inawezekana hujamfahamu vizuri Prof. Assad jamaa ana akili sio za nchi hii..kwa ufupi nikwambie ana makusudi yake na kamwe huwa hateteleki...na nina imani hata kamati wanalifahamu hilo na mazungumzo yao yalikuwa ya kawaida na sio ya kuonyana kama wengi wenu mlivyotarajia..na ndio maana kama mnakumbuka vizuri kwa wle waliosikiliza press conference ya mwisho aliyoifanya CAG juzi kabla ya kuhojiwa alisema kuwa kwa wakati ule asingejibu maswali yoyote atakuwa tayari kujibu maswali au kuongea baada ya kutoka kwenye kikao cha kamati ya maadili yaani jana.Hii maanake ni kwamba alikuwa amejiandaa endapo kamati nayo ingeleta pumba mezani kama alivvyokurupuka aliyewatuma basi angewapa vidonge vyao na baadae kumwaga manyanga jana hiyo hiyo lakini kamati nadhani kwa ushauri kitoka kwa few brains zilizobaki nchini walipikwa wakapikika mapema na wakaweza kuendesha kikao kwa adabu na ndio maana alipotoka hakuwa na neno
 
Jana CAG alihojiwa na Kamati ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge. Kinachosikitisha ni namna ambavyo Prof. Assad alitendewa na ungozi wa Bunge. Nina taarifa za uhakika za maelekezo ya Ndugai yeye binafsi kwa walinzi na watendaji wa Bunge ya kumdhalilisha Assad. Mfano , kwa hadhi yake Assad alitakiwa kuingia viunga vya Bunge akiwa ndani ya gari, lakini jana alishushwa nje na kuingia kwa miguu. Pili, Ndugai alielekeza Assad akaguliwe kwenye mashine za usalama akiwa amevua viatu kinyume kabisa na utaratibu wa viongozi wakuu kuingia bila kupitia mashine za ukaguzi kwa hadhi yao.

Tatu, ndugai akatoa maelekezo kuwa Assad apigwe picha za kutosha akiwa ndani ya viwanja vya Bunge ili kuendelea kuonyesha Umma kuwa yeye ni mbabe. Na la kushangaza zaidi gazeti kama Mwananchi ambalo siku za nyuma lilikuwa na weledi linatumia picha ya Assad akiwa na kandambili katika ukurasa wake wa mbele kuendeleza udhalilishaji huo.

Ndugu zangu, CAG kikatiba ni nafasi muhimu sana, yeye ndiye anayeidhinisha pesa yote toka mfuko mkuu wa Serikali ( japo katika awamu hii Rais amegoma, na amevunja katiba), udhalilishaji huu anaofanyiwa Assad una baraka za Ofisi Kuu ya Nchi kwa nia ya kumuintimidate Assad hasa katika kaguzi zinazoendelea. Ndugai kutekeleza maelekezo ya IKULU bila tafakari ni aibu kubwa.

Wewe utakuwa muislam liongo la kulalamika lalamika,
 
Ndugai kuyafanya hayo kuna dhihirisha Udhaifu wa Bunge lake.

Sasa anamdhalilisha CAG ili iweje? Ili aonekane mbabe zaidi ya ASSAD. Sawa akionekana Mbabe na Hana Akili itaashiria nini?

Bila shaka JOB anatoa amri zake kutoka juu na bila ya kufikiria ye anatenda tu. Nikisema JOB ni kuku wa kisasa Nitakua nimekosea?

Nchi inakata roho

Sent from my SM-J530F using Tapatalk
 
Back
Top Bottom